• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wafanyabiashara wa Tanzania walioko China watangaza mikakati ya uwekezaji zaidi

    (GMT+08:00) 2017-06-15 08:44:59
    Na Theopista Nsanzugwanko, Beijing

    TANZANIA na China imekuwa na mahusiano ya muda mrefu katika sekta mbalimbali ikiwemo uhusiano wa Kidplomasia, kiuchumi, kisiasa lakini kubwa zaidi ni kibiashara ambapo kuna watanzania wanaofanya baishara nchini China.

    Kutokana na mahusiano hayo Tanzania ni nchi mojawapo kati ya nchi nne za Afrika zilizohusishwa katika pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja iliyoundwa na Rais wa China Xi Jinping mwaka 2013 kwa ajili ya kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katiaka Nyanja tofuati ikiwemo biashara.

    Inakadiliwa kuwa biashara baina ya nchi hizo mbili zimefikia zaidi ya dola bilioni tano. Katika kuhakikisha wanadumisha ushirikiano huo,watanzania wanaoishi na kufanya biashara katika miji mbalimbali nchini China wameanzisha Tanzania Chamber of Commerce in China china (TCCC) itakayosaidia kuhamasisha uwekezaji Tanzania pamoja na kuweka mikakati na kuwekeza China.

    Umoja huo uliopo katika hatua za awali kupata usajili inawashirikisha watanzania waanzilishi zaidi ya 20 wanaofanya biashara halali na kusajiliwa kulipa kodi nchini China.

    Makamu Mwenyekiti wa TCCC, Abraham Merishani anaeleza kuwa suala la kuandaa katiba linaendelea na liko katika hatua za mwisho huku wakiwa na uhakika kuwa mwezi ujao watakuwa wameishapata usajili. Anasema lengo la umoja huo ni kwa ajili ya masuala ya biashara baina ya nchi hizo mbili na kuhakikisha wanakabiliana na changamoto zote kwa wafanyabisahra wa pande zote mbili.

    "Tuko katika hatua ya kuandika katiba na kusajili na kufikia mwezi ujao tutakuwa tumekamilisha taratibu zote za kutambulika kisheria nchini hapai "anasema.

    Anaweka wazi kuwa kuanzishwa kwa umoja huo kumetokana na ushauri wa Balozi wa Tanzania nchini China ,Mbelwa Kairuki aliyefika na kukutana na wafanyabishara wa kitanzania na kuwata kuunda umoja huo kwa maslahi ya nchi zote mbili.

    Anasema katika waanzilishi wengi wamezaliwa Tanzania lakini sasa wanaishi na kufanya biashara nchini China,tena wakiwa wamewekeza kwa kuanzisha viwanda hivyo wanajua mazingira ya nchi zote kwa kuangalia namna ya kuwezesha uwekezaji na biashara.

    Anasema umoja huo utasaidia kutoa elimu kwa wamewekezaji wanaotaka kuwekeza nchini pamoja na watanzania wanaotaka au wanaofanya biashara kukabiliana na changamoto mbalimbali, ikiwemo sheria na taratibu za kufuata kwa nchi husika.

    "Pia tutakuwa voice kwa wafanyabiashara wa pande zote katika kujenga mahusiano kwa kueleza taasisi husika pale inapotokea changamoto katika uwekezaji kama kutambua wawekezaji halali, mishahara kwa wafanyakazi baada ya kuwekeza na mengineyo katika kuhakikisha kila nchi inanufaika kutokana na uwekezaji na biashara.

    "Katika umoja wetu, Pia tuitaweka mikakati ya uelewa masuala mbalimbali ya teknolojia yanayotakiwa nchini na kusaidia katika sekta mbalimbali kama kilimo kwa kulima na kufanya biashara ya mazao yanayohitajika nchini China" anaeleza.

    Anasema watahakikisha wanatafuta masoko ya uhakika kwa ajili ya kuwainua watanzania ambao bila kuwa na sehemu kama hiyo wanaweza kukutana na wateja ambao siyo waaminifu na kudhurumiwa.

    Merishani anasema watahakikisha wanawakusanya watanzania waliopo China kujiunga kwa pamoja na kuweka mikakati ya pamoja ya kufungua maeneo ya uwekezaji kwa kutumia Teknolojia mbalimbali za China kuliko kuwekeza mmoja mmoja kama wanavyofanya sasa.

    "Ndoto ni kuhakikisha watanzania wa China wanawekeza katika maeneo kama ujenzi wa Hospitali ya Kisasa itakayomnufaisha kila mtanzania au kufungua "Industry Zone" ambayo itatoa ajira kwa watanzania"anasema

    Lakini pia kusaidia serikali katika kuwabaini wawekezaji wa kweli au walio wa uongo au wababaishaji kwa kutumia jumuiya hiyo ambyo wengi wao wameoa na kuwa na familia nchini china kupata wawekezaji halisi ambao wanabadilika na kuanza kuuza bidhaa ndogo ndogo Kariakoo. Merishani anasema pia watasaidia katika masuala mbalimbali ikiwemo kujenga mahusiano katika jamii ili kuwe na mwingiliano mzuri baina ya watanzania na Wachina katika kufanya biashara.

    "Tutasaidia kukabiliana na kutoelewana kutokana na tofauti za tamaduni kwani tofauti nyingi siyo za kibiashara bali kutoelewana kitamaduni hivyo katika umoja wetu tutakuwa tukitoa elimu kwa wafanyabiashara wa kitanzania wanaokuja China kwa kutumia makongamano na majarida mbalimbali" anasema.

    Anazungumzia udhibiti wa bidhaa zizizo na ubora zinazotoka China kuingia nchini, anasema kwanza ni vema kutambua kuwa wafanyabiashara wa kiafrika wakiwemo Tanzania ndiyo wanaotaka bidhaa hizo zisizo na ubora kwa lengo la kupata faida.

    Merishani lakini anaweka wazi kuwa kipindi cha bidhaa hizo kuingia Tanzania kinaisha kwani ilikuwa ni kipindi cha mpito tu ambacho hata China wenyewe wamepitia kwani sasa wananchi wamekuwa makini wanafahamu bidhaa hizo hivyo wafanyabiashara wamekosa soko na sasa na kupunguza kuagiza viwandani.

    "Ni lazima kukubaliana kuwa usimamizi mbovu wa kukagua bidhaa ulisababisha kuingia kwa wingi,hivyo kwa kutumia umoja huu tutashauri serikali kuhakikisha tatizo hili linakwisha kabisa" anasema.

    Anaeleza kuwa kwa bidhaa kama vile za umeme watu walizoea kununua kwa kuangalia majina wakifikiri ndiyo ubora jambo lililofanya wafanyabiashara kuanza kutengeneza zenye ubora usiokidhi viwango lakini sasa watu wameacha kununua bidhaa kwa majina bali wanazingatia ubora.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako