Na Eric Biegon katika Beijing, China.
Rais Xi Jinping sasa anasema atatumia hadha aliyotunukiwa katika jamii ya Kichina kuboresha maisha ya wengi katika nchi zinazoendelea. Xi anasema mawazo yake sasa zinatoa mbinu mbadala kupambana na changamoto zinazokabili nchi nyingi.
Akizungumza mara tu baada ya Chama cha Kikomunisti kuweka mawazo yake katika katiba ya chama hicho, kiongozi huyo wa Kichina alisema kuwa njia, nadharia, mfumo na utamaduni wa Ujamaa yenye sifa za Kichina zimeendelea kukua, na kuingia viwango vipya na vitasaidia nchi nyingine zinazoendelea kufikia upeo wa maendeleo.
"Inatoa fursa mpya kwa ajili ya nchi nyingine na mataifa ambazo zinataka kuongeza kasi ya maendeleo yao huku zikihifadhi uhuru wao, na inatoa hekima ya Kichina na mbinu ya Kichina kutatua matatizo zinazowakabili wanadamu." Alieza mkutano wa CPC.
Tangu aingie madarakani, Rais Xi amekuwa akisukuma kuweko kwa maendeleo ya jamii ya pamoja, na daima kuhamasisha mageuzi ya mfumo wa utawala wa kimataifa.
Mkanda mmoja njia moja katika Katiba
Lakini hili kuafikia lengo hili, Rais Xi amebuni mipango kadhaa muhimu, mojawapo ni mfumo wa Mkanda mmoja njia moja (OBOR) ambayo yeye yeye anasema itakuwa kichocheo kikubwa kwa ajili ya maendeleo katika dunia ya sasa.
Inaonekana azma hii imewekwa nguvu zaidi kwani kati ya marekebisho mengine makubwa kwa katiba yake, chama kikomunisti imejumuisha mfumo huo wa OBOR katika katiba yake. Mradi huo wa karne kama inavyotazamiwa na Rais Xi sasa ni sehemu ya katiba ya chama na nchi.
Ndani ya katiba iliyofanyiwa marekebisho ya Chama cha Kikomunisti cha China, chama hicho kinasema kwamba .... (China) itazingatia sheria wakati wa kutafuta maslahi ya pamoja, shughuli ya kujenga jamii ya pamoja ya baadaye kwa ajili ya watu, kwa kufuata kanuni ya kufikia ukuaji wa pamoja kwa njia ya majadiliano na ushirikiano na kutekeleza mpango wa mkanda mmoja njia moja."
Baadhi ya nchi za Afrika kama vile Kenya na Ethiopia ni miongoni mwa nchi za kwanza zilizotia saini makubaliano na China kuwa sehemu ya mfumo huo. Mara tu baada ya kuzinduliwa kwa mfumo huo jijini Beijing mwezi Mei mwaka huu, Rais Xi alitangaza milioni 100 dola za Marekani zilizotengwa na serikali yake kusaidia mpango huo. Aidha kiongozi huyo wa China alizindua mfuko wa Silk Road Fund kufadhili miradi mikubwa katika nchi wanachama.
Hivi karibuni, Beijing ilitangaza kuwa idadi ya nchi zinazoendelea zimeonyesha nia ya kuingia katika mpango huo. Alisema nchi kadhaa zimetuma maombi ambazo zimepokelewa na kwa sasa zinaendelea kukaguliwa lakini ikasisitiza kwamba nchi zote, hasa zile zinazoendelea ziko wazi kujiunga.
Wengi ndani ya chama cha CPC wanaona mpango huo wa mkanda mmoja njia moja kama njia bora ya Rais Xi kuunganisha nchi zilizoko bara Asia, Afrika na Ulaya.
Mawazo ya Xi
Siku ya Jumanne, Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), iliinua hadhi ya rais Xi Jinping katika uongozi wa nchi hiyo kwa kuweka mawazo yake katika katiba ya chama. Hatua hii ya chama tawala kwa hatua moja ikamuidhinisha Rais Xi kama kiongozi mwenye nguvu zaidi nchini China baada ya mwanzilishi wa taifa Rais Mao Zedong.
Uamuzi juu ya iwapo chama ingeweka mawazo ya Xi ndani ya katiba ya chama ulikuwa unasubiriwa sana. Lakini baada subra, Chama cha Kikomunisti, ambacho kimekuwa kikikutana kwa wiki moja iliyopita, hatimaye ilipiga kura bila kupingwa na kubuni "Mawazo ya Xi" kama sehemu mpya ya mwongozo wa chama.
Zaidi ya wajumbe 2,300, ambao wamekuwa wakihudhuria mkutano katika jumba la Great Hall of the People iliyoko mji Mkuu wa Beijing, waliidhinisha ushirikishwaji wa mawazo Xi Jinping kuhusu Ujamaa yenye sifa za Kichina ili kuleta mwamko mpya katika jitihada za "kushughulikia maswala makubwa yanayohusiana na nyakati hizi.
Hadhi mpya aliyopewa rais Xi inaonekana kuimarishwa hata zaidi kwani wakati wa kupiga kura, hakuna mjumbe hata mmoja aliyepinga hoja ya kuweka mawazo yake katika katiba ya chama, na kuashiria mwamko mpya China.
Muda mfupi baada ya tukio hilo, Xi alitoa wito kwa wajumbe wa CPC "kusoma, kukagua, kutumia na kutekeleza katiba ya chama, na kufuata kwa karibu fikra za Kamati Kuu ya CPC katika mwelekeo wa kisiasa na vitendo."
"Katika chama chetu, kila mmoja avute hewa sawa na wengine, kushiriki hatima sawia, na kuishi kwa kushikamana," alisema.
"Matarajio ya watu kuishi maisha bora lazima iwe lengo la juhudi zetu." Alisisitiza.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |