• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yaadhimisha tamasha la mbalamwezi

  (GMT+08:00) 2017-10-07 17:55:44

  Na Eric Biegon katika Beijing, China

  China inafahamika kwa uaminifu wake kwa mila za tangu jadi. Taifa hilo kubwa zaidi barani Asia kwa kweli imesifika kwa utajiri wa tamaduni. Mila hizi kwa njia nyingi zimezidi zile za nchi nyingine. Sifa mojawapo ya kipekee ya watu wa China, ni kujitolea kwao kuhadhimisha sherehe za mabadiliko ya hali ya hewa. Tamaduni hizi zimekuzwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

  Hata ingawa usasa umejipenyeza katika jamii ya China, mila ya kale inaonekana ina mizizi na imeshika jamii. Hata hivyo, kila tamaduni inayoadhimishwa hapa ina maana ya kiasili kwa Wachina. Kwa kweli, desturi hizi si rahisi kufutilia mbali.

  Hivi sasa, kuna sikukuu rasmi za umma saba zinazotambulika nchini China. Sikukuu hizi ni pamoja na ile ya Mwaka Mpya, tamasha la Spring, siku ya ufagiazi wa makaburi au Tomb Sweeping, Siku ya wafanyikazi, Sikukuu ya tamasha la Dragon Boat, tamasha la mbalamwezi au Mid-Autumn festival na sherehe ya kuadhimisha siku ya Taifa. Hadi sasa, likizo tano za kwanza zimeadhimishwa.

  Wiki hii, tamasha la sita na ya pili ya mwisho wa mwaka, ile ya mbalamwezi maarufu kama Mid-Autumn au Moon Festival, inaadhimishwa. Kama likizo nyingine, tamasha la mbalamwezi ina umuhimu mkubwa kwa watu wa China.

  Kwa kweli, miji mikubwa ya Kichina huwa faragha kwani karibu raia wote wa China wanasafiri nyumbani kuwa pamoja na familia zao kwa ajili ya tukio hili. Ofisi za serikali, shule, mabenki na majengo ya biashara binafsi, kwa mfano, hufunga milango yao kutokana na ukosefu wa shughuli na biashara.

  Katika tamasha lililoandaliwa na Beijing Service Bureau for Different Missions katika Wilaya ya Chaoyang jijini Beijing, mwanachama wa chama tawala nchini China, CPC, ambaye alihudhuria sherehe hilo alibainisha wazo hili.

  "Familia huja pamoja katika siku hii na kufurahia mwezi na upendo kati ya wanafamilia." Alisema

  Tamasha hilo lilifanyika katika hekalu la Dong Yue na ratiba ya sherehe hiyo ilijaa mfululizo wa shughuli zilizokuwa zimepangwa kwa ajili ya kuadhimishwa siku ya tamasha hilo pamoja na hotuba kutoka kwa watu maarufu. Hata hivyo kila shughuli ilielekezwa moja kwa moja kwa mbalamwezi.

  Idadi kubwa ya wafuasi wa tamaduni hii wanadai kuwa mwezi ina ishara ya mavuno makubwa. Basi tamasha la mbalamwezi kwa urahisi imetafsiriwa kuwa tamasha la kusherehekea mavuno.

  "Hata ingawa mila zimebadilika kwa muda mrefu na usasa kukita mizizi katika jamii, mshikamano na tamasha la mbalamwezi limebakia sawa. Inahusu ustawi wetu. Ni wakati wa kuangalia nyuma na kutafakari mafanikio tuliyopata. Lakini pia ni juu ya umoja wetu." Afisa mmoja wa serikali ya China alisema.

  Wengine wanaamini kwamba hii ni wakati mzuri kwa ajili ya kukutana, kama vile familia na marafiki kuja pamoja. Wao wanasema kwamba mwezi mpevu inawapa fursa ya kushiriki muungano wa familia.

  Bado wengine wengi wanashikilia kuwa ni wakati wa kutoa shukrani kupitia sala kwa Uungu. Sala maalum hufanyika wakati huu kama vile kuomba baraka ya kuwa na watoto, wanandoa, maisha ya muda mrefu au kwa ajili ya maisha bora.

  Aidha, vijana wa kiume na wale wa kike walioko katika mahusiano wanakienzi tamasha hilo na hivyo wapenzi hao hutumia fursa hiyo kutoa viapo vyao kila mmoja. Kwa wengine hata hivyo, ni nafasi ya kupendekeza uchumba au ndoa. Haya yote hufanyika chini ya mbalamwezi ingaayo.

  Ni jambo linalogusa kila mwanachama na nyanja ya jamii ya Kichina. Hakuna mtu anayehisi kutengwa au kuachwa nje.

  Wakati wa maadhimisho ya wiki nzima, keki spesheli aina ya "mooncakes" uandaliwa na kusherehekewa kwa sana. Hii ndio chakula mahususi ya tamasha hili. Katika utamaduni wa Kichina umbo la duara linaashiria ukamilifu.

  Lakini mbali na umuhimu wake wa jadi kwa Wachina, viongozi wa serikali lililo na makao yake makuu jijini Beijing, wanatumia fursa hii kutoa ajenda ya serikali. Maarufu sana katika ajenda hii ni ujumbe wa China wa kushinikiza utandawazi. Maafisa hao wakidumisha dhamira ya Rais Xi Jinping wa utekelezaji kamili wa ndoto ya serikali yake kuhusiana na mfumo wa uchumi wa Mkanda mmoja njia moja.

  Chini ya mfumo huu, maafisa hao wanasema kuwa nchi wanachama yatashuhudia kuinuka kwa uchumi kulingana na mapendekezo yaliyowekwa. Wao walisifu mpango huo wakisema ni bora sana kwani itainua hasa hali ya maisha na kupunguza makali ya umaskini katika nchi zinazoendelea za Afrika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako