• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wafanyabiashara kutokaAfrika waonyesha nia kuwekeza Sichuan

  (GMT+08:00) 2017-07-24 11:16:57
  By Theopista Nsanzugwanko in Sichuan, China

  Sichuan ni jimbo ambalo uchumi wake unakua kwa kasi mno na imeibuka kuwa kitivo cha uvumbuzi wa teknolojia, viwanda na maendeleo ya vipuri mbalimbali va usafiri wa anga.

  Pato la ndani (GDP) katika jimbo la Sichuan ni trillioni 3.26 Yuan ya China ikiwa inashikilia nafasi ya sita kwa ukuaji wa uchumi kwa mikoa yote nchini China.

  Kama ilivyo kwa nchi nyingine duniani, jimbo hilo limekuwa likipanua mahusiano ya kiuchumi na nchi mbalimbali za Afrika ambapo kwa sasa ina mahusiano na zaidi ya wafanyabiashara 500 katika mataifa 200 duniani.

  Naibu mkurugenzi wa itifaki na mawasiliano kwenye ofisi inayoshughulikia mambo ya nje, Xiao Yonggang, anasema wawekezaji na kampuni kutoka mataifa saba ya Afrika zikiwemo Cameroon, Ghana, Ivory Coast, Kenya, Nigeria, Seychelles na Mauritius wamewekeza dola milioni 7.25 za Marekani katika jimbo hilo hadi kufikia mwisho wa mwaka 2016.

  Hata hivyo, Yonggang hakubainisha maeneo hasa ya uwekezaji yanayofanywa na kampuni na wawekezaji kutoka nchi hizo, lakini anaeleza kuwa maendeleo ambayo yameshuhudiwa ni ushahidi wa kukua kwa biashara baina ya jimbo hilo na Afrika.

  Katika kukuza mahusiano hayo, mabalozi wa nchi za Afrika walifanya ziara katika jimbo hilo mwezi machi mwaka jana kwa mwaliko wa watu wa eneo la Chengdu.

  Katika ziara hiyo, zaidi ya maafisa 100 waliohudhuria mkutano huo wakiwemo wafanyabiashara kutoka China na wanadiplomasia kutoka nchi za Afrika walielezea sera za nchi zao katika masuala ya uwekezaji na matumaini yao katika kuimarisha ushirikiano na kubadilishana uzoefu baina ya mataifa hayo mawili.

  Takwimu zinaonesha kuwa mpaka sasa jimbo hilo linapeleka misaada ya wafanyakazi 669 kusaidia katika masuala ya matibabu huku uwekezaji wake katika bara la Afrika mwaka uliopita ulihusisha miradi zaidi ya 100 yenye thamani ya dola bilioni 1.6 za marekani.

  Mkurugenzi wa kukuza masoko katika Kamati ya Maendeleo ya utalii katika jimbo hilo Yu Xin alifichua kuwa jimbo la Sichuan ni maarufu kwa wanyama aina ya Panda ambao ni nadra sana duniani na vyakula vya aina mbalimbali zaidi ya 6,000.

  Pia , juhudi za kuwezesha raia kutoka mataifa 15 kuingia mkoa huo bila kutumia viza zimeimarishwa. Aidha, kulingana na Yu kumekuwa na mchakato wa kuwa na usafiri wa ndege wa moja kwa moja kutoka mji mkuu wa Chengdu kuelekea nchi za Mauritius na Ethiopia ambapo anasema ikifanikiwa itapunguza masaa ya usafiri wa ndege kwa zaidi ya saa sita.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako