• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kituo cha mradi wa uchunguzi wa miali ulimwengu chaanza kujengwa nchini China

  (GMT+08:00) 2017-06-05 16:20:53

  Kituo cha mradi wa uchunguzi wa miali ulimwengu kutoka urefu mkubwa kutoka usawa wa bahari LHAASO kimeanza kujengwa mwezi Julai kwenye mlima Haizi wenye urefu wa mita 4,410 kutoka usawa wa habari mkoani Sichuan China. Mradi huo ukimalizika unatazamiwa kutafiti chanzo cha miali ulimwengu.

  Miali ulimwengu ni vyembe vyenye nishati kubwa kutoka anga ya juu, ni njia ya pekee kwa binadamu kukusanya sampuli kutoka nje ya mfumo wa jua.

  Mwanasayansi mkuu wa mradi huo Bw. Cao Zhen amesema utafiti wa miali ulimwengu ni njia muhimu ya kutafiti mabadiliko ya ulimwengu. Tangu miali ulimwengu ianze kugunduliwa mwaka 1912, wanasayansi walioitafiti wamepata medali nyingi za tuzo ya Nobel, lakini hadi sasa binadamu bado hawajagundua chanzo cha miali hiyo.

  Bw. Cao amefahamisha kuwa kituo cha LHAASO kitaundwa na sehemu tatu. Sehemu ya kwanza ni bwawa lenye ukubwa wa mita elfu 80 za mraba na kina ya mita 5, ambalo litatumiwa kukusanya photon za Gamma kutoka vitu vya angani viliyoko mbali sana, kama vile shimo jeusi lililoko umbali wa miaka milioni 300 ya kusafiri kwa mwanga kutoka dunia yetu. Sehemu ya pili yenye ukubwa wa kilomita 1 ya mraba ina vyombo 5200 vya kuchunguza vitu vinavyometameta na vyombo 1200 vya kuchunguza Muon vitakavyowekwa mita 2.5 chini ya ardhi. Sehemu ya tatu ina mifumo 12 ya darubini. Sehemu hizo tatu zitaunda mfumo mkubwa wa uchunguzi wa miali ulimwengu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako