• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Inner Mongolia yapanua biashara na Afrika huku China ikitafuta mahusiano zaidi

    (GMT+08:00) 2017-07-03 10:43:35
    Na Eric Biegon katika Inner Mongolia, China

    Jimbo la Mongolia ya ndani ipo kaskazini mashariki mwa China katika mpaka wa Mongolia na Urusi. Si mengi yametangazwa kuhusu mkoa huu lakini umesajili maendeleo makubwa tangu kiongozi Deng Xiaoping kuweka mageuzi ya kiuchumi China mwaka 1978.

    Pato lake la mwaka kwa miaka 15 iliyopita inadhihirisha kuwa imekuwa miongoni mwa mikoa inayofanya vyema zaidi katika China. Kwa miaka sasa, mkoa huu umeshuhudia kunawiri kwa uhusiano wake wa biashara na Afrika. Hii iliwekwa wazi na kuthibitishwa na utawala wa Inner Mongolia.

    Akihutubia waandishi wa habari 27 kutoka Afrika waliokuwa wakitembelea mkoa huo wiki hii, bwana Ding Xiaolong, ambaye ni afisa mwandamizi wa mamlaka wa Inner Mongolia katika Idara ya Biashara, alisema biashara kati ya mkoa huo na Afrika kufikia mwaka 2016 ilikuwa na thamani ya milioni 302 Dola za Marekani.

    "Chuma, mafuta na makaa ya mawe ni baadhi ya mali ambayo inasafirishwa China kutoka Mauritania, Madagascar, Nigeria na Afrika Kusini. Kwa upande mwingine, Inner Mongolia inasafirisha bidhaa kama vile dawa na chuma, magari ya abiria, miongoni mwa bidhaa mengine." Xiaolong alisema.

    Jimbo hilo ilishuhudia asilimia kubwa yake ya mauzo kuelekea nje mwaka 2016 kufikia billioni 4.5 Dola za Marekani, huku uagizaji kutoka mataifa ya nje, zikiwemo nchi za Afrika, ukiinuka kwa thamani kifikia billioni 7.3 dola za Kimarekani.

    Idadi kubwa ya makampuni ya biashara yenye makao makuu katika eneo hili pia zimepanua biashara zao barani Afrika. Kampuni ya North Heavy Truck Ltd, kwa mfano, inazalisha vitengo 1,000 kila mwaka, hii ikiwa ni idadi ya juu zaidi ya kampuni yoyote China.

    Kampuni hii inafanya mauzo ya malori na matrekta mazito kwa ajili ya matumizi katika migodi wazi kwa nchi 60 zilizoko bara la Asia na Afrika. Kati ya mauzo hayo nje ya nchi, kampuni hii imefichua kuwa kiwango cha chini cha vitengo vinavyouzwa Afrika ni matrekta 300 kila mwaka.

    Baadhi ya nchi za Afrika ambazo zimekuwa zikiagiza magari hayo kutoka kampuni ya NHL ni pamoja na Zambia, Namibia, Afrika Kusini, Nigeria, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na Zimbabwe.

    "Nchi ya DRC ni mshirika wetu mkubwa katika bara la Afrika. Lakini kampuni yetu pia ulitia saini mkataba wa kibiashara karibuni na taifa la Algeria." Akasema bwana Liu Zhi, ambaye ni mhandisi mtafiti mwandamizi katika kampuni hiyo.

    Liu alithibitisha kuwa Afrika imekuwa soko kubwa ya bidhaa kutoka kampuni ya NHL kwani mahitaji ya malori na matrekta yake katika bara hilo inaendelea kuongezeka.

    Kutokana na hali hii, wasimamizi wa kampuni hiyo wanasema wataendelea kuzalisha vifaa vinavyofaa hali ilivyo Afrika huku wakidumisha kuwa matrekta yanayouzwa Afrika yanaendelea kuchunguzwa na kutengenezwa nyakati zote bila malipo kupunguza kuharibika kwa haraka.

    Na hili kudhihirisha kuwajibika kwa jamii kwa kampuni hiyo, wakurugenzi wake wanasema NHL imekuwa ikiendeleza mafunzo ya bure kuhusu matumizi ya mitambo yake kati ya wenyeji katika nchi ambazo matrekta na malori hayo yamenunuliwa.

    Ujuzi huu, wanasema, ni muhimu kwani utasaidia wananchi katika juhudi za baadaye kwani sekta ya ujenzi wa miundombinu unazidi kunawiri barani Afrika kutokana na suala la ufunguzi wa mataifa unaoendelea, mpango ambao unaendeshwa na China.

    Aidha, kampuni hiyo imefichua kuwa inatafuta huduma za mawakala katika baadhi ya nchi za Afrika inapopanua shughuli zake za biashara barani humo. Mashirika hayo kulingana na NHL, yatakuwa kama daraja kati ya makao makuu ya kampuni hiyo iliyoko China na wateja wake katika Afrika.

    "Hatuna mawakala hadi sasa katika Afrika. Kwa sasa tunatazamia kuanzisha afisi za mawakala katika bara hilo. Tunataka ofisi za wawakilishi wetu huko." Akasema Liu

    Ingawa Inner Mongolia haijaendelea sana kama sehemu ya magharibi na kusini mwa China, inajivunia kilomita 190,000 za barabara za lami, kilomita 13,500 za reli, na vituo vya afya ya umma 24,000 ikiwa ni pamoja na bandari 18. Hii ni kwa mjibu wa Luo Yonghong, ambaye ni afisa mwandamizi wa serikali ya jimbo hilo.

    Biashara ya kanda ya mkoa huu ulikuwa kwa kiasi mwaka jana kufikia bilioni 11.7 dola za Marekani. Pato la GDP mwaka huo ulikuwa trillioni 1.86 Yuan ya China, wakati GDP ya kila mwananchi kwa kipindi hicho ilikuwa 74,000 Yuan. Katika sekta ya elimu, milioni 12 Yuan ya China zimetengwa kila mwaka kwa ajili ya masomo ya wanafunzi kutoka nchi za kigeni.

    "Katika mwaka wa 2016, kulikuwa na wanafunzi 3,300 wa kigeni kwa udhamini, pamoja na idadi nzuri kutoka Afrika." Luo Yonghong alisema.

    Katika mpango wa Ukanda mmoja njia moja, viongozi hao wa Inner Mongolia walitangaza kwamba wao wako tayari kuchangia uzoefu wao na Afrika na kusaidia hasa katika vita dhidi ya umaskini. Kwa hiyo, wao waliisifia mpango huo walioutaja kuwa njia muafaka ya kujenga jamii yenye mafanikio sawa duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako