• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • CPC waandaa maonyesho ya mafanikio ya awamu ya kwanza ya Rais Xi ikiwemo kuimarika ushirikiano na nchi za Afrika.

  (GMT+08:00) 2017-10-23 20:17:37

  Theopista Nsanzugwanko katika Beijing

  WAKATI mkutano wa taifa ya 19 wa Chama cha Kikomunisti (CPC) ukiendelea mjini hapa ,Chama hicho kimefungua maonyesho katika ukumbi mkubwa wa vyumba 10 na kuonyesha mafanikio ya awamu ya kwanza ya utawala wa Rais wa nchi hiyo Xi Jinping ikiwemo mahusiano yaliyopo baadhi ya nchi mbalimbali duniani.

  Katika maonyesho hayo,kumewekwa chumba maalum kuonesha juhudi za Kidplomasia zilizofanywa na Rais huyo kwa kuonesha nchi mbalimbali alizotembelea kama Tanzania iliyokuwa nchi ya kwanza ya Afrika kutembelea mara tu alipochaguliwa pamoja na Zimbabwe na nchi nyinginezo.

  Pia kuna picha akiwa na viongozi mbalimbali wa nchi za Afrika katika mikutano ya Ukanda Mmoja Njia Moja uliofanyika mwezi May mwaka huu pamoja na mkutano wa ushirikiano baina ya China na Afrika (FOCAC) uliofanyika nchini Afrika Kusini Mwaka 2015.

  Ukiachilia mikutano hiyo,lakini amekuwa na picha za mikutano mimgine iliyohusisha Afrika pamoja na viongozi waliotembelea nchini China kutoka bara hilo linaloendelea.

  Mbali na mahusiano,pia yanaonyesha mafanikio ya miaka mitano ya Rais huyo katika masuala ya Uchumi, siasa, tamaduni, kijamii, mazingira, ulinzi na usalama na mengineyo katika kuleta maendeleo ya nchi hiyo.

  Tangu kuzinduliwa rasmi ,watu wambalimbali wamekuwa wakimiminika kujionea masuala hayo wakiwemo wanafunzi kutoka shule mbalimbali,wageni na hata wananchi wa kawaida na kushihidia maonyesho hayo yaliyowekwa kwa njia ya picha pamoja na video huku wakishabihisha na maswala halisi ya Rais huyo.

  Akifungua maonesho hayo,katibu wa kamati kuu ya Chama ahicho,Liu Yunshan anasema maonyesho hayo yatasaidia wanachama wa chama hichona wananchi kujifunza kuhusu faida za siasa zinazofanywa na chama hicho.

  "pia kufahamu maendeleo mapya ya ujamaa maalum wenye sifa za kichina kusaidia kuhamasisha kufanya kazi kwa bidii kwa lengo la kufikia malengo ya baadaye"anasema

  Katika maonyesho hayo pia inaonyesha juhudi za Rais huyo katika kupambana na vitendo vya rushwa hivyo kuna picha za maafisa wakubwa waliotuhumiwa kwa rushwa kama Zhou Yongkang, Bo Xilai, Guo Boxiong, Xu Caihou, Sun Zhengcai na Ling Jihua.

  Liu ameeleza kuwa maonesho hayo yatasaidia kuonesha watu mafanikio ya Rais huyo tangu alipoingia madarakani mwaka 2012 kwa alipoitoa nchi hiyo na ilipo sasa katika masuala ya uchumi,jamii na hata ulinzi na usalama kwa kuona matukio mbalimbali kwa picha.

  Mamia ya picha za Rais Xi zikimuonyesha akiwa maeneo mbalimbali ikiwemo akiwa katika mavazi ya kijeshi,katika mikutano mbalimbali ya kimataifa huku nyingine akipiga makofi katika eneo la wanyamapori huko Zimbabwe mbele ya mtoto wa tembo.

  Katika chumba kingine,kuna picha ya Rais Xi akiwa na Malkia Elizabeth na mtoto wake wa kiume Prince Philip,pamoja na ziara zake nyingine katika nchi za Urusi,Ureno na Hungary

  Sehemu nyingine inaonesha akila chakula na wanakijiji alipowatembelea huku akisalimiana na wanakijiji masikini katika jimbo la Hunan akiwa katika mapambano na umasikini jambo lililomfanya kuondoa watu milioni 60 katika hali hiyo.

  Katika maonyesho hayo, kuna sehemu maarufu na inayoonekana kuvutia wengi ni maonesho ya kijeshi ambayo kuna picha mbalimbali zaidi ya 24 ikionesha miakkati ya jeshi hilo kufikia kiwango cha jeshio kubwa duniani.

  Pia kuna sehemu inayoonyesha jinsi nchi hiyo ilivyopendelea kiteknolojia katika Nyanja mbalimbali kwa miaka mitano ya utawaka wa Rais huyo kama teknolojia za mitandao,intelejensia pamoja na matumizi ya Roboti.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako