• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Utalii umekuwa motisha muhimu kwa ongezeko la uchumi duniani

  (GMT+08:00) 2018-01-17 17:44:36


  China hivi leo imetoa waraka kuhusu maendeleo ya utalii ya mwaka 2016-2017 nchini China na dunia nzima. Waraka huo wenye kauli mbiu ya "mageuzi na uvumbuzi wa sekta ya utalii ya China katika zama mpya", umetoa makadirio kuhusu maendeleo ya utalii katika mwaka 2017-2018 nchini China na dunia nzima, na kuchambua masuala nyeti ya maendeleo ya utalii. Waraka huo umekadiria kuwa idadi ya watalii nchini China itakuwa karibu bilioni tano, na mapato ya utalii yanatarajiwa kuwa yuan trilioni 4.4, sawa na dola za kimarekani bilioni 680, na kuongezeka kwa asilimia 12.5.

  Waraka huo pia unasema, mwaka 2017 hali ya uchumi duniani imeboreshwa, imani ya watu wa nchi mbalimbali kuhusu uwezo wao wa kiuchumi imeinuka, mahitaji ya utalii katika nchi hizo yameongezeka hatua kwa hatua, miundo mbinu ya utalii unaovuka mipaka imeboreshwa, gharama za utalii umepungua, na njia ya kupata viza imekuwa rahisi zaidi. Kutokana na hali hiyo, idadi ya jumla ya watalii na mapato ya jumla ya utalii duniani umedumisha mwelekeo wa ongezeko kubwa, na utalii umekuwa motisha muhimu kwa ongezeko la uchumi duniani.

  Kuhusu sekta za utalii barani Afrika, Umoja wa Mataifa pia umetoa ripoti, ikieleza kuwa utalii umekuwa sehemu muhimu ya uchumi wa Afrika, na watalii wa ndani ndio motisha kuu ya maendeleo ya utalii. Mwaka 2016, mapato ya utalii barani humo yalikuwa dola za kimarekani bilioni 73, na yanakadiriwa kuongezeka na kuwa bilioni 121 hadi kufikia mwaka 2026. Shughuli za utalii zitaongeza nafasi za ajira milioni 11.7 kwa nchi za Afrika, haswa wanawake.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako