• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mahakama yaamuru mtoto alipe mamake malipo ya malezi

  (GMT+08:00) 2018-02-02 15:52:21


  Mahakama ya juu zaidi kisiwani Taiwan, nchini China imeamuru kuwa mwanamume mmoja amlipe mamake zaidi ya dola za kimarekani elfu 750 kugharamia malezi na masomo ya kuwa daktari wa meno. Habari zimewahi kuripoti kuhusu wazazi kuwashtaki watoto wao ili kupata usaidizi wa kifedha lakini kesi hii ni tofauti kwa sababu inahusisha mkataba wa maandishi uliofikiwa kati ya mzazi na mwanawe

  Uamuzi wa mahakama ya juu zaidi kisiwani Taiwan ulieleza kwamba mama yake anakabiliwa na deni la dola elfu mia sita alilopata akiwalea na kuwasomesha watoto wake wawili tangu kutengana na mumewe.

  Alikuwa na wasiwasi kwamba wanawe huenda hawatatimiza wajibu wa kumlinda siku za baadaye, ndipo akaandikisha mkataba na wanawe wa jinsi watakavyomlipa pesa alizotumia kuwaelimisha na kuwatunza.

  Kwa mujibu wa mkataba huo ulioletwa mbele ya mahakama, wanawe wawili, punde tu wanavyohitimu kama madakatari wa meno, walifaa kulipa mama yao asilimia 60 ya mapato yao kila mwezi.

  Mwanawe wa pili ana kliniki yake ya meno, na alimuuliza amlipe kulingana na mkataba wao.

  Mwanawe naye amesema kwamba wakati alipoingia mkataba huo, alikuwa na miaka ishirini tu, na ni ukiukaji wa haki zake kama binadamu na si halali.

  Mahakama ya Juu zaidi ilishikilia msimamo kwamba sheria ya mizozo ya kiraia inakubali mtu kufanya mkataba na kuna kiwango fulani kinachoruhusiwa wakati wa malipo.

  Mahakama hiyo pia imesema kwamba makubaliano hayo kati ya mzazi na watoto haitaathiri maisha ya wanawe mwanamke huyo, watamudu, na pia mkataba haujakiuka haki yake kwani alikuwa ametimiza umri wa mtu mzima

  Mahakama imeamua kwamba mwanawe ambaye ni dakatari wa meno tangu mwaka wa 2003, atimize matakwa ya mkataba wake na mama yake kwa kumlipa deni ambalo limefika kwa dola milioni moja za Marekani

  Nchini China, wazazi wengi bado wana desturi ya kuwategemea watoto wazima kuwatunza baada ya wao kuzeeka.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako