• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wasomi na mikakati ya China kumaliza umasikini Afrika

    (GMT+08:00) 2017-06-20 12:58:07
    Na Theopista Nsanzugwanko, Beijing

    AFRIKA yenye idadi ya watu zaidi ya bilioni 1.1 ina rasilimali nyingi za asili zenye thamani kama Mafuta, gesi, madini mbalimbali na vinginevyo lakini inakabiwa na changamoto kubwa ya umasikini .

    Wasomi wa China na Afrika walikutana mwaka jana nchini China na kuzungumzia sababu za Afrika kukithiri kwa umasikini na mikakati ya kupunguza umasikini.

    Inakadiliwa kuwa asilimia 75 ya nchi masikini duniani ziko katika bara la Afrika.

    Hali ya Umasikini:

    Takwimu za benki ya dunia na Umoja wa Mataifa kwa mwaka 2010 zinaonesha kuwa watu milioni 414 katika nchi za Afrika zilizo katika jangwa la Sahara wanaishi katika umasikini uliokithiri kwa asilimia 48.5 kwa kuishi kwa dola za marekani 1.25 kwa siku.

    Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Chakula na Kilimo (FAO) linakadilia kuwa watu milioni 239 ambao ni asilimia 30 ya wananchi wa nchi hizo za Afrika waliokabiliwa na njaa mwaka 2010.

    Ripoti zinaeleza kuwa watu milioni 589 wanaoishi katika nchi za afrika zilizo katika jangwa la sahara hawana uwezo wa kupata nishati ya umeme huku milioni 738 wakiwa hawapati maji safi.

    Hali hiyo ya umasikini inafanya watu zaidi ya milioni 500 magonjwa mbalimbali hasa yale yanayotokana na wanasumbuliwa na magonjwa ukosefu wa maji safi na salama kwani asilimia 50 wamekuwa wakisumbuliwa na magonjwa yanayotokana na kutumia maji yasiyokuwa safi kama Kipindupindu.

    Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi (UNHCR) linaeleza kuwa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, migogoro mbalimbali, vita na ukosefu wa haki za binadamu unasababisha watu zaidi ya milioni 18 kuishi katika makambi ya wakimbizi au uhamishoni.

    Vifo vya uzazi wakati wa mimba au kujifungua, vimekuwa vya kjutisha kwani takwimu zinaonesha mwanamke mmoja kati ya 16 anakufa wakati katika nchi za Amerika Kaskazini mwanamke mmoja hufa katika nyakati hizo kati ya wanawake 4,000.

    Ugonjwa wa Malaria umekuwa changamoto kubwa kwani, watu zaidi ya milioni moja wengi wao wakiwa watoto chini ya miaka mitano hufariki kwa ugonjwa huo.

    Sababu za Umasikini:

    Wataalamu na wasomi mbalimbali kutoka Afrika na China ambao mwaka huu wanakutana katika mkutano wao kwa mara ya sita kujadili masuala mbalimbali wanachambua kuwa changamoto hapo juu ni sababu ya umasikini kwa bara hilo.

    Lakini pia kuna Rushwa kwa serikali nyingi ikiambatana na vitendo vya ubadhilifu wa mali za umma huku wakiwa hawana mipango ya maendeleo kwa kuwekeza katika maeneo yasiyokuwa na tija kwa wananchi kwani wanatakiwa kuwekeza katika maeneo muhimu kama maji salama, ajira, nishati ya umeme na mengineyo

    Migogoro ya wenyewe kwa wenyewe imekuwa ikiendelea kwa muda mrefu hususan vita kama vile nchini Somalia, migogoro ya Ethiopia, Eritrea na kwingineko inafanya kuwa na wakimbizi na vita vikisababisha kusimamisha shughuli za maendeleo.

    Ukosefu wa ajira: ukosefu wa elimu ni matokeo ya kutopatikana kwa ajira jambo linalosababisha matatizo mbalimbali miongoni mwa jamii.

    Matumizi Mabaya ya Ardhi,ni changamoto nyingine ambayo idadi kubwa ya ardhi inamilikiwa na wageni huku serikali ikishindhwa kuisajili na hata iliyosajiliwa na kupangwa utekelezaji wa matumizi hakuna.

    Mazingira imekuwa changamoto kutokana na mmomonyoko wa ardhi, ukame, ukataji miti ovyo, ukosefu wa maji na mengineyo yanayosababisha umasikini kwa kupunguza vipato vya watu na kuathiri kilimo.

    Ukosefu wa miundombinu ni sababu nyingine inayochangia umasikini pamoja na Magonjwa kutokana na kuwa kushambuliwa na magonjwa mbalimbali kama Ukimwi ambao umesababisha familia kubaki masikini.

    Wasomi wanaweka wazi suala masuala yote hayo yanaweza kusababisha kuongezeka kwa umasikini kwani ugharimu maisha ya watu.

    Mapendekezo:

    Wasomi wanatoa pendekezo kuwa katika kukabiliana na masikini nchi za afrika zinatakiwa kufanya haya hata kama matokeo yatachukua muda lakini yataonekana baadaye.

    Ni vema kuhakikisha wanaondoa migogoro katika nchi za Afrika, kupambana na ukosefu wa ajira,kupatikana kwa huduma za Afya na miundombinu ya kijamii kwa kuwa na mipango madhubuti.

    Kuhusu vitendo vya Rushwa, kuwe na sheria madhubuti na adhabu kali kwa wanaofanya vitendo hivyo,kuweka mifumo madhubuti ya usajili wa Ardhi na kutoa haki kwa wananchi wake.

    Pia kutoa elimu itakayosaidia kuongeza ufahamu wa wananchi na kuwekeza katika sekta ya kilimo ikiwemo kujenga viwanda ambavyo pia vitasaidia kutoa ajira.

    Vilevile serikali kuweka mazingira ya kuhakikisha wananchi wafahamu kuhusu uzazi wa mpango kwa kuwa na watoto unaoweza kuwahudumua na kuwapatia elimu.

    Pia nchi za Afrika zinatakiwa kujikita katika ushirikiano wa Kikanda kwa kuongezeka biashara ndani ya kanda na mtiririko wa vitega uchumi kama kwa kutumia ushirikiano jumuiya ya maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) Ushirikiano wan chi za Afrika Mashariki na nyinginezo.

    Kutumia sera za kimataifa katika kuhakikisha wanakabiliana kwa umasikini, suala ambalo tayari China wametumia katika kuhakikisha wanasaidia Afrika kuondokana na Umasikini.

    China ni nchi yenye watu zaidi ya bilioni 1.36 lakini imekuwa na maendeleo kwa kuwajali wananchi wake kwa kuhakikisha watu wake wakifanya kazi na kupata mahitaji yote muhimu.

    Kupambana na umaskini, ni moja ya maswala yanayopewa kipaumbele na serikali ya China katika mipango yake ya maendeleo na Katika mpango wa 13 wa maendeleo ya miaka mitano, kupambana na umaskini na hasa kuwaondoa watu milioni sabini wanaishi katika lindi la umaskini kabla ya mwaka 2020.

    Kutokana na uhusiano mkubwa baina ya China na Afrika,nchi hiyo imeamua kuweka mikakati yake kusaidia Afrika kupambana na Umasikini kwa kuweka mikakati mbalimbali ya kuondoa umasikini katika bara la Afrika ikiwemo Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC.

    Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika lilianzishwa mwaka 2000 na baada ya miaka mitatu ilitoa mkopo dola za kimarekani bilioni 20 kwa nchi za Afrika, kutekeleza miradi 900 ya misaada na kuandaa wataalamu zaidi ya 30,000 kwa nchi hizo.

    Pia ilijenga ilijenga miradi mikubwa ya reli kama vile reli za kutoka Addis Ababa hadi Djibouti, na kutoka Nairobi hadi Mombasa.

    Suala la kuondoa umasikini kwa nchi za afrika ni moja ya ,Programu 10 zilizotangazwa na Rais wa China Xi Jinping katika kuimarisha ushirikiano wa Afrika na China kwa miaka mitatu wakati wa Mkutano wa FOCAC uliofanyika mwaka 2015 nchini Afrika Kusini.

    Programu nyingine ni viwanda, kilimo cha kisasa, miundombinu huduma za kifedha, biashara, uwekezaji, afya, ulinzi na Usalama na nyinginezo ambavyo ukiangalia kwa umakini vyote vitasaidia katika kuondoa umasikini katika bara hilo.

    Mwaka huo China ilihaidi kutoa dola za Marekani bilioni 60 pamoja na dola za Marekani bilioni tano kama msaada na mikopo kuhakikisha wanatekeleza mikakati 10 ya kusaidia Afrika.

    Katika ushirikiano huo kuna makubaliano 243 ya ushirikiano yenye thamani ya jumla dola za kimarekani bilioni 50.7, kati ya hayo, uwekezaji wa moja kwa moja wa makampuni ya China kwa Afrika na mikopo ya kibiashara imezidi dola za kimarekani bilioni 46.

    Ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na Afrika umeonesha uhai mkubwa na hali ya kufurahisha, na kudhihirisha mustakbali mwema wa ushirikiano hasa katika kumaliza umasikini Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako