• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • BRICS yaelekeza macho yake kwa mataifa yanayoendelea Afrika

    (GMT+08:00) 2017-09-04 10:28:42
    Na Eric Biegon katika Fujian, China.

    Kenya ni miongoni mwa mataifa yanayoshiriki mkutano wa BRICS unaoendelea Mkoani Fujian, eneo la Xiamen nchini China. Nchi hiyo kutoka Afrika Mashariki ilialikwa kushiriki katika mkutano huo kwa mara ya kwanza kabisa huku ikidhihirika kwamba kongamano hilo linabadili mwelekeo na kutaka kuvutia mataifa yanayoendelea barani Afrika.

    Kenya, Guinea na Misri yanatuma wajumbe ambao watajiunga na wenzao kutoka Afrika Kusini, mwakilishi pekee katika bara la Afrika tangu ilipozinduliwa, huku mfumo huu wa uchumi ukiimarishwa kuwa BRICS Plus (+) ili kujumuisha nchi zaidi ya mataifa tano wanachama.

    Kidesturi mkutano huo huleta pamoja Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini. Kamati ya kiufundi ya mkutano huo hata hivyo inasisitiza kwamba jukwaa hilo si ya nchi hizo tano pekee, kwani inapanuliwa zaidi kwa minajili ya kuimarisha usalama na uchumi duniani.

    Kamati hiyo inasema hii itafanyika kupitia benki mpya iliyozinduliwa karibuni ya New Development Bank, NDB, iliyoanzishwa hasa kwa madhumuni ya kuwezesha utendakazi wa mfumo huo.

    Kutokana na hayo, miradi ya maendeleo katika Afrika na Amerika ya Kusini sasa zitaangaziwa zaidi na taasisi za kifedha za jukwaa hilo, kama vile Benki Mpya ya Maendeleo NDB, pamoja na ile ya Asian Infrastructure Investment Bank, AIIB.

    Wizara ya kigeni ya China inasema mipango inaendelea kwa kasi kuhakikisha kwamba kuna ushirikiano kati ya Benki zinazofanya kazi chini ya BRICS na benki kutoka mataifa ya Afrika.

    Aliyekuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Uchumi Duniani, Prof Chen Fengying anasema kuwa nchi zinazoendelea za Afrika zina sababu ya kutabasamu kwani wao hatimaye wana taasisi inayonasa matarajio yao ya kifedha.

    "Kuna Benki nyingi za maendeleo katika dunia ya leo, kubwa zaidi ikiwa ni Benki ya Dunia. Lakini Benki Mpya ya Maendeleo inayomilikiwa na BRICS ni benki pekee inayoangalia nchi zinazoendelea kama uti wa mgongo." Akasema Profesa Chen

    Chen ambaye ni mkurugenzi wa zamani anasema jukwaa hilo sasa linaweka msingi kuhusu maendeleo katika miaka kumi yajayo hasa kwa kupitia benki ya NDB.

    "Tumezindua benki hii. Sisi tunataka kuitumia ili kukabiliana na changamoto halisi. Hii si baraza tu. Ni shirika halisi, ambayo ni wazi kwa nchi zinazoendelea na masoko mapya." Yeye alielezea.

    Prof Chen alisema kwamba macho yote yataangazia BRICS Plus wakati huu kwani lina udhibiti wa karibu asilimia 23 ya uchumi wa dunia. Akihutubia waandishi wa habari, Chen alisema bayana kwamba lengo kuu ni kuona kuwa Benki mpya ya Maendeleo, NDB, Asian Infrastructure Investment Bank, AIIB na Shirika la uchumi la BRICS zimechukua nafasi ya benki mbadala ya Benki ya Dunia.

    "Suala la maendeleo ya BRICS tayari imepanuka zaidi ya mataifa wanachama. Benki mpya ya Maendeleo imeanza kazi, na sasa imemaliza masuala dhahania na kushughulikia mambo halisi. Kama jukwaa iloyowazi, BRICS Plus inahusu Afrika na Amerika ya Kaskazini, na hivyo ushawishi wa BRICS utaendelea kuinuka zaidi, "Chen alisema.

    Aliongeza kuwa ili kupanua wigo wa shughuli zake na kuwa endelevu kwa muda mrefu, NDB na AIIB zinapanua huduma zao katika Afrika na Amerika ya Kusini na kufadhili miradi ya maendeleo.

    Prof Chen alisema BRICS iko na nia ya kupanua wajibu wa masoko mapya na sio tu ya nchi wanachama watano. Kutokana na hali hiyo, Kamati ya ufundi inasema itaimarisha ushirikiano kati ya BRICS na Umoja wa Mataifa.

    Katika uwanja wa kisiasa, yeye alitaka kuondolea mbali hofu unaoendelea kuhusu mzozo wa mpaka kati ya China na India, na kwamba itazungumziwa wakati wa mkutano huo akisema kwamba viongozi wahusika hawana wasiwasi na kile ambacho alitaja kuwa "suala ndogo."

    Kwa kutimiza sera ya China ya kutoingilia migogoro ya kisiasa na kijamii katika nchi rafiki, Prof Chen alisema kuwa BRICS haiwezi kuingilia kati katika masuala ya ndani ya nchi wanachama, na kuongeza kwamba changamoto zinazowakabili viongozi wa Afrika Kusini na Brazil ni za mpito . Alisema kuwa vyanzo vya migogoro ni kushuka kwa bei za bidhaa, na tofauti za kisiasa na kiuchumi, akisema jawabu ipo katika kuhakikisha maendeleo sahihi.

    "Masuala watakayoshiriki viongozi wa Afrika Kusini na Brazil katika mkutano hayatakuwa ya kutiliwa shaka kwa sababu viongozi huja na kuondoka, lakini mataifa zinasalia," alisema.

    Mkutano wa mwaka huu ina madhumuni matatu hasa juu ya biashara, fedha na uchumi. Kwa kufanya hivyo, BRICS inataka kuongeza juhudi za kufufua uchumi dunia kupitia uwazi, kuheshimiana, faida kwa wote na kushirikishana.

    Ni ndoto hii hasa inayosukuma wanachama wa BRICS kuendeleza majadiliano kuhusu mchakato unaoendelea kuhusu mpango wa ulinzi wa kibiashara unaoendeshwa na baadhi ya nchi za magharibi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako