• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yasema mpango wa Ukanda Mmoja na Njia Moja ni njia rahisi ya kusaidia nchi wanachama

  (GMT+08:00) 2017-06-15 13:26:57
  Na Eric Biegon mjini Beijing, China

  Beijing imesisitiza kuwa mpango wa kiuchumi wa karne ya 21 wa Ukanda Mmoja na Njia Moja ni mfumo bora mno ambayo China itatumia kutoa msaada wake kwa nchi zinazoendelea ambazo zimeamua kushirikiana na taifa hilo lenye uchumi mkubwa zaidi barani Asia.

  Waziri wa mambo ya kigeni wa China Wang Yi anasema Jamhuri ya Watu wa China itatumia jukwaa hilo kushiriki mafanikio yake na mataifa marafiki, huku akiweka wazi kuwa nchi yake itatoa misaada yote itakayohitajika kwa mataifa ambayo tayari wamejiunga na mpango huo wa mabilioni ya dola.

  "Tunataka kubadilishana uzoefu wetu wa maendeleo na nchi nyingine ili wapate kutambua ukuaji wao wa uchumi na maendeleo bora kwa kasi." Bwana Wang alisema.

  Akizungumza wakati wa maonyesho ya mkoa wa Jilin mjini Beijing, waziri huyo wa kigeni alisema kuwa chini ya mpango huo wa Ukanda Mmoja na Njia Moja, mataifa yatapata fursa dhabiti na ya kweli ya ushirikiano.

  Kwa maoni yake, watakaofaidi zaidi kutokana na mpango huu ni mataifa yanayoendelea barani Afrika ambazo kwa muda mrefu yameshuhudia miundombinu mbovu na hafifu, ukosefu wa fedha kwa ajili ya miradi ya msingi na kukosa ujuzi wa kutosha kufanikisha ajenda zao za kiuchumi.

  Akipongeza mpango huo kama moja ambayo itatoa fursa ya usawa kwa nchi wanachama na taasisi, Wang alizirai nchi ambazo hadi sasa zimewakilishwa katika mpango huo kuzungumzia kwa uwazi maeneo ambayo wangependa China iweze kuingilia kati.

  "Tunatoa wito kwa wote watoe mapendekezo kuhusu jinsi ya kushirikiana. Tunawaomba wazungumze na sisi. Tunataka wabadilishane mawazo yao na sisi, nasi pia kwa furaha tutachukua hatua juu yao na kuyatekeleza." Wang alisisitiza.

  Katika hotuba yake wakati wa kuzilizinduliwa rasmi kwa mfumo huo mwezi uliopita mjini Beijing, rais wa China Xi Jinping alisema harakati za mpango huu "inatokana na ushauri na mazungumzo ya kina na faida zake kufaidi sisi wote."

  "Tunapaswa kujenga Mkanda Mmoja Njia Moja kama barabara ya mafanikio. Maendeleo ni muhimu kwa kutatua matatizo yote. Tunapaswa kuzingatia suala la msingi la maendeleo, tutoe uwezo wa ukuaji wa nchi mbalimbali na kufikia ushirikiano wa kiuchumi wa pamoja na kutoa faida kwa wote. "Akasema Rais Xi.

  Mwanachama wa kamati Kuu ya chama cha Kikomunisti cha China Bayanqolu aliilimbikizia sifa mpango huo maarufu kama OBOR akiutaja kama mradi mkubwa ambayo utasaidia katika utunzaji na kushughulikia masuala ambayo yanakabili dunia kwa sasa. Alisema haya yote yatawezekana kupitia mkakati wenye sura tano kama uliyoratibishwa na waandaaji wa mpango huo.

  Bayanqolu alisema dhamira ya pamoja ya kujenga uchumi wa wazi, kuhakikisha biashara huru na umoja, kuzuia aina zote za ulinzi wa biashara huru, yataafikiwa kupitia uratibu wa sera imara, kuunganishwa kwa miundombinu na vifaa, kutolewa kwa misaada ya kibiashara, ushirikiano wa kifedha na mahusiano ya watu-kwa-watu baina ya mataifa husika.

  Gavana wa mkoa wa Jilin Liu Guozhong alisema mfumo huo ulizindua kwa wakati bora zaidi. Gavana huo alidokeza kuwa mkoa wake tayari imeratibu baadhi ya maeneo ambayo inataka kutumia ili kuingiliana na dunia ya nje.

  "Sisi tunaunganika vizuri katika mfumo huu wa Mkanda Mmoja Njia Moja. Tunataka kutoa mchango wetu pia." Akasema bwana Liu.

  Kupitia sifa yake ya kumiliki mashamba makubwa ya mchele, mkoa wa Jilin imetambuliwa kote duniani kutokana na mchango wake wa kisasa kwa kilimo. Gavana Liu anasema ni mbinu hii bora ndio mkoa wake unataka kushirikisha dunia.

  Mbali na mashamba yake ya mchele, Jilin, pia inajulikana kama ghala la taifa la China. Pia imesifika mno kwa utengenezaji wa magari, utengenezaji wa treni za kisasa, pamoja na uvumbuzi wa vifaa vya satelaiti ya raia.

  Baadhi ya wawakilishi kutoka nchi mbalimbali ambao walifika kwa ajili ya maonyesho hayo walipongeza China kwa kuwa kipaumbele katika kufanikisha kuundwa kwa mpango huu wa karne ya 21 wa kiuchumi ambayo walisema utahakikisha ustawi wa mataifa husika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako