• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya kutafuta fursa ya biashara zaidi na China kupitia mpango wa Mkanda Mmoja Njia Moja

  (GMT+08:00) 2017-06-09 10:18:34
  Na Eric Biegon mjini Beijing, China

  Nairobi imetangaza kuwa itaanza kuwinda nafasi za biashara zaidi na Beijing kupitia mpango wa kiuchumi uliozinduliwa karibuni wa Mkanda Mmoja Njia Moja. Waziri wa biashara na viwanda wa Kenya Adan Mohamed anasema mfumo huu unaofuata barabara ya kale ya Silk ambao una mizizi yake China utahusisha matrilioni ya dola ya uwekezaji na miradi mikubwa muhimu katika kila moja ya nchi husika.

  Waziri huyo anasisitiza kuwa Kenya na Afrika kwa jumla itafaidika sana kutokana na kuwa na uhusiano na mataifa yenye uchumi kubwa duniani kama vile China, huku akitoa mfano wa miradi mikubwa ambayo hadi sasa imekamilika chini ya mpango huo.

  "Muunganisho ni muhimu. Kwa upande wetu, tunaona miradi kama vile reli ya kisasa ya SGR pamoja na upanuzi wa bandari ya Mombasa kama muhimu, ambapo kuna uwezekano wa mkondo wa bahari kutia nanga kutoka mataifa ya dunia kabla ya kupenyeza kote barani Afrika." Waziri alisema.

  Mohamed, ambaye alikuwa sehemu ya ujumbe ambao ulihudhuria kongamano la Mkanda Mmoja Njia Moja mwezi uliopita mjini Beijing, anasema mpango huu ni wa kihistoria hasa nchini Kenya kutokana na kwamba Mombasa imekuwa kitovu kwa bidhaa zitakazoingia Afrika.

  "Hakika ni mradi wa ushawishi wa kiuchumi ambao utaleta mabadiliko makubwa kwenye miundombinu si tu nchini Kenya na Afrika, lakini duniani." Yeye alisema.

  Kuwa sehemu ya mfumo huu, waziri huyo wa biashara na viwanda alifichua kuwa Kenya itatumia fursa hiyo kupanua biashara na China na mataifa mengine yenye uchumi kubwa ambayo hadi sasa wamejiunga katika mpango huo.

  Waziri huyo anasema kwa muda mrefu, kwa mfano, Kenya haijakuwa na utaratibu wa biashara huru na China, huku akifichua kwamba urari wa biashara kati ya Beijing na Nairobi imeegemea taifa hilo lililoko mashariki ya mbali. Anasema mpango wa OBOR utawezesha nchi zote mbili ili kujadili biashara na jinsi ya kufungua soko la China hususan, kwa bidhaa kutoka Kenya.

  Kuboresha biashara kwa kuunganishwa biashara, Waziri huyo alidokeza kuwa mpango unaendelea utakaohakikisha kuwa ndege nyingi zitafanya safari ya moja kwa moja kutoka Kenya kuingia sehemu mbalimbali za China. Chini ya mpango huo, Mohamed anasema Kenya inataka hasa safari za moja kwa moja za Kenya Airways hadi mji mkuu Beijing, lakini akakiri bado kuna mengi ya kutekelezwa na Kenya.

  "Baada ya muda, tunahitaji kuimarisha ushindani wetu kuwa na uwezo wa kuingia masoko kama China. Lakini hatua ya kwanza ni kuwa na mfumo wa biashara wenye utaratibu huru na China ambayo imekuwa ni ndoto kwa muda mrefu. "

  Kwa mujibu wa Mohamed, Kenya kwa sasa ni inatazamia China kama "taifa moja ambalo tunataka kusafirishia bidhaa zetu ya kuingia mataifa ya nje. Kwa muda mrefu sasa, kumekuwa na wasiwasi Kenya kuhusiana na hatari ya kufungua soko la Kenya kwa China bila kulipa ushuru wowote. Kwa maoni ya waziri huyo, hofu hii inatokana na dhana kwamba China, kutokana na ukubwa wake na kwa sababu ya kitengo chake cha gharama, ambayo ni ya chini sana kuliko katika sehemu yoyote ya dunia, inaweza kwa urahisi kuwa soko ambayo tu itasambaza bidhaa zake katika Afrika Mashariki.

  Licha ya tahadhari hii, waziri huyo wa viwanda anasema China haiwei kupuuzwa tena katika suala lolote inayogusia juu ya biashara.

  "Lazima tuhakikishe kwamba tunakuwa na ushindani wenyewe kama njia ya kurahisisha njia yetu ya kufikia soko hili muhimu." Alisema.

  Mohamed aliweka wazi kuwa Kenya sasa ina mpango wa kuboresha mauzo ya nje yake katika China jinsi ambayo imekuwa ikifanya katika maeneo mengine ya dunia. Kwa maoni yake, Kenya inakusudia kutumia mfumo huu maarufu OBOR kuhakikisha Kenya inapata mafanikio ya hali ya juu.

  Miongoni mwa mambo mengine, mpango huu wa Mkanda Mmoja Njia Moja inataka kujenga uchumi wazi, kuhakikisha biashara huru na umoja, pamoja na kupinga kila aina ya ulinzi wa soko. Kama sehemu ya mkakati wa ushirikiano, marais 30 na viongozi kadhaa wa taasisi kubwa duniani ambao walikutana wakati wa kongamano la BRF Beijing walizungumzia haja ya kuweka kipaumbele mashauriano ya sera, kukuza biashara, kuunganishwa kwa miundombinu, ushirikiano wa kifedha na ubadilishanaji wa watu-kwa- watu.

  Katika tamko lao la pamoja baada ya mkutano, viongozi hao waliazimia kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara na kuunga mamlaka na ufanisi wa mfumo wa biashara pamoja na kukuza biashara na uwekezaji huria na uwezeshaji.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako