• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kutoka nyumbani bila ya pochi ni zoea jipya la wachina

    (GMT+08:00) 2018-01-10 16:07:20


    Takwimu zimeonyesha kuwa kutokana na miamala mingi kufanyika kwa njia ya simu za mkononi, mtindo wa kimaisha wa wachina umebadilika kinyemela, na kutoka nyumbani bila a kubeba wallet kumekuwa ni mazoea mapya kwa wachina, na pia ni mtindo mpya duniani. Mwezi Machi maka jana miamala iliyofanyika kwa njia ya simu za mkononi ilichukua asilimia 82 ya malipo yote katika mtandao wa ulipaji wa Zhifubao yaani AliPay, na kuweka rekodi mpya. Sababu moja ya kuongezeka kwa ulipaji wa kutumia simu za mkononi, ni kutumika kwa wingi kwa code ya kulipa. Mamilioni ya maduka katika mitaa mbalimbali nchini China yametimiza maendeleo ya kidigitali katika mchakato wa kupokea pesa kwa kutegemea karatasi yenye code hii ya kulipia. Hivi sasa, haijalishi kama ni kulipia chakula kwenye mgahawa, au kufanya manunuzi madukani, na hata unaponunua matunda na mboga kando ya barabarani, unaweza kutumia simu za mkononi ku-scan code.

    Usafiri wa umma ni njia muhimu ya usafiri wa mjini, lakini kwa muda mrefu kutokana na mahitaji kwa mawimbi ya mawasiliano na muda, ulipaji wa kutumia simu za mkononi umekuwa ukikwamishwa, na mazoea ya ndani ya China na nje ya nchi ni kubeba pesa kidogo au kutumia smart-card ya usafiri. Kutokana na maendeleo ya teknolojia, mwaka jana ulipaji wa kutumia simu za mkononi uliweza kutumiwa katika mabasi na subway katika miji zaidi ya 30, na watu wengi wanasema "sababu ya mwisho ya kutoka nyumbani na wallet imeisha".

    Wakati huohuo, idara mbalimbali za huduma za umma zimefungua "madirisha" katika mtandao wa ulipaji wa Alipay ili wakazi waweze kulipa na kupata huduma hizo wakiwa nyumbani bila ya kuhitaji kutoka nje. Mwaka jana, watu milioni 200 walitumia mtandao huo kulipia pensheni za jamii, kulipa usafiri na mambo ya kiraia na huduma nyingine zaidi ya 100.

    Ulipaji wa kutumia simu za mkononi pia umeenea katika nchi na sehemu nyingine nje ya China. Mwaka jana, malaki ya maduka ya nchi 36 za nje yamejiunga na mtandao wa ulipaji wa Alipay, na oda zilizolipwa katika mtandao huo ziliongezeka kwa asilimia 306 kuliko mwaka 2016, na kwamba mtindo huo wa kimaisha unaanza kutumika kote duniani.

    Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na kampuni ya utafiti wa soko ya Forrester, soko la ulipaji wa kutumia simu za mkononi la China ni kubwa mara 90 kuliko la Marekani, na kuongoza duniani. Na uchunguzi uliowashirikisha vijana wa nchi 20 unaonesha kuwa ulipaji wa kutumia siko za mkononi wa Alipay, treni ya mwendo kasi, biashara ya kwenye mtandao wa internet na baiskeli ya kutumiwa kwa pamoja ni vitu vinne muhimu zaidi vilivyobuniwa nchini China.

    Ulipaji wa kutumia simu za mkononi sio tu umetoa urahisi kwa mtu mmoja mmoja, bali pia umetoa mchango kwa jamii. Kwa upande mmoja, ulipaji wa kutumia simu za mkononi unaweza kuongeza alama za imani, kadri matumizi yako yanavyozidi kuongezeka, ndivyo huduma za kifedha unazoweza kupata zinavyoongezeka. Na hata duka la kuuza chapatti au kibanda cha mboga kinaweza kupata mkopo kwa kufungua code ya kulipia. Credit ulizopata kupitia kulipa kwa simu za mkononi zinaweza kusamehe malipo ya awali, ambayo unaweza kuyatumia mahali pengine. Vilevile katika usafiri wa kutumia mabasi, kampuni ya mabasi inaweza kuamua kama itaongeza mabasi kwa kuangalia idadi ya abiria wanaopanda na kushuka kwenye mabasi, ili kutatua msongamano wa magari mjini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako