• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaendelea kutekeleza ahadi ya FOCAC kwa kujenga Bandari Tanzania

    (GMT+08:00) 2017-05-25 09:30:13
    Na Theopista Nsanzugwanko, Beijing

    Mwaka 2015 kulifanyika mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika (FOCAC) katika mji wa Johannesburn Afrika Kusini.

    Katika mkutano huo, Rais wa China Xi Jinping alihaidi nchi yake itatoa dola bilioni 60 kufadhili miradi ya maendeleo barani Afrika, katika mipango ya nchi yak kwa nchi za Afrika wenye vipengee kumi wa taifa lake barani Afrika akisema anataka kujenga uhusiano wa haki na washirika walio sawa.

    Alisema fedha hizo ni kwa ajili ya kuangazia mambo matatu yanayoaminika kuirejesha Afrika nyuma kimaendeleo, ambayo ni masuala ya, miundo mbinu, ukosefu wa wataalamu walio na ujuzi mbali mbali na ukosefu wa fedha za kuendeleza miradi hiyo.

    Alisema fedha zitakazotolewa zitajumuisha dola bilioni tano ya mikopo isiyokuwa na riba na dola bilioni 35 ya mikopo ilio na mashrti nafuu itakayotolewa kwa Afrika.

    Tangu mwaka huo,kumekuwa na miradi mbalimbali nchini Tanzania ikifadhiliwa kwa kutumia fedha hizo ambazo tayari zimeanza kutolewa katika nchi mbalimbali za Afrika.

    Wiki hii, Tanzania ilipata taarifa za ujenzi wa bandari muhimu kwa maendeleo ya nchi na ukanda wa Afrika Mashariki baada ya jopo la waliopewa dhamana ya kusimamia fedha hizo nchini China kusema wako tayari kuto fedha kwa ajili ya ujenzi wa Bandari ya Mwambani mkoani Tanga na kuwa ya kisasa.

    Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, Prof Makame Mbarawa hivi karibuni baada ya kukutana na jopo hilo katika mji wa Beijing China,mara baada ya kumalizika kwa mkutano mkubwa wa Ukanda Mmoja na Njia Moja ambao Waziri huyo alihudhuria.

    Mbarawa anasema baada ya kukutana na wanaosimamia Fund wameonyesha nia kuwekeza katika bandari ya Mwambani Tanga na kusema wako tayari kujenga bandari hiyo kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi.

    "Kwa sasa wanachotaka ni kujua mipango ya serikali kama tunaenda kwenye mfumo wa PPP au mfumo wa aina gani lakini wao wako tayari kwa ajili ya ujenzi huo" anasema.

    Anaweka wazi kuwa katika mipango ya serikali wataangalia mfumo mzuri na kutafuta mwekezai ili kujenga badari hiyo muhimu kukuza uchumi wa nchi.

    Anasema katika kuhakikisha nchi ya Tanzania inaendelea kufunguka katika fursa ya usafirishaji hasa usafiri wa Ndege kutoka Tanzania hadi China serikali imejikita kumaliza tatizo hilo kwa miaka mitano ijayo.

    Anasema kwa kutumia ndege aina ya "Boeing 787 Dreamliner" inayotarajia kuwasili nchini hivi karibuni watatatua tatizo la usafiri lililopo katika nchi za Ulaya na miji mikubwa ya Guangzhoe, Beijing na shaghai.

    Anasema lengo la kuanzisha safari hizo ni kuondoa usumbufu uliopo sasa ambao mtu analazimika kwenda nchi za ulaya kasha kufika China au kwenda Tanzania sasa safari hizo zitakuwa maalum kwa ajili ya kuleta watalii na kukuza biashara katika miji hiyo huku katika bajeti ya mwaka huu wametenga fedha taklibani bilioni 500 ili kununua ndege nyingine kubwa kama hiyo.

    "Serikali imejipanga ili kuhakikisha katika kipindi kifupi cha miaka mitano shirika la ndege Tanzania (ATCL) linafufuka ili hasa kukuza sekta ya utalii na biashara iweze kukua, kwani tunaamini ukiwekeza katika sekta ya anga mbali na mapato yalakini sekta nyingine pia zinakua" anasema.

    Waziri Mbarawa anasema ukinunua ndege lazima kuboresha na viwanja kwani haitakuwa na maana ukiwa na ndege huku hauna viwanja hivyo serikali imejipanga kutengeneza viwanja vyote vya ndege nchini.

    Alisema upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuwa na Terminal III unaendelea vizuri huku kiwanja cha Ndege Mbe ujenzi wa jengo la Abiria ukiendelea huku Mwanza ujenzi wa jengo la Abiria na kuongeza urefu wa Kiwanja.

    Anataja viwanja vingine vilivyo katika hatua mbalimbali za ujenzi ni kuongeza Urefu wa kiwanja cha Ndege Dodoma,huku wiki mbili zilizopita wametangaza Zabuni ya ujenzi kiwanja cha Shinyanga na kiwanja cha Sumbawanga wakitafuta Mkandarasi.

    Anasema kiwanja cha Ndege cha Kigoma Mkandarasi yupo site na katika bajeti ya mwaka huu watakarabati viwanja vya ndege vya Iringa, Musma na Songea ili ndege zituo katika viwanja vyote na kuchangia ukuaji wa uchumi.

    Tanzania imechaguluwa na China kuwa miongoni mwa nchi nne zikiwemo Kenya, Ethiopia, Jamhuri na Kidemkrasi ya Congo (DRC) ambazo China itahamishia viwanda vyake ikiwa ni mkakati wa kukuza uhusiano wa Kihistoria uliopo baina ya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako