• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Treni za mwendo kasi: China kujenga mtandao mpya wa kilomita 23,000 kufikia 2030

    (GMT+08:00) 2017-11-24 16:08:29

    Na Eric Biegon katika Beijing, China

    Tangu China ilipozindua treni za mwendo kasi mwaka 2008, nchi hiyo imejenga kilomita 22,000 za reli, na kuwa mtandao mkubwa zaidi duniani kwenye masuala ya mfumo huo wa usafiri ikilinganishwa na mataifa mengine. Lakini shughuli hii bado haijakamilika kwani uongozi wa nchi hiyo unapanga kujenga kilimita 23,000 mpya za mtandao wa treni za mwendo kasi na kufikisha jumla ya mtandao huo urefu wa kilomita 38,000 kufikia mwaka wa 2025 na hatimaye kilomita 45,000 mwaka wa 2030.

    Naibu Mkurugenzi wa chuo cha sayansi ya reli nchini China, CARS, Zhao Zhangshan, anasema mtandao huo wa reli haujasaidia tu kuboresha mtandao wa barabara nchini China bali pia umeweza kuinua viwango vya uchumi katika majimbo yote nchini humo.

    Zhao alifichua kuwa abiria bilioni 7 tayari wameweza kusafirishwa kwa kupitia mtandao huo mpya nchini ndani ya miaka saba iliyopita bila kushuhudia ajali yoyote.

    "Ubinifu wetu na teknologia tunaotumia ni wa kipekee. Mtandao huu ulijengwa na raia wetu na ni dhabiti mno. Tumefaulu kuwekeza kwenye mfumo wa usafiri ulio salama zaidi duniani." Alisema Zhao.

    Wakati huo huo, China inasifika kote ulimwenguni kwa kuwa taifa la pekee lenye kutoa huduma kupitia treni za mwendo kasi kwani vyombo hivyo vya usafiri vina uwezo wa kusafiri kilomita 350 kwa saa.

    Mfumo huu mpya ulianza kufanya kazi Septemba 21, 2017. Tangu mwaka wa 2008 hadi 2016, treni za kwenda kwa kasi China zilikuwa na uwezo wa kusafiri kilomita 300 kwa saa. Reli ya kuunganisha Beijing-Shanghai yenye ukubwa wa kilomita 1,318 ilizinduliwa kwa matumizi ya usafiri wa umma mwaka 2012 na sasa treni spesheli aina ya "Fuxing" zinahudumu kwenye mtandao huo.

    Safari ya kuelekea Shanghai kutoka Beijing, kwa mfano, treni hiyo uchukua masaa 4, dakika 28 pekee hata baada ya kusimama kwa kipindi kifupi katika vituo kadhaa.

    Huku ikiunganisha mji mkuu wa China ulioko kaskazini na kitovu cha biashara kwenye kusini mwa nchi hiyo, reli ya kisasa ya Beijing-Shanghai ni moja yenye shughuli nyingi zaidi nchini, huku takwimu zikionyesha kuwa unasafirisha zaidi ya abiria milioni 100 kwa mwaka.

    Zhao anasema kuwa treni hizo, zinazoashiria mwamko mpya China, viliundwa na viwanda vilivyoko nyumbani China – huku akizisifia kuwa za laini mno. Aidha mtandao huo umeboreshwa zaidi kwani makocha yake hayana kelele, ni rahisi, yenye mazingira ya kirafiki, starehe na gharama nafuu.

    Zaidi ya hayo, viti vyake ni pana huku kukiwa na nafasi nzuri ya kupumzika. Kwa mara nyingi ni vigumu kutofautisha starehe itokanayo na usafiri huu na ule wa daraja la kwanza katika ndege.

    Treni hii ya mwendo kasi aina ya "Fuxing" imeboreshwa kwa kiwango kikubwa ikilinganishwa na ile ya awali inayojulikana kama "Hexie" au "Maelewano." Mfumo ya ufuatiliaji wa kisasa ulioezekwa ndani mwa treni hiyo, moja kwa moja unathibiti kasi yake endapo hali ya dharura au hali isiyo ya kawaida itatokea.

    Treni hizo mpya tayari zimeuzwa kwa mataifa kama vile Indonesia, Urusi, Iran na India; wakati wahandisi kutoka China wanaendelea kujenga mtandao wa reli wa mwendo kasi katika bara la Asia na Ulaya.

    Lakini si hayo tu, kwani, kama sehemu ya jitihada zake wa uvumbuzi wa teknolojia, China mnamo Agosti 30, 2017 ilitangaza kuwa itabuni "treni ya kupaa" iliyo na uwezo wa kusafiri kwa kilomita 4000 kwa saa, hii ikiwa ni mara 5 zaidi kuliko ndege za kusafirisha abiria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako