• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vyombo vya habari China vyafungua milango zaidi kwa Waandishi wa Habari za Afrika

    (GMT+08:00) 2017-06-16 09:10:09
    Na Theopista Nsanzugwanko, Beijing

    UHUSIANO baina ya nchi ya China na Afrika umekuwa ukiimarika siku hadi siku kiasi ambacho habari za pande hizo mbili zimekuwa zikitangazwa katika upande mwingine kwa kiasi kikubwa. Ukiangalia vyombo vya habari nchini China ni lazima utakutana na habari ya nchi za Afrika katika sekta mbalimbali hasa kwa Afrika na jinsi China ambayo ni nchi inayoendelea inavyojikita katika kusaidia.

    Waandishi wa habari wa China na Afrika wamekuwa na uhusiano mkubwa kwa kubadilishana uzoefu lakini China kwa kutumia wizara ya Mambo ya Nje ya China kupitia mpango wa "Kituo cha Mawasiliano ya Habari kati ya China na Afrika" ambao umetekelezwa kwa miaka mitatu mfululizo toka mwaka 2014. Mwaka huu, wanahabari 279 kutoka nchi za Afrika wako nchini China kushiriki kwenye mpango huo kwa miezi 10 tangu Februari 2017.

    Wiki hii waandishi hao walitembelea vyombo mbalimbali vya habari kwa lengo la kuona utendaji kazi wao, uendeshaji upataji habari na vinginevyo ambapo walialikwa kuchangia katika vyombo hivyo wakiwa nchini China na hata watakaporejea katika nchi hizo. Lengo kubwa ikiwa ni kueleza wananchi wa Afrika Ukeli kuhusu China na pia wananchi wa china wakafahamu nchi za Afrika na Uhusiano uliopo baina ya nchi.

    Inaelezwa kuwa China imekuwa na idadi kubwa ya vyombo vya habari kwani ina vituo vya luning 3,240, Redio 643 na hata magazeti ya kila siku zaidi ya 800 ambayo mengi yao yakiwa yanamilikiwa na serikali ya chama tawala cha Kikomunisti lakini huru kuandika habari zozote kulingana na mikakati yao lakini ziwe za kweli na zenye kufuata maadili ya uandishi wa habari.

    Katika ziara ya waandishi wa Afrika waliweza kutembelea vyombo vya habari vya China Investment Magazine, Global Times (Online Media ) China International Publishing Group, Gazeti la China Daily, CCTV au CGTN na baadaye China Radio International ambapo mengi yamekuwa yakimiliki tovuti zake zinazofanya kusomwa na watu wengi zaidi.

    Katika ziara hiyo, mbali na kuangalia namna ya uzalishaji, usambazaji na mengineyo hususan kwa nchi za China na Afrika Waandishi hao wa habari walialikwa kuandika katika taasisi hizo za Habari China. Katika jarida linalotolewa kila mwezi la Afrika linalotolewa na China Investment Magazine kwa Africa wamealika waandishi wa habari kuchagia wakiwa China na hata wakirejea katika nchi zao.

    Katik ofisi za Global Times ambao ni wamiliki wa mtandao wa habari wa Huanqiu.com, Mkurugenzi wake, Shan Chengbiao anasema ilianzishwa mwaka 2007 na kuthibitishwa na baraza la habari la nchi hiyo. Huanqiu.com ina waandishi wa habari wa kujitegemea katika nchi zaidi 150 na kutangaza habari kutoka pande zote za dunai kwa kutumia lugha ya Kichina na Kiingereza.

    Anasema asilimia 1 hadi 2 pekee ya waafrika ndiyo wanatembelea mtandao huo na wamepanga kuimarisha mahusiano kwa kutafuta wadau mbalimbali ikiwemo waandishi wa katika kuimarisha mahusiano.

    Katika majarida ya "Beijing Review" ambalo hutolewa mara moja kwa wiki kwa lugha ya Kiingereza ilianzishwa mwaka 1958 ikiwa inasambaza nakala zaidi ya 70,000 kwa kila toleo huku likiwa na matawi mawili zaidi ya makao makuu ya China ambayo ni Marekani na Afrika Kusini.

    Mhariri Msaidizi wa jarida la Beijing review, liitwalo China Africa, Ni Yanshuo anasema serikali ya nchi hiyo haiingilii utoaji wa habari kwa kuwa taarifa zinatolewa za uhakika na bila upendeleo hivyo hakuna sababu ya kuwa na woga katika kuandika habari kwa kuwa inamilikiwa na serikali.

    Licha ya kutumia lugha ya kichina lakini wamekuwa wakichapisha majarida yao kwa lugha mbalimbali ikiwemo kiingereza na kifaransa lakini wakiwa na mikakati ya kwenda mbali zaidi kwa jarida hilo la Afrika kuongeza lugha kadhaa ili kufikia waafrika wengi. Anaeleza kuwa lengo la jarida hilo ni kuhakikisha wanatoa habari zinazohusu China na kufanya Africa wafahamu vizuri kinachoendelea nchini humo kwa uwazi kuelezea maeneo mbalimbali na tarari wanasambaza katika nchi za Afrika Kusini, Malawi, Kenya na kwingineko. Anawaalika waandishi wa habari kuchagia kuandika katika jarida hilo ilita kuongeza wigo wa kupata habari za Afrika.

    Katika ofisi ya gazeti maarufu nchini humo la China Daily, Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Habari za Kimataifa, Su Quiang anasema katika kuhakikisha wan.akuza ushirikiano na nchi za Afrika wana tawi lao Nairobi Kenya huku wakitarajia kufungua matawi katika nchi nyingine. Anasema pia wana jarida lijulikanalo kama "Teens magazine" kwa ajili ya wanafunzi kujifunza lugha ya Kiingerea lilizna mwaka 1993 na mpaka sasa wanachapa nakala zaidi ya milioni mbili.

    Wanataka kuandika story nyingi za Afrika kwa kutumia tawi lao lililopo nchini Kenya na kufikia habari toka nchi za Nigeria, Afrika Kuisni na Kwingineko huku wakihakikisha wanatumia mitandao ya kijamii kutoa habari kwa Afrika na china.

    Katika ofisi ya kituo cha Luninga cha China Global Television Network (CGTN) ambayo ilizinduliwa mwaka 2016 na kituo cha kimataifa cha Luninga nchini humo cha National Broadcaster China Central Television (CCTV) kwa lengo la kuhuhisha utoaji wa habari za kisasa duniani kwa lugha mbalimbali.

    Mkurugenzi wa CGTN kwa lugha ya Kiingereza Li Bin anasema wana uwezo wa kupata habari kutoka nchi mbalimbali zaidi ya 70, ikiwa na habari za saa 24 kwa lugha ya Kiingereza na lugha nyingine wakitumia kutangaza habari zao ambazo ni Kispaniola, Kifaransa, kiarabu na Kichina.

    Katika nchi za Afrika wana tawi lao katika mji wa Nairobi nchini Kenya lakini wakiwa na waandishi wa habari wakitoa habari kutoka nchi za Afrika Kusini, Sudan, Misri na kwinginezo lakini bado wanafanya jitihada kujipanua katika nchi zingine ili kuwa na habari mchanganyiko. Anaalika waandishi wa habari Afrika kuchangia katika kutoa habari kwa lugha za kiarabu na kifaransa kwani wanahitaji habari za jamii za nchi hizo.

    Anaeleza kuwa luninga hiyo ina ushirikiano na vituo mbalimbali vya habari Afrika ikiwemo Shirika la Habari Kenya (KBC) lakini hawana shida Katika kushirikiana na vyombo vya habari binafsi kwani nchini Kenya pia hushirikiana na KTN ambacho ni chombo cha habari binafsi. Anaweka wazi kuwa katika kushirikiana na vyombo vya habari Afrika wamekuwa na changamoto ya Teknolojia kuhakikisha wanapata habangine hazijafika Afrika jambo waliloweka wazi kulifanyia kazi.

    Katika ofisi ya Radio ya Kimataifa ya China (CRI) ambayo ni moja ya taasisi kubwa za uandishi wa Habari China ilianzishwa Desemba 3 mwaka 1941 ikimilikiwa na serikali ya China, waandishi hao walitembelea idara mbalimbali. CRI imekuwa ikitumia matangazo yake ya Radio na mitandao kwa lugha za Kiswahili, Kifaransa, English, Kiarabu Hausa na Kireno ambapo wamekuwa wakishirikisha waandishi wa Habari Afrika kuandika habari mbalimbali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako