• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • FAIDA YA RIPOTI YA SERIKALI YA UCHINA KWA BARA AFRIKA

  (GMT+08:00) 2018-03-06 20:14:17

  Hatimaye hafla ya kufungua mikutano ya miwili muhimu nchini China ilifanyika, na kama ilivyo desturi, wabunge wapatao elfu tatu kutoka mikoa mbalimbali walimiminika kwenye ukumbi mkuu wa watu wa China ili kuweza kuhudhuria na pia kusikiliza hotuba ya waziri mkuu Bw. Li. Keqiang.

  Hotuba iliyotolewa na waziriri mkuu chini ya mada Ripoti juu ya Kazi za Serikali iligusia maswala mengi yanayohusu nchi ya China ikiwemo kukuza uchumi, gharama ya matumizi ya mitandao, uhifadhi wa mazingira safi, ukuzaji wa sekta ya viwanda na teknolojia, uhusiano na nchi za nje, vita dhidi ya umaskini na ukosefu wa kazi na mbinu ambazo Chama cha Kikomunisti cha China CPC kitatumia katika kutekeleza malengo ya serikali katika miaka mitano ijayo.

  Kama mwanahabari nilikuwa makini kutaka kujua ripoti hii itagusia vipi hali zinazolikumba bara la Afrika na nchi ya Kenya .

  Bila shaka swala la mradi wa Ukanda Mmoja Njia Moja lilijitokeza, huku Waziri Mkuu Li akiangazia kwamba China kupitia mbinu za kidiplomasia, imeweza kujitahidi kufanya kongamano la kwanza la Ukanda Mmoja Njia Moja mwaka jana. Alisisitiza kwamba nchi hii imekata shauri kutia juhudi katika kuwa na uhusiano mwema na nchi za nje, zikiwemo za Afrika.

  Ripoti hiyo pia iliainisha mbinu zitakazotumiwa na serikali kukabiliana na umaskini na ukosefu wa ajira, ikiangazia lengo la kupunguza idadi ya watu wananaoishi katika umaskini kwa milioni kumi. Serikali hii pia inatarajia kupambana na janga hili kupitia ukuzaji wa viwanda, sekta ya elimu na huduma za afya .

  Umaskini ni janga ambalo bara la Afrika limepambana nalo kwa muda mrefu, kwa hivyo hii ni fursa ya kuweza kujifunza kutoka China jinsi ya kuondokana nalo kwa kupiga vita changamoto kama ufisadi na utovu wa nidhamu.

  Kando na hayo , Bw. Li Keqiang aligusia kazi ambayo China inafanya katika ulinzi wa amani kote duniani huku ikishirikiana na nchi za nje kwa mfano katika eneo Ghuba ya Edeni. China pia imeweza kushirikiana na Umoja wa Mataifa na kusaidia katika pambano dhidi ya ugaidi, kulinda haki za maji na pia kusaidia katika uokoaji wakati wa maafa.

  Katika sekta ya matibabu , waziri mkuu alisema kuwa serikali ina mipango ya kutilia mkazo matumizi ya sayansi na teknolojia katika utafiti kuhusu magonjwa katika maabara ya kisasa. Pia ameahidi kuwa serikali itahimiza vyuo vikuu na taasisi mbalimbali zilizo na uwezo wa kufanya utafiti utakaosaidia kumaliza maradhi yanayowasumbua raia. Hizi ni mbinu ambazo nchi mbalimbali za Afrika zinaweza kutumia kukabiliana na maradhi kama vile malaria na saratani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako