• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maendeleo na ujenzi wa kihistoria China baada ya tetemeko la ardhi

    (GMT+08:00) 2017-06-16 14:00:52
    Na Eric Biegon katika Sichuan China

    JE, utafanya nini iwapo tetemeko la ardhi wenye ukubwa wa 8.0 kwenye Richter utazuka na kufanya uharibifu mkubwa na kuleta pigo mijini na vijijini? Mbaya zaidi, unaweza kufanya nini wakati vitetemeko zaidi vinaendelea kwa maeneo yaliyokaribu kwa miezi kadhaa baada ya tetemeko hilo kuu na kusababisha majeruhi zaidi na uharibifu?

    Tetemeko la ardhi yenye ukubwa huu mara nyingi utokea ukiambatana ya vifo na uharibifu mno. Kwa mara nyingi, nchi zimeachwa ukiwa na bila sura. Hii ndio taswira kamili ya mambo yalivyokuwa katika maeneo ya Wenchuan na Lixian mkoani Sichuan nchini China miaka 9 iliyopita.

    Mei 12, 2008 ni siku ambayo wengi katika China kamwe hawatasahau. Wale ambao hasa wanatoka maeneo ya milima ya Wenchuan na Lixian, ambao walinusurika tetemeko hilo, milele wataishi na kovu hili.

    Zaidi ya watu 80,000 walipoteza maisha yao kutokana na tetemeko hilo. Wengine 375,000 walinusurika na kupata majeraha makubwa. Lakini kuchochea majeraha haya hata zaidi, karibu waathirika milioni 4.8 waliachwa bila makao. Walibaki bila makazi kwani nyumba zao za awali ziliporomoshwa vibaya sana.

    Katika hali kama hiyo, jinsi inavyokuwa katika sehemu nyingine nyingi duniani ambayo yamepigwa na mawimbi, viongozi pamoja na raia wanabaki kukata tamaa bila kujua nini cha kufanya baada ya hapo.

    Kwa kweli, mara nyingi, inachukua kuingiliwa kati kwa wahisani na wanachama wa jumuiya ya kimataifa kujaribu kurejesha mambo angalau kama yalivyokuwa japo kwa kiwango kidogo.

    Lakini China ilifanya nini kuwawezesha watu wake walioathirika kuinuka na kuendelea na maisha ya kawaida? Maendeleo na ujenzi uliotekelezwa na nchi hiyo umetajwa na wengi kama ya kihistoria.

    Muda ambao serikali ya China ilichukua kurejesha maisha ya kawaida kwa maeneo ambayo yalikuwa yamekumbwa na tetemeko umevutia sifa kede kede. Chini ya miaka 3, taifa hilo linaloongozwa na chama cha kikomunisti ilikuwa imebuni makazi mapya kwa wasiokuwa na makazi katika jamii. Wao hatimaye walikuwa na mahali wanapaita nyumbani tena.

    Siku chache zilizopita nilitembelea baadhi ya maeneo ambayo yalipigwa na tetemeko hilo. Katika baadhi ya maeneo, madhara ya tetemeko la ardhi bado ni dhahiri kwa wote kuona. Katika Wenchuan, magofu ya shule ya sekondari ya Xuankou yanaonekana juu ya ardhi. Sehemu ya shule ambayo ilizama chini imebaki kuzikwa kama ilivyokuwa baada ya tetemeko hilo.

    Kulingana na rekodi, watu 55 walipoteza maisha hapa. Walimu, wanafunzi, wafanyakazi na baadhi ya wazazi walikufa wakati wa tetemeko la ardhi. Sehemu ya kumbukumbu ulianzishwa ndani mwa shile hiyo, ila kila mtu ambaye anazuru eneo hilo la mkasa anashikwa na maumivu ya moyo tu anapowaza kuhusu yaliyotokea wakati wa janga hilo.

    Mipango ya kurejesha kila kitu kwa hali yake ya awali yazinduliwa. Hali Wenchuan ilikuwa ni sawa na ya Lixian. Mamlaka yaliongoza juhudi za kuwasaidia wanafunzi ambao walinusurika tetemeko la ardhi kurejelea masomo yao.

    "Baada ya tetemeko la ardhi, kamati ya chama na serikali katika ngazi zote walikuwa na wasiwasi sana kuhusu shule. Madarasa yalianzishwa tena katika vyuo vikuu 3 mjini Chengdu." Akasema bwana Wang Shiwei, gavana wa kaunti ya Lixian.

    Pamoja na juhudi za ziada kutoka jamii, Wang alibainisha kwamba walimu na wanafunzi walihamia mji wa Changzi, mkoani Shanxi kwa mpito kama sehemu ya kupata msaada.

    Muda mfupi baadaye tulitembelea jamii ambayo iliathirika na tetemeko hilo. Lakini katika eneo hili, maisha inaonekana kawaida. Kwa kweli, bila mtazamo huu wa kihistoria, huwezifikiria umeingia makao ya waathirika wa tetemeko. Hapa, wakazi yaonekana wanaishi maisha ya kutosheleka. Ni jamii ya kupangwa.

    Mamlaka ya Kichina bado wanapendelea kutaja sehemu hii kama kijiji. Jamii ya Juilong ni moja kati ya vijiji vyao vingi ambavyo vilijengwa na kuenea kote Sichuan kutoa mahala pa kukaa kwa waliokosa makazi. Lakini jinsi gani China ilifikia ufanisi huu kwa kipindi kifupi?

    "Katika kukabiliana na hayo maafa makubwa, chama nzima (CPC), vikosi vya jeshi na watu wa makundi yote ya kikabila nchini China walijikusanya na kusimama kidete nyuma ya uongozi mzima wa kamati ya CPC ili kupambana na wakati huo mgumu." Gavana Wang alisema.

    Kwa mujibu wa Long Bo, ambaye ni msimamizi wa jumuiya hii na ambaye pia ni katibu wa chama cha CPC katika kata, jamii ya Jiulong sasa inatoa makazi kwa familia 1,500. Anasema wengine, walihamishwa kwenye jamii za karibu ambazo zimeundwa kwa madhumuni hayo.

    "Baada ya tetemeko la ardhi, serikali ilichukua hatua za haraka kuweza kuwasaidia wale ambao walikuwa wameathirika na tetemeko la ardhi. Kijiji hiki kilijengwa katika miezi 9 tu. Theluthi mbili ya wakazi ambao waliishi hapa awali wanaishi hapa leo." Akasema Jiulong.

    Kumbukumbu zinaonyesha kuwa jumla ya askari 130,000 na mamia ya wafanyakazi wa misaada walitumwa kwenye eneo la mkasa na serikali ya China ili kusaidia ujenzi na makazi. Usimamizi wa China ulioko Beijing ulihamasisha rasilimali na kuzielekeza kwa ujenzi huo.

    Hata kama jumuiya ya kimataifa walichangia kusaidia waathirika wa tetemeko hilo, Bo anasema, serikali ya China na raia wake walifanya kazi kwa pamoja ili kuhakikisha hali ya kawaida imerejea.

    Kaunti zote mbili kwa sasa zinashuhudia mabadiliko makubwa hasa katika miundombinu ambayo yalikuwa yameharibiwa mno. Barabara na reli yanajengwa kwa vijiji vya zamani. Hata hivyo mabadiliko hayo ni ya kubuni na wala si chaguo-msingi. Serikali kuu ya China ilitoa majukumu kwa mamlaka ya mikoa kadhaa yenye afya nzuri kiuchumi kuelekeza asilimia fulani ya rasilimali zao na misaada ya ujenzi kusaidia Sichuan.

    Sehemu kubwa ya maendeleo ambayo yanashuhudiwa, kama nilivyoona, unafanywa kwa njia ya msaada wa mikoa mingine yenye maendeleo zaidi kama vile Guangdong ambayo kwa sasa inafurahia kiwango kikubwa na pato lake nchini China.

    Kando na maeneo ambayo yalibaki katika hali yao ya awali baada ya tetemeko la ardhi, labda kama ukumbusho, ni vigumu kujua kuwa Sichuan ilikumbwa na tetemeko la ardhi kubwa sana miaka michache ya nyuma. Kwa sasa, eneo hilo imepata uhai, hata zaidi ya ilivyokuwa kabla ya tetemeko la ardhi, kulingana na wale walizungumza nasi.

    Kwa kila hali, ni rahisi kuona kwamba China ilipata jibu la ndani ili kushinda madhara ya tetemeko kubwa zaidi kuwahi kutokea nchini humo tangu mwaka wa 1976.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako