• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mafanikio na uzoefu wa China katika kupunguza umaskini

  (GMT+08:00) 2017-06-20 12:54:24
  Na Eric Biegon, Beijing

  "LAZIMA tuondoe umaskini ambao upo katika akili zetu kabla ya kuuondoa ndani ya maeneo tunaotawala, kabla ya kusaidia raia na taifa kutoka kwenye minyororo ya umaskini na kuanza barabara ya mafanikio."

  Haya ni maneno ya kiongozi wa China Xi Jinping katika kitabu chake maarufu "Kuondokana na Umaskini." Kitabu hiki kinatoa maelezo ya kina kuhusu jinsi yeye alifanikiwa kukabiliana na kushinda vita dhidi ya umaskini kama kiongozi katika Ningde, moja ya sehemu ya Mkoa wa Fujian iliyokuwa na umaskini zaidi katika miaka ya 1980.

  Azimio lake la kuinua watu wake juu ya umaskini ni bayana kwa kila hali. Wakati huo, alikuwa na mtazamo kwamba "Maeneo fukara hayawezi kuwa na maadili fukara. Kusubiri misaada ya serikali, kutegemea misaada ya kifedha, kuhitaji posho ya umaskini, na kulaumu kila mtu lakini sisi mwenyewe. Dhana hii yote lazima itokomezwe kwenye kaburi la sahau."

  Xi baadaye alipanda ngazi na sasa ni Rais wa taifa wenye uchumi wa pili kwa ukubwa duniani, lakini maneno haya yamebaki kweli na kudhihirika katika mtindo wake wa uongozi. Pengine, hii ni kile jamii ya wachina pia ulikumbatia na kufanya mwongozo wake katika lengo lake la kutaka kuwa namba moja katika uchumi wa dunia kufikia au kabla ya mwaka 2030.

  Kutokana na kuanza kwa ufunguzi wake, China iliweka azimio imara la kukabiliana na umaskini iwapo ingetambua maendeleo yoyote ya maana.

  Sasa si siri kwamba China imewainua raia wake wengi kutoka umaskini kwa viwango ambavyo havijashuhudiwa kokote ulimwenguni. Juhudi hizi zimepokea uungwaji mkono kote duniani.

  Rekodi katika Afisi ya kupunguza umaskini na Uhamiaji China zinaonyesha kwamba zaidi ya watu milioni 700 kutoka China wameondolewa kutoka hali ya umaskini tangu 1978.

  Jambo la kushangaza ni kwamba China ina shabaha ya kuwaondoa wananchi wake wote kutoka kwenye ufukara kufikia mwaka wa 2020. Ni vigumu kuona kwa nini hii haitawezekana kwani sera hasa ziliyoanzishwa na serikali ya China zaonekana zitafanikisha juhudi hizi.

  Watu milioni 700 ni idadi ya juu mno popote duniani. Lakini ni kwa njia gani China ilifikia hatua hii?

  China inatambua kwamba imefanya juhudi kubwa ili kupunguza umaskini kutoka idadi yake ya watu bilioni 1.4. Lakini kwanza, taifa hilo liliandaa mfumo sahihi wa usimamizi ambapo rekodi ya watu wote wanaoishi katika umaskini zinanakiliwa. Hii pia ni pamoja na wanamoishi, ni wangapi katika familia na ni nini sababu ya wao kuwa maskini.

  Taarifa hii yote baadaye inahifadhiwa kwenye benki ya data ya serikali. Kila mtu binafsi ambaye majina yake yamenakiliwa atakuwa na faili yake ya kipekee. Utaratibu huu, kwa jinsi nilivyogundua, ulichukua miaka miwili kukamilika. Mamilioni ya watu waliajiriwa na serikali kutekeleza mradi huu.

  Kwa mujibu wa afisa mmoja katika ofisi ya umaskini China, hii imeweka msingi imara kwa vita nchini humo dhidi ya umaskini.

  Baada uchunguzi wa karibu hata hivyo, afisi hiyo iligundua kwamba wengi wa walioandikishwa kama maskini waliishi katika maeneo ya chini ambayo hayazalishi mazao mema mashambani. Mamlaka hizo kwa haraka zilianzisha harakati za kuwahamisha watu kutoka walopokuwa hadi maeneo mengine yanayowezesha uzalishaji.

  Na ili kuhakikisha mafanikio, serikali ilihakikisha kuwa watu wanaoishi chini ya umaskini wamesaidiwa kupata kazi. Kutoka mwanzo walitakikana kukuza ujuzi wao kwa ajira. Kwa njia ya mwingiliano, serikali pia iliweza kutambua kwamba theluthi mbili ya watu vijijini walikuwa na uwezo wa kufanya kazi yoyote.

  Hili likiendelea, sekta ya viwandani ilikuwa inachukua sura mpya. Serikali ilihakikisha kwamba kila kijiji na kila kaunti kilikuwa na mpango na mwongozo wa kuendeleza makampuni na biashara binafsi kubwa na ndogo. Wananchi wakati huo walihimizwa kuelekeza macho yao kando na ajira katika sekta ya umma na badala yake wakahimizwa kuingia kwenye biashara binafsi kwa njia ya ubunifu.

  Lakini Serikali ya China yenye makao yake Beijing, haikuwaacha wasimamizi wa malmaka mbalimbali kuketi kitako. Wao walilazimika kuanzisha mipango ya muda mrefu na mipango ya muda mfupi kwa ajili ya kupambana na umaskini. Lakini kubwa, hata hivyo, yaonekana ilikuwa kuhakikisha mafunzo yametolewa kwa kina.

  "Tunaamini kwamba kama kila familia ina angalau mtu mmoja wa kufanya kazi, wao wataondokana na umaskini." Afisa mmoja katika afisi ya umaskini alisema.

  Kisha kulikuwa na utoaji wa ruzuku kwa familia maskini. Muhimu zaidi ni katika eneo la elimu na afya. Wanafunzi kutoka familia maskini walipata na bado wanapewa miaka 15 ya elimu bila ya malipo. Miaka hii katika shule ni lazima kwa wote.

  Kwa mujibu wa Zhang Haipeng, ambaye anafanya kazi katika afisi hiyo, hali ya afya ya raia maskini inashughulikiwa kwa kiwango kikubwa na serikali hii ikiwa ni pamoja na gharama ya huduma ya matibabu katika familia maskini. Anasema sera za serikali zinazuia hospitali kutoza malipo kutoka familia maskini zaidi ya asilimia 10 ya bili zao za matibabu. Mengine yanalipiwa na serikali ya kitaifa.

  "Baada ya miaka ya uchambuzi, tumekuja na hitimisho kwamba magonjwa na maradhi ni sababu ya watu kurejea hali mbaya ya ufukara." Akasema bwana Zhang.

  Isipokuwa kwa serikali ambayo inachukua majukumu ya wananchi, makampuni kutoka China yamekuwa yakihimizwa kushiriki kikamilifu katika programu za kupunguza umaskini. Taasisi za binafsi na za serikali hadi sasa zinashiriki katika mpango huu.

  Mikoa ambayo yameshuhudia maendeleo kuliko mengine yamekuwa yakitoa msaada zaidi katika suala hili pia. Wao wanafanya hivyo kupitia mfumo wa moja kwa moja (1 + 1), ambapo maeneo yaliyo na utajiri zaidi yanahimizwa kutoa msaada kwa mikoa maskini.

  Kwa maoni ya maofisa hao, viwango vyote vya jamii nchini China vinashiriki katika mpango wa kupunguza umaskini.

  Zaidi ya hayo, serikali ya China inahimiza maamuzi ya kina ndani ya ngazi zote za uongozi. Viongozi katika ngazi ya taifa, mkoa na manispaa wanatakiwa kutumia muda zaidi kwa kushughulikia masuala muhimu ya kupunguza umasikini.

  Hii ni falsafa ambayo imeenea kwa sehemu kubwa, kama si yote, ya jamii nchini China. Kiongozi wake Rais Xi Jinping ana wazo hili kama ilivyonakiliwa katika kitabu chake. Yeye anaamini kwamba vita dhidi ya umaskini zitafaulu. Anasema, ni lazima ushindi upatikane.

  "Iwapo tunaendelea kupigana na matatizo, kwa kuwa mwaminifu katika mchakato huu, kufanya jitihada za kuendelea na kukataa kukata tamaa katika mapambano yetu, basi tutaweza kujikomboa kutoka minyororo ya umaskini kabisa." Akasema Rais Xi.

  Mafanikio ya harakati ya China dhidi ya umaskini, yamefanya mataifa mengi kutazamia mtindo huu. China kwa upande mwingine inataka kutoa uzoefu wake na mafanikio katika kupunguza umaskini kwa nchi nyingine zinazoendelea yenye nia ya kutokomeza janga hili.

  Mfumo wa Mkanda mmoja Njia moja, ambayo hivi karibuni ulizindua mjini Beijing, ni njia muhimu katika kuafikia utambuzi huu. Na kwa kweli China inataka kutumia mfumo huu mpya kujenga jamii ya pande zote zenye mafanikio.

  Wakati wa uzinduzi wake mwezi uliopita, viongozi wa dunia ambao walikutana katika kongamano hilo waliukaribishwa ushirikiano wa biashara baina ya nchi, pembe tatu, kikanda na kimataifa ambapo nchi ziliweka mkazo, kati ya mambo mengine, kutokomeza umaskini.

  Katika hotuba yake ya ufunguzi, Rais Xi alisema kuwa ana shauku kuhusu nia yake ya kuona watu kutoka mataifa yaliyojiunga na mpango huu wamewekwa huru kutokana na pingu za umaskini.

  "Kwa upande wa hali halisi, tunajikuta katika ulimwengu ulio na changamoto nyingi. Ukuaji wa pamoja unahitaji vichocheo vipya, maendeleo inahitaji zaidi kushirikisha kila mmoja, na kwamba pengo kati ya matajiri na maskini imepunguzwa mno." Alisema Rais Xi.

  Waangalizi wa karibu hadi sasa wamepongeza mpango huu wakisema Afrika itafaidika mno kutokana na kwamba dhana ya Mkanda mmoja Njia moja umeipa kipaumbele bara la Africa, huku kukiwa na wito kwa ajili ya kuimarisha miundombinu, taasisi na watu kwa watu kuunganishwa kati ya nchi.

  Tayari, miradi muhimu katika sekta ya viwandani, kilimo, utalii na teknolojia yanayotekelezwa katika baadhi ya nchi za Afrika chini ya mpango huu. Inatarajiwa kwamba fursa zaidi za kazi zitaundwa chini ya mfumo huu.

  Wakati huo huo, China inadhihirisha nia yake ya kutaka kusaidia Afrika kupambana umasikini kupitia uundwaji wa kundi la wataalam maarufu China Africa Think Tank. Baraza hili linatoa jukwaa au daraja kwa kuunganisha mawazo muhimu ya wasomi wa Kichina na wa Afrika.

  Umaskini ni mojawapo ya maswala ambayo kwa sasa wanachunguza kwa lengo la kupendekeza suluhisho kamili.

  Kundi hilo litaandaa mkutano wake wa kila mwaka baadaye wiki hii mjini Addis Ababa, Ethiopia, ambapo linatarajiwa kutoa matokeo yake kuhusu kinachochangia umaskini katika Afrika na njia muhafaka ya kuzishughilikia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako