• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yashuhudia ukuaji mkubwa katika sekta ya anga

  (GMT+08:00) 2017-11-14 09:00:42

  Na Eric Biegon mjini Beijing, China.

  China kwa sasa inajenga mojawapo ya uwanja mkubwa wa ndege duniani. Uwanja huo mpya wa Beijing Daxing Airport inajengwa kwa gharama ya bilioni 12 dola za Marekani na itakuwa uwanja wa ndege wa tatu katika mji mkuu wa China, Beijing.

  Mara tu baada ya kukamilika kwake, mradi huu mkubwa utaingia kwenye daftari za kumbukumbu kama uwekezaji wa miundombinu moja mkubwa zaidi chini ya uongozi wa rais wa sasa wa China Xi Jinping.

  Mamlaka ya China imeweka wazi kuwa uwanja huo mpya wa ndege inaundwa ili awali iweze kushughulikia abiria milioni 45 lakini hatimaye kugonga abiria milioni 100 na tani milioni 4 za mizigo kila mwaka. Mji mkuu wa China ni nyumbani mwa watu milioni 23 kwa sasa.

  Shughuli za ujenzi wa uwanja huo mpya zilizinduliwa mwaka 2014 na inatarajiwa kwa zitamalizika mwezi Oktoba mwaka 2019 wakati uwanja huo itaanza rasmi shughuli za usafiri. Wazo la ujenzi wake ilitokana na msongamano unaoshuhudiwa katika uwanja wa Beijing Capital International Airport, BCIA na ule wa Beijing Nanyuan Airport, ambazo zote ziko katika mji mkuu, Beijing.

  "Zaidi ya asilimia 90 ya kuinua boma la udongo na uimarishaji wa msingi ulikamilika mwisho wa Septemba 2017," Mhandisi wa mradi huo alisema.

  Utawala wa Usafiri wa Anga China (CAAC) inasema kuwa Beijing Capital International Airport kwa sasa ni uwanja wa ndege yenye shughuli nyingi zaidi nchini China.

  Mamlaka hiyo ilifichua kuwa BCIA ilibeba zaidi ya abiria milioni 90 mwaka 2016 peke yake, na kuzidi uwezo wake iliyoundwa ya abiria milioni 82.

  CAAC inaweka idadi ya safari za ndani na kimataifa zilizolifanyika mwaka jana nchini China kuwa milioni 487.

  Imebainika kuwa kuongezeka kwa usafiri wa anga nchini China kwa kiasi kikubwa kinaendeshwa na raia wa China ambao wanatumia kiasi kikubwa cha fedha kwenye likizo ya ndani na nje ya nchi.

  Kwa mujibu wa msemaji wa mradi huo Zhu Wenxin, wanaosafiri kuelekea kwenye uwanja huo wa ndege mpya watakwenda kwa kupitia barabara pana au expressways na treni yenye kasi.

  "Abiria watakaowasili kupitia treni ya chini kwa chini (Subway), barabara pana (Expressway) au treni kasi watatumia lifti moja kwa moja hadi kwenye kumbi ya kuondoka iliyoko juu katika majengo hayo bila ya kutembea mbali." Alisema

  Vifaa vingine katika uwanja huo wa kisasa ni pamoja na hoteli ya kimataifa yenye vyumba 500.

  Wafanyakazi katika mradi huo wanatumaini kumaliza kufunga pazia la kioo na paa la uwanja huo kabla ya mwisho wa 2017.

  Eneo ambapo uwanja huo wa ndege umekalia ni mita milioni 7.5 mraba, sawa na viwanja 44 vya soka.

  Wakati huo huo, mashirika ya ndege tayari yameanza kuhamia uwanja huo mpya na kuanza ujenzi wa ofisi zao. Barabara zinazounganisha hadi uwanja huo wa ndege tayari zimekamilika.

  Zhu anasema mashirika makuu mawili ya ndege nchini China, China Eastern Airlines, na China Southern Airlines, zitaamia uwanja huo mpya punde tu baada ya kukamilika kwa ujenzi, na kupunguza msongamano unaoshuhudiwa kwa sasa.

  Ujenzi wa jengo hilo la kifahari linaendeshwa na makampuni ya ujenzi tatu na jumla ya wafanyakazi wa ujenzi 20,000.

  Uwanja huo mpya wa ndege ni mojawapo ya maendeleo mahususi ya utawala wa Rais Xi Jinping, miaka 5 baada ya kuchukua hatamu uongozi wa nchi hiyo yenye uchumi wa pili kwa ukubwa duniani.

  "Ni mfano wa kuigwa na inadhihirisha uwezo wa China ya uzalishaji wa kitaifa." Akasema msemaji wa mradi.

  Mradi huu unafanyika huku kukiwa na shinikizo la China kuwa moja ya kitovu kinachoongoza duniani kwa mambo ya angani. Nchi hiyo pia imeanzisha ujenzi wa ndege za usafiri. Ndege ya kubeba abiria iliyotengenezwa China maarufu C919 tayari imefanikiwa kumaliza maelfu ya maili katika safari za majaribio.

  Uvumbuzi huu wa karibuni kutoka China ina maana kwamba Boeing na Airbus sasa zimepata mshindani imara wa kukabiliana nao katika soko la anga.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako