• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya watu kuongezeka China baada ya kutekelezwa sera mpya kupanga uzazi

    (GMT+08:00) 2017-11-24 15:29:10

    Na Theopista Nsanzugwanko mjini Beijing

    SERA ya uzazi wa mpango nchini China iliyoratibishwa mwaka 1979 na kuanza utekelezaji wake mwaka 1980 ambapo familia zilitakiwa kuzaa mtoto mmoja tu.

    Kuratibishwa kwa sera hiyo kulitokana na ongezeko kubwa la watu nchini humo ambapo mwaka 1949 walikuwa watu milioni 54 lakini kufikia mwaka 1978 walifikia watu milioni 1978.

    Ikiwa ni tofauti kubwa kwa nchi za Afrika ambapo familia moja inaweza kuzaa watoto hata 10,kutokana na malengo waliyokuwa nayo sera hiyo ilitiliwa mkakati usio wa kawaida kuhakikisha inafanikiwa.

    Katika miaka 30 ya utekelezaji wake,ilifanikiwa na kuanza kuzoeleka lakini mwaka 2015 ikiwa ndiyo mwisho wa sera hiyo walitambulisha Sera mpya ya kuruhusu familia kuzaa watoto wawili.

    Kuanza kwa sera hiyo mpya kulitokana na nchi hiyo kubaini kuwepo wazee wengi kuliko nguvu kazi ambayo wengi wao ni vijana,kutokana na kipindi hicho kuzuia kuongezeka kwa watu milioni 400.

    Hatua hiyo inaelezwa kutokana na Sensa ya Taifa ya nchi hiyo kuwa mwaka 1964 kulikuwa na watu milioni 695,mwaka 1982 walikuwa bilioni moja na kufikia mwaka 2000 walifikia bilioni 1.2 na mwaka 2010 bilioni 1.3 na mpaka mwaka huu inakadiliwa kufikia bilioni 1.4.

    Inaelezwa kuwa baada tu ya kuruhusiwa kwa sera hiyo mpya Januari mwaka 2016 watoto zaidi ya milioni 17 wamezaliwa nchini humo.

    Tume ya Taifa ya Afya na Uzazi wa mpango nchini humo inaeleza kuwa watoto wanaofikia milioni 17.86 walizaliwa na kati yao asilimia 45 ni kutoka katika familia ambazo tayari zilikuwa na mtoto mmoja.

    Profesa katika masuala ya jamii anayefanya kazi na kituo cha kushughulikia idadi ya watu na hali ya Jamii katika Chuo Kikuu cha Renmin,Yang Juhua anasema serikali inahamasisha wanandoa kupata mtoto wa pili.

    "serikali inahamasisha wanandoa kupata mtoto wa pili baada ya kupitishwa kwa sera hiyo mpya kwa ajili ya maendelea ya familia na kutoa huduma bure ya matunzo mbalimbali kwa watoto chini ya miaka mitatu"anasema

    Anaeleza kuwa ingawa katika utafiti uliofanywa Desemba mwaka jana na Shirikisho la wanawake nchini China na kituo cha uvumbuzi cha taifa inaonesha katika familia 10,300 zenye mtoto mwenye umri wa zaidi ya miaka 15,asilimia 53.3 hawako tayari kupata mtoto mwingine kwa sasa.

    Huku,asilimia 20.5 pekee wakiwa tayari kupata mtoto wa pili na asilimia 26.2hawana uhakika na majibu yao,huku wengi wanaoishi katika miji iliyoendelea wakiwa hawako tayari kuongeza mtoto.

    "ababu kubwa wanayotoa kutoridhia kupata mtoto mwingine ni pamoja na gharama kubwa za maisha kama matibabu,shule pamoja na ubora wa bidhaa za watoto"anaeleza

    Anasema kuwa katika miaka ya 1970 kwa wastani wanawake wa nchini China walikuwa na watoto milioni 4.77 lakini idadi hiyo ilishuka kufikia milioni 1.64 mwaka 2011.

    "bila ya kuwepo na sera husika,kwa sasa kungekuwa na watu walioongezeka milioni 400 " alisema Yang.

    Anaweka wazi kuwa kwa sasa umri wa kuishi kwa wananchi wa China ni miaka 79 kwa wanawake na 75 kwa wanaume huku wastani wa jumla ikiwa miaka 76.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako