• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wachina Waadhimisha tamasha la Duanwu

    (GMT+08:00) 2017-05-31 09:18:33
    By Eric Biegon katika Beijing, China

    Wachina wanaadhimisha sherehe ya siku tatu kwa kuandaa tamasha la Duanwu maarufu kama Dragon Boat Festival. Tamasha hili linaandaliwa kukumbuka mshairi mkubwa tajika ambaye alipigana dhidi ya mateso ya raia maelfu ya miaka iliyopita.

    Kama wasomi wengi wa fasihi hufanya leo, Qu Yuan aliandika mengi kuonyesha upendo wake na kujitolea kwa nchi yake. Shairi zake hata hivyo yasemekana yalikosoa vikali utawala wa kukandamiza. Matendo yake yalivutia hasira kutoka uongozi wakati huo ambao uliamua kumpeleka uhamishoni.

    Lakini Qu, hakukubali uamuzi huo, badala yake akachagua kuzama mwenyewe katika mto badala ya kuishi kuona nchi yake ikizama. Kifo chake kimekuwa kikiadhimishwa tangu wakati huo. Ametajika kuwa mshairi mkubwa zaidi kuwahi kutokea katika historia ya China.

    Tamasha hili limepata jina lenye kutokana na mashindano ya mashua ambayo ni maarufu katika kipindi hiki. Muda mfupi baada ya kuchipuka kwa taarifa ya kujuia kwa Qu, wafuasi wake mara moja walizindua shughuli za uokozi kwa kutumia boti bila mafanikio.

    Wakati jitihada hizo ziliambulia patupu, wao walianzisha shughuli ya kulinda mwili wake kutoliwa na viumbe vya majini. Wao waliendesha boti zao kuzunguka eneo alikotumbukia kuwafukuza wanyama hao mbali.

    Aidha walitayarisha wali, ambayo wao walitupa ndani ya mto kama sadaka ili kutuliza viumbe majini kutokula mwili wa Qu.

    Hii inaeleza ni kwa nini wakati wa tamasha hili la Duanwu, wachina wanaandaa aina ya mchele, maarufu kama Zongzi, kama desturi. Zongzi ulio na umbo la piramidi, ni mchele uliofungwa katika majani ya mwanzi kabla ya kupikwa. Mchele huo unaongezewa ladha kupitia matumizi ya vijazi tofauti kama vile maharage tamu, nyama, na yai pingu na kadhalika

    Maarufu kwa mashairi yake, Qu amehamasisha vizazi ambavyo vimekubali na kuendeleza ujuzi wake na sanaa.

    Katika mji mkuu wa Beijing, idadi kubwa ya maonyesho yalifanyika katika siku ya kwanza ya sikukuu ya kusherehekea tamasha hilo.

    Kwenye ukumbi wa Beijing Folk Custom Museum, kwa mfano, viongozi na wasanii walikusanyika kuzungumzia watu na kuwaongoa waliojitokeza kwa ajili ya tukio hilo kwa mtiririko huo.

    Lakini hawakufika hapa kwa mavazi ya kawaida. Wote walivaa vazi maalum kwa jina "Hanfu", ambayo ni nguo ya jadi ya kitamaduni ya Kichina.

    Baadhi ya viongozi waliofika hapa waliwarahi Wachina kuendelea kufanya kazi kuelekea kujenga jamii yenye mafanikio kiasi.

    Maono ya rais wa China Xi Jinping wa utekelezaji kanuni elekezi ya Chama cha Kikomunisti na kuendeleza ujamaa na ishara maalum ya Kichina yalisheheni vizuri katika hotuba zao.

    Rais Xi amedumisha muda baada ya mwingine kuwa juhudi ya nchi nzima umeonyesha kuwa ujamaa tu ndio unaweza kuokoa China na kwamba ujamaa na ishara maalum za Kichina zinaweza kuwawezesha Wachina kuendelea wenyewe.

    Baada ya hotuba mbalimbali, ilikuwa ni fursa ya kufurahia maonyesho kutoka kwa makundi mbalimbali. Kama ilivyo desturi, katika muda wa siku tatu, watu wa China wanatumia fursa hiyo kuonyesha urithi wao na upendo wao wa kina kwa utamaduni wao.

    Shughuli kama vile uchoraji na Kaligrafi yalipewa kipaumbele. Kisha kulikuwa na sherehe ya chai, uchongaji mbao, maonyesho ya desturi ya Hanfu, upigaji mishale ya jadi, mapambo ya fundo, kukata karatasi, uchongaji udongo, uzoefu wa kutengeneza shanga miongoni mwa wengine.

    Baadhi ya maonyesho ya Opera pia zilisheheni wakati wa maadhimisho haya ya siku nzima.

    Wengine hata hivyo wanaamini kwamba tamasha hilo la Duanwu linafanyika ili kufanya ibada kwa joka. Kwa maoni yao, tukio hili ni muhimu tu kwa kuwa Wachina wanaamini ni wana wa joka.

    Yote pamoja, tamasha hili hata hivyo imeenea zaidi ya fikra na mawazo hizi kinzani. Wakati Wachina wanaadhimisha Duanwu kuonyesha na kukuza utamaduni wao tajiri, tamasha hili haliandaliwi na Wachina pekee.

    Mbio za mashua zimekuwa matukio ya kimataifa. Michezo hii kwa sasa ni maarufu katika Afrika, Marekani, Canada, Ulaya, Australia, Taiwan, Hong Kong, Singapore miongoni mwa nchi nyingine.

    Kwa wengi, tamasha ili limetoa nafasi murwa ya utalii si tu kwa China bali pia kwa mataifa ambayo tamasha hilo uandaliwa kila mwaka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako