• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • CADFund yafadhili  miradi zaidi ya 90 Afrika

    (GMT+08:00) 2017-09-04 10:32:39

     

    Na Theopista Nsanzugwanko,Beijing-China

    MFUKO wa maendeleo baina ya China –Afrika (China-Africa Development Fund (CADFund) ni moja ya juhudi za serikali ya China katika kuhakikisha wanadumisha ushirikiano na nchi za Afrika.

    katika mkutano wa ushirikiano baina ya nchi za afrika na China uliofanyika mwaka 2007,mfuko huo ulianzishwa kwa lengo la kuhamasisha na kusaidia kampuni kutoka China kuwekeza katika nchi za Afrika na kushirikiana na wadau wa Afrika katika uwekezaji.

    taasisi hiyo ya kifedha ambayo ni ya kwanza kwa utoaji fedha kwa usawa katika nchi za Afrika imeishafadhili miradi 90 yenye thamani ya dola za marekani bilioni 20 katika nchi 36 za Afrika.

    Makamu wa Rais wa CAD Fund Wang Yong, anawaeleza waandishi wa habari kutoka nchi 27 za Kiafrika kuwa China imewekeza jumla ya dola za Marekani bilioni 20 kwa miaka 10 huku dola za marekani bilioni mbili zikipatikana kwa kuuza bidhaa nje ya nchi na dola za marekani bilioni moja mapato ya kodi zikipatikana.

    Amesema katika miradi iliyopo kwenye nchi hizo za Afrika imeweza kutengeneza ajira kwa wananchi wake zaidi ya 74,000,hivyo kusaidia kukabiliana na tatizo la ajira kwa nchi hizo za Afrika.

    Yong anasema kama iliyo kwa misaada mbalimbali ya China kwenda Afrika haipeleki miradi kwa kuangalia nchi huku miradi inayofadhiliwa na CAD Fund imekuwa ikipewa fedha na ushauri kwa kampuni za China zinazowekeza Afrika ili kuhakikisha inaendeshwa vema .

    Mkurugenzi Mtendaji wa Usimamizi wa miradi katika CADFund, Jiang Lin,amesema taasisi hiyo ilianzishwa mwaka 2007 kutokana na China kuwa na Imani kubwa na afrika kutokana na uwezo wa uzalishaji na kuwepo kwa nguvu kazi ya vijana na kufanya ukuaji wa uchumi kuwa kwa asilimia mbili kwa mwaka.

    Amesema Afrika ni mdau mkubwa wa biashara na China ambapo uwekezaji wake unatarajiwa kufikia dola za marekani bilioni 100 ifikapo mwaka 2020.

    Amesema katika kuharakisha utendaji kazi kwa nchi za afrika wamekuwa na ofisi tano za kanda katika nchi za Ethiopia, Ghana, Zambia, Kenya na Afrika Kusini .

    Naye Mkurugenzi Mtendaji katika idara ya Utafiti na Maendeleo wa CADFund, Wu Zheneng amesema mfuko huo umekuwa ukisaidia jamii katika masuala mbali mbali ambapo kwa miaka 10 watu zaidi ya bilioni moja wamenufaika.

    Amesema bishara baina ya China na Afrika kwa sasa imefikia Dola za Marekani bilioni 188 na katika nnusu ya kwanza ya mwaka 2017 inaonesha kukua kwa asilimia 19 wakati mtaji kwa mwaka 2016 ilikuwa dola za Marekani bilioni 35 lakini inatarajia kufikia 100 bilioni mwaka 2020.

    Katika kuhakikisha malengo yake yanatimia kwa kufikia nchi nyingi na miradi mingi,mwaka 2013,Rais wa China Xi Jinping alitembelea nchi za Afrika ikiwa ni ziara yake ya kwanza Tangu kuchaguliwa kuwa rais.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako