• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Xi atangaza mwamko mpya katika awamu ya pili ya utawala wake.

  (GMT+08:00) 2017-10-26 20:31:12

  Na Theopista Nsanzugwanko,Beijing

  BAADA ya kufanyika kwa mkutano mkuu wa Chama tawala cha kikomunisti,Rais wa China Xi Jinping ametangaza safu mpya ya uongozi wa kamati kuu ya chama hicho kwa muhula mpya wa miaka mitano,yenye lengo la kuimarisha ustawi na kupanua ushawishi wa taifa hilo kimataifa.

  Chama hicho tayari kilipandisha hadhi ya Rais huyo kwa kuweka itikadi yake katika katiba ya chama, sambamba na viongozi waliopita - Mao Zedong na Dang Xiaoping, na hivyo kumfanya kuwa kiongozi mwenye nguvu zaidi wa taifa hilo katika kipindi cha miongo kadhaa.

  Chama hicho kimeweka kwenye katiba yake masuala kadhaa ikiwemo itikadi ya Rais Xi Jinping ya uongozi wa maendeleo ya nchi yenye nguzo ya ujamaa wenye sifa za kichina,mfumo wa Njia moja na ukanda mmoja ambao unashirikisha nchi za Afrika Pamoja na masuala ya kupambana na Rushwa na ufisadi.

  Akitangaza orodha hiyo Xi ambaye aliteuliwa kama katibu mkuu wa kamati hiyo aliweka wazi kwamba wajumbe hao saba waliteuliwa bila kupigwa katika mkutano mkuu.

  Kamati hiyo inayotambulika kama ''Politiburo" ni kamati ya kisiasa nchini humo yenye nguvu zaidi yenye majukumu ya inayofanya majadiliano ya seara na kufanya maamuzi kuhusu masuala makubwa ya taifa

  Muundo wa Kamati Kuu mpya ya chama cha Kikomunisti, yenye wajumbe saba, unaakisi juhudi za Xi kuimarisha umoja, kwa kufanya nchi yenye maslahi tofauti katika chama hicho chenye wanachama milioni 89, mnamo wakati akitafuta kukiweka katika nafasi nzuri ya kudhibiti masuala ya China ndani na nje.

  Kilichovutia wakati wa kutangazwa kwa uongozi huo mpya, wa wajumbe saba ambao wote wana umri wa zaidi ya miaka sitini ni kuwa kati ya viongozi saba walioshikilia nyadhifa hiyo katika awamu iliyopita ni wawili tu waliosalia ambao ni Katibu Mkuu Xi Jinping na Waziri Mkuu wake Li Kegiang.

  Wajumbe wengine wa kamati hiyo kulingana na mpangilio wa ukuu ni mkurugenzi wa ofisi kuu ya chama ambaye pia ni mkuu wa shughuli za ofisi ya rais, Li Zhanshu, Naibu Waziri Mkuu Wang Yang, mkurugenzi wa ofisi kuu ya utafiti ya chama Wanga Huning, mkuu wa shirika linalohusika na utoaji kazi Zhao Leji, na kiongozi wa chama katika mkoa wa Shanghai Han Zheng.

  Katika uteuzi huo,watu maarufu walioachwa ni pamoja na Makamu wa kwanza wa Waziri Mkuu Zheng Gaol na kiongozi vita dhidi ya ufisadi Wang Qishan pamoja na Liu Yunshan na Yu Zhengsheng.

  Akizungumza wakati wa kutangaza majina hayo,Xi anasema kuwa kuchaguliwa tena kuwa katibu Mkuu wa taasisi hiyo ya watu saba si kukubaliwa kwa kazi nzuri alizofanya tu bali kumuhasisha kufanya kazi zaidi.

  "kwa niaba ya viongozi wapya waliochaguliwa,napenda kutoa shukrani kwa wanachama wa chama wenzangu kwa jinsi walivyotuamini na kutupa nafasi hii,tunahaidi kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo ya Chama"anasema

  Pia, Xi anaeleza kuwa zaidi ya vyama vikubwa vya siasa duniani 452 kutoka nchi 165 wametuma salamu za pongezi kwa mkutano huo uliofanyika na kutoka na maamuzi muafaka.

  Katika baadhi ya mabadiliko ya katiba yaliyofanywa,katika mkutano huo mkuu wa 19 wa chama hicho tawala imejumuisha mfumo wa Njia moja na ukanda mmoja katika katiba yake ikiwa ni njia ya kuhamasisha biashara kutoka China kwenda Ulaya na Afrika kwa kujenga miundombinu.

  Kuhusu,Mawazo ya Rais Xi kuingizwa kwenye Katiba ya chama inaeleza wazi kuendeleza kwa muda mrefu masuala ya maendeleo ya nchi yaliyoanzishwa na Rais huyo.

  Mawazo hayo ya Rais Xi yamejikita katika misingi nane ikiwemo ujamaa katika tabia ya kichina katika mwamko mpya wa uongozi,Maelekezo,aina na mikakati mbalimbali katika masuala ya kisiasa.

  Kuhusu mapambano ya Rushwa na ufisadi kuwekwa kwenye katiba,itahamasisha chama kuongeza nguvu kuhakikisha mapambano ya kupinga rushwa yanaendelea.

  Chama kitafanya kazi ya kutunga sheria za kupambana na vitendo vya rushwa na kuanzisha sehemu ya wananchi kupeleka malalamiko yao kuhusu vitendo vya rushwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako