• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • FAIDA YA MKANDA MMOJA NJIA MOJA BARANI AFRICA

    (GMT+08:00) 2018-03-06 08:49:40

    Trix Ingado Luvindi

    Je mradi wa Ukanda Mmoja Njia Moja umepiga hatua zipi tangu kuzinduliwa kwake miaka mitano iliopita?

    Hii ni mojawapo ya maswali yaliyoyotolewa kwa naibu wa waziri wa maswala ya nje Bw. Zhang yesui mnamo tarehe nne mwezi machi katika jumba kuu la wachina alipokuwa akitoa taarifa kwa wanahabari. Bila shaka hili ni swali ambalo wengi wanao fahamu kuhusu mradi huu na nafasi ambayo Africa inachukua katika mpango huu wamepata kujiuliza mara nyingi.

    Bwana. Zhang Yesui aliweza kuweka wazi kuwa mradi huu , unaotarajiwa kugharimu mabilioni ya dila za marekani , umeweza kuchukua hatua kadha wa kadha ambazo labda hazijaangaziwa katika viombo za habari zikiwemo ushirikiani na nchi husika katika kuweka miundombinu itakayo zaa mazao ya mapema, mawasiliano kuhusu sera zitakazo fanikisha mradi huu na pia majadiliano kuhusu utaratibu utakao fwatwa ili kuwezesha mradi huu wa Belt and Road kunawiri.

    Licha ya hayo , ilibainika kwamba kuna changamoto za kawaida ambazo serikali ya Rais. Xi Jinping inajitahidi kukabiliana nayo kwanza kabla hatua nyingi zingine zichukuliwe.

    Kama mwana Afrika Mashariki na mzaliwa wan chi ya Kenya , haja yangu ni kuelewa ni faida zipi zitakazotokana na ushirikiano wa kiuchumi kwa nchi yangu ambayo kwa sasa inamahitaji mengi yatakayo tatuliwa na amaendeleo ya kiuchumi.

    Kwa sasa , nchi ya Kenya tayari inatarajia kufaidika kwa shilingi bilioni 142, jambo lakutia moyo haswa ukizingatia kwamba Rais Uhuru Kenyatta alisisitiza umuhimu wa kuwepo na faida za kiuchumi na heshima kwa pande zote mbili katika kongamano la Mkanda mmoja Njia Mmoja lililowakusanya viongozi wa dunia nchini China mwaka jana.

    Historia inaonyesha kwamba ,licha ya Afrika kuwa na raslimali chungu nzima, haija weza kujiendeleza vilivyo kwa sababu ya ushirikiano na nchi mbalimbali za nje zilizokosa kuzingatia faida kwa wote. Mradi huu, hivyo basi unanitia moyo kwa vile unaahidi maendeleo kwa nchi yangu ya Kenya.

    Hii ni dhana iliyotiliwa mkazo na Naibu wa Wizara ya Maswala ya nje Bw. Zhang katika taarifa yake aliposisitiza kwamba nchi ya Uchina inatamani sana kuleta maendeleo kwake na nchi zingine kwa njia ya amani bila uporaji.Pia alisisitiza kuwa wahusika wote wako sawa na hakuna nchi husika itakayo achwa nje.

    Katika hafla ya kung'oa nanga mkutano wa kitaifa wa kongamano la watu wa Uchina, Waziri Mkuu Li Keqiang alitoa ripoti kwamba serikali ya nchi hiyo ilikuwa imafuzu kwa njia tofauti katika ulingo wa diplomasia mojawapo ikiwa kongamano la Ukanda moja Njia moja Mei mwaka jana. Hii ni ishara kwamba China bado inaipa swala hili kipaumbele.

    La furahisha pia ni azimio la Uchina kuhakikisha uwazi , jambo linalobainika tayari kupitia miradi kama Standard Gauge Railway pamoja na mradi wa Lamu Port – South Sudan – Ethiopia –Transport Corridor , almaarufu LAPSSET inayotekelezwa nchini Kenya.

    Ila tu ni muhimu kwa nchi za bara Afrika kuweza kuchukua fursa hii kujifunza utaalamu kutoka kwa Uchina. Miradi hii inapotekelezwa, iwe ni wakati wa kujifunza kwa makini ili Afrika pia ipate kisomo kitakacho wezesha bara la Afrika kujieng'oa katika matatizo ya umaskini na ukosefu wa miundo mbingu.

    Hii itawezesha vizazi vijazo kutupilia mbali tabia ya kutarajia kupewa au kusaidiwa na kuiweka katika ulingo wa mabara na nchi ambazo zitaweza pia kutoa pendekezo za miradi ya kuleta maendeleo sio tu barani bali pia katika nchi zingine za nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako