• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China inakuza sekta ya nishati mbadala kupigana na uchafuzi wa mazingira

    (GMT+08:00) 2017-07-12 18:52:25

    Na Eric Biegon, Inner Mongolia - China

    China inazidi kupunguza utegemezi wake juu ya makaa ya mawe kama nguvu ya nishati, badala yake inaendeleza miradi ya vyanzo vya umeme mbadala. Ujenzi wa mitambo ya upepo na umeme wa jua kwa sasa inafanyika katika karibu mikoa yote ya taifa hilo ya mashariki ya mbali. Utegemezi wa nishati inayotokana na makaa ya mawe imetajwa kama moja ya sababu kuu ya uchafuzi wa mazingira na mabadiliko ya tabia ya nchi kama inavyoshuhudia nchini China. Viwanda vya uzalishaji wa umeme kupitia makaa ya mawe kwa sasa vinapunguzwa kwa kasi kubwa.

    Takwimu katika tume ya maendeleo ya taifa na mageuzi pamoja na utawala wa nishati nchini humo zinaonyesha kuwa mwishoni mwa mwaka 2016, vyanzo vya nishati mbadala viliongezeka kwa idadi kwa asilimia 30 ya mahitaji ya nishati katika mikoa ya China ambapo viwango vya matumizi ya makaa ya mawe kama njia ya kuzalisha nishati ilishuka hadi asilimia 70 ambayo baadaye inaunganishwa kwa gridi mbalimbali mikoani. Inner Mongolia, kwa mfano, ina uwezo mkubwa wa kuzalisha nishati ya upepo ikilingalishwa na sehemu nyingine China. Aina hii ya nishati ya upepo umeendelezwa katika mkoa huu kufikia zaidi ya megawati 10,000. Mradi huu ulizinduliwa mwaka 2006 baada ya kuzinduliwa kwa sheria mpya za nishati. "Sheria hii ilihitaji wahudumu wote kwenye sekta ya nishati kuwekeza na kununua rasilmali ya umeme kutoka kwa wazalishaji ambao wamesajiliwa kuzalisha nishati mbadala pekee." Akasema afisa mmoja kutoka kampuni ya Huitengxile Grassland wind power plant iliyoko Inner Mongolia. Utawala wa Inner Mongolia aidha ulifichua kuwa hakuna kurudi nyuma kwa wajibu huu hivyo juhudi kabambe ziliwekwa kwa minajili ya kuanza safari ya kuzalisha nishati safi. "Asilimia 30 ya nishati mbadala katika Inner Mongolia inaweza kuonekana kama isiyoridhisha, lakini kwa kuzingatia kwamba hii imewezekana ndani ya kipindi cha miaka 10 iliyopita tu, inamaanisha sisi tunasonga katika mwelekeo sahihi. Hatua kwa hatua tutakuwa na nishati ya upepo na nishati ya jua kama vyanzo vyetu kuu vya umeme." Afisa huyo alibainisha. Jingneng New Energy Company Ltd lina shamba kubwa la nishati ya upepo katika Huitengxile ambalo ni la pili kwa ukubwa China na lilianza kazi mwezi Agosti 2006. Mitambo yake yanaenea kilomita 50 mraba katika eneo hili. Katika mkoa huu, kampuni hii imewekeza kwa mitambo yenye uwezo wa kuzalisha megawati 260 - megawati 200 kutokana na upepo na megawati 60 kutokana na jua. "Kampuni yetu imewekeza Bilioni 12 Yuan katika miaka ya hivi karibuni katika viwanda 9 ya kuzalisha nguvu za umeme kupitia upepo." Aliongeza Inner Mongolia kwa jumla ina uwezo wa kuzalisha nishati kufikia kiwango cha kilowati milioni 100. Kwa asilimia 70, wanategemea makaa ya mawe, wakati asilimia 30 ya nishati yake ni kutokana jua na upepo.Sheria mpya ya nishati mbadala pia inatoa motisha ya kifedha, kama vile mfuko wa taifa wa kuendeleza nishati mbadala, na punguzo ya mikopo na mapendekezo ya kodi kwa ajili ya miradi ya nishati mbadala. Maendeleo ya kiuchumi ya haraka China imesababisha ongezeko kubwa la matumizi ya nishati, na maafisa wa Inner Mongolia wanakubaliana kwamba imesababisha kupanda kwa uzalishaji wa madhara na uhaba wa umeme. Kwa maoni yao, sharia mbadala ya nishati imeundwa ili kusaidia kulinda mazingira, kuzuia uhaba wa nishati, na kupunguza utegemezi wa nishati kutoka nje.Aidha, maafisa hao wamehamasisha Afrika kukumbatia vyanzo vya nishati mbadala huku wakifichua kuwa mradi wenye kilowatt elfu 50 ya nguvu, unaweza kuendelezwa kwa kutumia chini ya milioni 50 dola za Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako