• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vituo vya reli ya Mombasa hadi Nairobi vyawavutia watu wengi

    (GMT+08:00) 2017-05-23 19:35:52

    Tarehe 13, mwezi wa Aprili, reli moja iliyotengenezwa na China iliendeshwa kutoka kituo cha Nairobi Kusini hadi kituo cha Mombasa Magharibi kwa kasi ya kilomita 110 kwa saa.

    Reli hiyo itaanza rasmi kufanya safari zake mwezi wa Juni mwaka huu.

    Hii ni picha ya vitu vilivyomo ndani ya behewa ya treni hiyo ambavyo vimesifiwa na wakenya kwa starehe na utulivu wa kuendesha.

    Mrembo huyu ni mfanyakazi mmoja wa treni hiyo.

    Kituo cha Nairobi Kusini kimebuniwa kama daraja la urafiki kati ya China na Kenya. Pia kitakuwa ishara ya mji wa Nairobi.

    Wafanyakazi wa China na Kenya wanasaidiana kukamilisha ujenzi wa reli hiyo.

    Vifaa vya ukaguzi wa usalama pia viko tayari kutumika.

    Njiani, abiria wanaweza kuona treni.

    Mfanyakazi anasafisha dirisha

     

    Mfanyakazi wa China anajionea fahari kwa ujenzi huo.

    Umbo la Kituo cha Mto Athi ni kama mlima.

    Kituo cha Emali kimebuniwa kwa umbo la ngumi ambayo inamaanisha mshikamano wa makabila.

    Kituo cha Kibwezi kimebuniwa kutoka majani ya mti.

    Ubunifu wa Kituo cha Mtito Andel unafanana na mlima Kilimanjaro.

    Kituo cha Voi ni kama "V" ambayo inamaanisha mafanikio (Victory) pia ni "V"oi

    Kituo cha Miaseni kimebuniwa kutokana na pundamilia na uchoraji wa kijadi katika mwili.

    Ubunifu wa Kituo cha Mariakani ni kama mianzi

    Kituo cha Mombasa kimebuniwa kutoka mnara wa taa na mawimbi

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako