• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Je, kwa nini "darasa la maadili ya wanawake" limezusha hasira kote nchini China?

    (GMT+08:00) 2018-01-10 15:21:16


     

    Katika miaka ya hivi karibuni, shule za kuwafundisha maadili wanawake kufuata zimeibuka katika sehemu mbalimbali nchini China, na zinasisitiza kuwa hadhi ya wanawake na kazi havipaswi kuwa pamoja, na kuwalazimisha wanafunzi wa kike kujifunza kazi za nyumbani. Shule moja inayoitwa "shule ya elimu na utamaduni wa jadi ya Fushun" iliyopo kaskazini mashariki mwa China imezusha malalamiko makubwa kutokana na kuwafundisha wanawake "maadili ya kike". Shule hiyo inasema wanawake wanapaswa kuwa tabaka la chini, hawapaswi kujibu wanapopigwa au kukerwa, hawapaswi kutaliki au kutalikiwa, kwani huko ni kwenda kinyume na maadili ya wanawake, kuagiza chakula na kutosafisha vyombo ni kinyume na maadili ya wanawake. Kutokana na kuongezeka kwa malalamiko katika jamii na mitandao ya kijamii, serikali ya mji huo imeagiza shule hiyo ambayo imekuwepo kwa miaka sita ifingwe.

    Mmoja wa watu waliowahi kushiriki kwenye darasa hilo, ameeleza furaha yake baada ya kuona shule hiyo kufungwa. Alipokuwa na umri wa miaka 13, mama yake aliona yeye ni mjeuri na alimpeleka kwenye shule hiyo, na kutarajia kuwa elimu ya kitamaduni inaweza kumfanya awe na adabu na maadili. Lakini huko shuleni "alilazimishwa kusafisha choo kichafu sana." Akaona kuwa binadamu wa kawaida hawawezi kuvumilia kambi ya mafunzo ya siku saba, na alitoroka usiku wa siku ya nne aliamua kuingia mitini. Watu walioelimika katika miji mikubwa kama Beijing na Shanghai, wanashtushwa na kushindwa kuamini kama kuna darasa la maadili ya wanawake. Lakini ukweli ni kwamba wazo hilo lililopitwa na wakati, bado lipo katika baadhi ya miji midogo na haswa maeneo ya vijijini.

    Hata hivyo utamaduni wa kimwinyi unaotetewa kwa kisingizio cha kulinda utamaduni wa jadi, ni jambo la kutia wasiwasi. Mtaalamu wa masuala ya wanawake wa China Xie Lihua anasema wanawake hukosa elimu na msaada wa kijamii, na wanawake wa maeneo ya vijijini kukosa ulinzi wa kisheria, kufanya wazo hilo baya kuenea kwa baadhi ya watu. Amesema wanawake wa vijijini pia wanakabiliwa na matatizo kama kudhalilishwa kingono na kutokuwa na haki ya kumiliki ardhi. Lakini anaona hakuna haja ya kuangalia kwa makini sana madarasa kama hayo, mkondo wa historia hauwezi kugeuka, na jamii ya China kwa sasa inaelekea kuwa ya usawa wa kijinsia.

    Idadi ya wanawake mabilionea nchini China inashika nafasi ya kwanza duniani, lakini kimapato, wastani wanapata asilimia 35 chini ya mapato ya wanaume.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako