• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mtandao wa reli nchini China wazidi kushika kasi.

  (GMT+08:00) 2017-11-14 08:59:21

  Na Theopista Nsanzugwanko,Beijing

  CHINA ni nchi inayoongoza kwa kuwa na usafiri wa Treni za Chini (Subway)zinazotoa usafiri wa wananchi wake kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa utaratibu maalum jambo linalosaidia kupunguza msongamano barabarani katika nchi hii yenye idadi kuwa ya watu zaidi ya bilioni moja.

  Mbali ya kufanikiwa kwa kiasi kikubwa katika ujenzi wa usafiri huo wa chini ya ardhi,bado wanaendelea kupanua mtandao wa reli hizo kwa kasi hasa katika miji yake mikubwa ya Shanghai, guangzhoe,Beijing na Tianjin huku mwishoni mwa mwaka huu wakijiandaa kuanza kutoa huduma kwa kutumia treni za aina hiyo zinazojiendesha zenyewe (Automatic Treni

  Beijing ukiwa ni mji unaoongoza kwa kuwa na mtandao mpana wa reli nchini humo zilizoanza kutoa huduma 2002 wakati huo kukiwa na njia mbili tu lakini sasa wana njia 19 huku wakitarajia kuwa na njia 30 zitakazosafirisha abiria zaidi ya milioni 18.5 katika kilometa 999 ifikapo mwaka 2020.

  Miji mingine kama Guangzhou ulioko katika jimbo la Guangdong ni ya nne kwa ujenzi wa mtandao wa Reli kwa njia ya kwanza ya reli hiyo ilianza kujengwa mwaka 1993 na kuzinduliwa rasmi miaka minne iliyofuata yaani mwaka 1997 ikiwa na njia tano.

  Lakini mpaka kufikia mwaka jana ina njia kumi zenye uwezo wa kusafirisha watu milioni saba kwa siku na kwa kufanya kazi katika vituo 184 zenye km 260.5.

  Katika kuongeza mtandao huo ,njia nne mpya zinajengwa huku nyingine zikipanuliwa hivyo kufanya baada ya njia zote kukamilika kufikia mwaka 2020 kutakuwa na kilometa zaidi ya 600.

  Reli ya Shanghai ilizinduliwa mwaka 1993 na ndiyo yenye mtandao mkubwa wa njia ya reli duniani kwa urefu wa njia ya kusafiri huku ikiwa ya pili duniani kwa wingi wa vituo 364 katika njia 14 zenye kilometa 588

  Kwa wastani wa watu milioni 10 wanatumia usafiri huo kila siku,huku wakiwa na mikakati ya kufikia njia 25 zenye urefu wa zaidi ya km 1,000 kufikia mwaka 2025.

  Katika mji wa Beijing,'Subway' inazidi kuendelea kupanua mtandao wake kutoka kilometa 574 zenye njia 19 mpaka kilometa 900 zitakazokuwa na njia 30 ifikapo mwaka 2020 huku wakitarajia kusafirisha abiria milioni 15 kwa siku.

  Katika mji huo mkuu wa nchi hiyo wenye idadi ya watu milioni 23 ili kufikia malengo hayo,mwisho wa mwaka huu njia mpya tatu zitakamilika na kufanya kuwa na njia 22 zenye kilometa 610.

  Kwa sasa watu milioni 11.5 wanatumia usafiri huo kwa siku huku ukitoa ajira kwa watu zaidi ya 30,000 katika treni 8,835walizonazo sasa.

  Mkurugenzi wa kituo cha kudhibiti usafiri wa treni, Zhan Minghui,anaeleza kuwa njia namba 10 yenye vituo 45 katika kilometa 54 ndiyo ina msongamano mkubwa kila wakati na kutumiwa na wasafiri zaidi ya milioni 1.7 kwa siku.

  Usafiri huo katika mji wa Beijing ulianza katika njia ya kwanza mwaka 1969 na mpaka mwaka 2020 kulikuwa na njia mbili tu zenye kilometa 54 huku ikisafirisha watu milioni mbili kwa siku.

  "baada ya miaka 17 sasa kuna njia 19 zenye mtandao wa kilometa 574 na kusafirisha wasafiri milioni 11.5 kwa siku huku kukiwa na vituo 345 .

  Inaelezwa kuwa kati ya mwaka 2003 na 2016,zaidi ya fedha za China RMB bilioni 600 zimewekezwa katika kupanua mtandao huo wa Reli.

  Katika kituo cha kuongoza na kusimamia usafiri huo wa Reli chenye wafanyakazi zaidi ya 400 wanafanya kazi kwa kutumia njia ya kuangalia sehemu mbalimbali za usafiri huo ambapo kila njia na kituo kuna kamera zinazowaonyesha.

  Wakiwa na takwimu za wasafiri wa kila siku wanaotumia usafiri huo pamoja na mwenendo mzima wa usafiri huo kwenye mji huo ikiwemo udhibiti wa ajali iwapo itatokea.

  Anazungumzia kuwa iwapo itatokea ajali ya moto au yeyote ,kuna mlio maalum utatokea na mitambo yote kuzima kwa lengo la kujulisha watoa huduma kutokana na kuwa umbali wa kituo kimoja mpaka kingine ni chini ya dakika mbili.

  Mikakati inaendelea kuendelea kutanua mtandao huo kwa miji jirani na Beijing ikiwemo kufika jimbo ya Hebei na pia kuunganisha katika njia mpya ya kilometa 150 kwa saa kutoka Uwanja mpya wa Ndege wa Beijing unaoendelea na ujenzi.

  Mwendo wa Treni hizo za Chini katika mji wa Beijing ni kilometa 80 kwa saa katikati ya mji na kilometa 100 kwa saa kwa pembeni ya mji.

  Akizungumzia treni za aina hiyo zinazojiendesha zenyewe (automatic) bila kuendeshwa na binadamu inafanyiwa majaribio katika eneo la Fan Shan lililopo kilometa 50 kutoka Beijing na zitakuwa 16 zinatarajiwa kuanza kazi mwishoni mwa mwaka huu katika njia ya kilometa 14.4.

  Meneja Mkuu wa Treni hizo zinazojiendesha ,Xu Ding anasema kila behewa la abiria gharama yake ni pesa za China RMB milioni nane na kila treni inahitaji behewa hizo nne.

  Anasema wanatumia teknolojia ya 4G kuwasiliana na Chumba cha kuongozea treni hizo ikiwa ni mara ya kwanza duniani kutumia teknolojia hiyo.

  Alisema treni hizo zinazoendeshwa bila kutumia binadamu baadaye zitasambazwa katika maeneo mbalimbali ya mji wa Beijing na katika miji 10 ya nchi hiyo.

  Anaweka wazi kuwa reli kwa ajili ya treni hizo ni sawa na za kawaida huku zikitembea kwa wastani wa kilometa 100 kwa saa ikianza kazi lakini kwa sasa ikiwa kwenye majaribio wanatumia mwendo wa kilometa 80 kwa saa kwa kuwa umbali wa vituo ni mfupi tofauti na treni za kawaida.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako