• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wadau walaumu wafanyabiashara toka Afrika kutozingatia vipimo halisi vya ubora kwa bidhaa toka China

  (GMT+08:00) 2017-07-14 18:25:44

  Na Theopista Nsanzugwanko,Beijing-China

  Ni jambo la kawaida katika nchi za Afrika kusikia wakilalamikia ubora wa bidhaa mbalimbali zinazosafirishwa kutoka nchini China kuwa hazina ubora lakini ikiwa tofauti kwa sehemu nyingine duniani ambao wanatumia bidhaa hizo.

  Mfanyabiashara kutoka nchini Ghana,Stephen Ketu anayeishi katika mji wa Beijing akiambatana na wadau wengine wa biashara na wasafirishaji kutoka Achina Kwenda Afrika anaweka wazi kuwa tamaa ya wafanyabiashara wengi kutaka faida bila kutumia vipimo maalum kwa bidhaa husika ndiyo chanzo cha bidhaa zisizo na ubora kusafirishwa katika nchi za Afrika.

  Anasema kinachojitokeza ni pale wafanyabiashara wanapotaka bidhaa Fulani katika viwanda china na kutakiwa kupeleka vipimo halisi ili kutengeneza kwa kuzingatia ubora wanakuwa hawana na kuishia kutengeneza zile zitakazowapatia faida ambazo hakika hazina ubora.

  Analalamikia serikali katika nchi za afrika kushindwa kudhibiti kuingia bidhaa hizo kwani inatakiwa kuweka ukaguzi imara na kuzingatia viwango vinavyotakiwa kuingiza katika nchi bila kujali gharama za kuuzia wananchi.

  Ketu anasema wafanyabiashara wengi wanaofika nchini China,hawajui soko la bidhaa wanazotaka na kuishia kununua bidhaa zizizo na ubora na kuuza katika nchi za Afrika kwa lengo la kupata faida.

  "hii inaonesha dhahi kuwa waagizaji wetu hawana uelewa kuhusu ubora wa bidhaa husika au ni watu wabinafsi wanoangali nini wanaingiza bila kujali wateja wao"anasema

  Kulingana na mfanyabiashara huyo,wafanyabiashara wengi kutoka Afrika wanajali tu bei ya bidhaa wala si ubora

  Ketu,ambaye ameishi nchini China kwa miaka zaidi ya 19 alianza kama kinyozi lakini sasa mkurugenzi wa kampuni kubwa ya kusafirisha mizigo sehemu mbalimbali za Afrika na kwinginezo huku akifanya biashara.

  Anasema biashara yake ya kwanza kutoka China mwaka 2002 ilikuwa kusafirisha bidhaa kuelekea nchini Norway.hata hivyo anadai kuwa raia na wafanyabiashara wan chi hiyo walisifia ubora wa bidhaa hizo.

  Anashangaa kuwa kuna dhana kwamba bidhaa toka China hazina ubora kwa barani Afrika suala ambalo amefutilia mbali .

  "ni wafanyabiashara wangapi Afrika wanatoa vipimo vya ubora kabla ya kuagiza bidhaa kutoka viwanda vya nchini China?"Anauliza

  "ni tatizo la Afrika.hawajui wanachotaka.hoja yao kubwa ni gharama tu, hawajui kuwa kwa jinsi unaendelea kutaka kupunguziwa bei ndivyo ubora unavyozidi kushuka."alisema

  Ameshauri viongozi wa nchi za Afrika,kufuata sheria. Kwa maoni yake serikali za mataifa ya Afrika ziwajibike kutoa vipimo vyenye viwango vya ubora kwa wafanyabiashara wote wanaosafirisha bidhaa kutoka China.

  Anaweka wazi kuwa amekuwa akitoa elimu kwa wafanyabaishara wa nchi ya Ghana kuhakikisha wanasafirisha bidhaa zenye ubora kwa kueleza jinsi ya kupata bidhaa zenye ubora.

  Anakiri kuwa wafanyabiashara wengi wa nchi yake aliofanya kazi nao kwa sasa ni matajiri hivyo anataka kupanua wigo kwa kushirikiana na wananchi kutoka nchi mbalimbali za Afrika kwa lengo la kumaliza tatizo la kuingia kwa bidhaa zisizo na ubora.

  China ni nchi ya pili kiuchumi duniani tangu mwaka 2010 na ukuaji wa uchumi unakuwa unaongezeka kwa kasi na wachambuzi wanaeleza kuw aifikapo mwaka 2030 itakuwa ya kwanza na kuishinda Marekani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako