• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kampuni inawaajiri wanafunzi wa vyuo vikuu kufuga kondoo

  (GMT+08:00) 2018-02-11 20:36:56


  Hivi karibuni, kampuni moja ya kufuga kondoo kwa njia ya kisasa ya China imejulikana kutokana na kutoa mshahara wa Yuan laki 4.8, sawa na dola za kimarekani elfu 75 kwa mwaka, kuwaajiri wahitimu wa vyuo vikuu vya Tsinghua na Peking, ambavyo ni bora zaidi nchini China, kufanya kazi ya kufuga kondoo. Mshahara huo unawavutia sana wahitimu wa vyuo vikuu wa siku hizi wanaokabiliwa na shinikizo kubwa la kutafuta ajira.

  Kampuni hiyo ilikwenda kufanya matangazo katika chuo kikuu kimoja na wanafunzi 67 walijitokeza kwenye usaili. Ofisa wa utumishi wa kampuni hiyo aliuliza swali "mnajua kazi yetu?" Wanafunzi wote walijibu na kusema "kufuga kondoo" halafu wakacheka. … Ye Peng ni mmoja wa walioshiriki katika shughuli hiyo. Alisema aliwahi kuona ng'ombe na kuku shambani, lakini kondoo aliwaona kwenye televisheni tu. Anatafuta kazi ya kuwa mchambuzi wa bidhaa za kilimo, anasema "watu wengi wanaona kampuni ya kufuga kondoo kazi yake ni kulisha nguruwe tu, shughuli ambayo haifai kuwepo katika karne hii. Lakini shughuli kama hiyo itakuwepo daima, na kufuga kondoo kwa njia ya kisasa ni tofauti na ya zamani."

  Kwa ukweli, kuwaajiri wanafunzi wa vyuo vikuu kufuga kondoo si jambo geni. Kijana Lu Buxuan aliyehitimu chuo kikuu bora zaidi nchini China yaani Peking University alijulikana kutokana na kujituma katika shughuli ya kuchinja kondoo, na aliwahi kusema "alikipaka matope na kuharibu jina la chuo kikuu chake." Lakini miaka kadhaa baadaye, alijiunga na kampuni ya mwenzake aliyetangulia kuhitimu chuo kikuu hicho Chen Sheng na kusema kwa kujivunia kuwa "mimi ni mtaalamu bora zaidi wa nyama ya kondoo nchini China" naye Chen Sheng pia amesema kufuga nguruwe na kuuza nyama ya kondoo ni kazi yake ya maisha.

  Meneja utumishi wa kampuni hiyo alisema wanafunzi wa vyuo vikuu bora wana malengo makubwa, hawapendi kujiunga na kampuni kama hiyo. Kampuni hiyo inajua hilo, hivyo inapenda kutoa mshahara mkubwa kuwavutia. Wu Kang mwenye shahada ya pili alijiunga na kampuni hiyo mwaka jana. Sasa amezoea kuamka saa moja kila siku na kwenda shambani kulisha kondoo, na baada ya majira ya baridi kuingia, kutokana na kondoo kuumwa kirahisi, hivyo yeye na wafanyakazi wenzake wanaishi mashambani. Anasema wanafunzi wa vyuo vikuu wanapaswa kujua kwa usahihi mahali pao, baada ya kuingia katika jamii, wanapaswa kujichukulia kama ni mmoja katika jamii. Lakini pia alisema wanafunzi wenzake wengi wanafanya kazi zisizohusiana na kozi walizosomea, wanaume wanajikita kwenye sekta ya fedha, soko la nyumba na wanawake wanajishughulisha na sekta ya dawa au utumishi wa serikali, hakuna mtu anayependa kufuga kondoo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako