• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China inavyotekeleza Diplomasia ya Uchumi kwa vitendo

    (GMT+08:00) 2018-03-07 09:26:09

    na Majaliwa Christopher

    Bunge la Umma la China linaendelea na vikao vyake. Pamoja na mambo mengine yanayojadiliwa, suala la mahusiano yake na mataifa mengine duniani linapewa msisitizo na uzito unaosatahili.

    Hivi karibuni, Baraza la Mashauriano la Kisiasa la China, ikitoa ripoti ya kazi kwa kipindi kilichopita, limeweka bayana kuwa limefanyia tathmini mfumo wa mahusiano yake na mataifa mengine na kuangalia namna ya kuboresha mahusiano hayo ili yawe bora zaidi.

    Mwaka huu pekee, kwa mujibu wa taarifa ya serikali, taifa hili linategemea kutumia zaidi ya dola trilioni 3.3 ambayo ni sawa na yuan trilioni 21.

    Ukiangalia kwa jicho la haraka haraka, na ukiwa umebahatika kutembelea miji mikubwa nchini China, utajiuliza hawa watu wamekosa nini labda? Paimoja na kuwa na uchumi mkubwa namna hii bado wana shida gani?

    Kwa taarifa tu, China, kwa mujibu wa taarifa za Benki ya Dunia, ni la pili kwa uchumi mkubwa ulimwenguni huku mchango wake kwa uchumi wa dunia ukizidi asilimia 30.

    Mara kwa mara, China imekuwa ikisisitiza na kuweka bayana kwamba inaamini katika ushirikiano wenye faida kwa pande zote mbili, kwa kiingereza wanaitwa "win-win situation"kwa lugha rahisi sana, unaweza sema "nipe, nikupe".

    Kwa jicho la kitaaluma, naliona kama ni aina ya diplomasia ya kiuchumi. Baada ya uhusiano katika nyanja zingine zote za kijamii na kiutamaduni, sasa haya mahusiano yanatumiwa vizuri katika kuboresha biashara na uwekezaji.

    Kihistoria, nchi zilizoendelea zilianzisha mfumo mpya wa diplomasia ya uchumi ambao ni zaidi ya mfumo wa kuhusiana tu kijamii na kitamaduni.

    Kwa kupitia mfumo huu mpya, kampuni kutoka nchi hizi zinafanya biashara na mataifa mengine kwa kutumia fursa ya uhusiano wa kidiplomasia. Hiki hasa ndicho kinachotumiwa na China kwa sasa.

    China ina maendeleo makubwa sana katika nyanja ya sayansi na teknolojia, ina viwanda vinavyozalisha karibia kila aina ya bidhaa duniani. Ina watu wengi zaidi ya bilioni moja na wanaendelea kuongezeka.

    Viwanda vyote hivi ili vizalishe bila kusimama vinaitaji mali ghafi. Hakuna nchi iliyojitosheleza, lazima iagize mali ghafi kutoka nje ya mipaka yake.

    Baada ya uzalishaji, kwa kuwa uzalishaji ni mkubwa sana na kuzidi soko la ndani, lazima bidhaa zitafutiwe soko katika mataifa mengine.

    Haya yote ili yawezekane, si budi uhusiano wa China uwe umeimarika ili kuweza kushindana na mataifa mengine makubwa yenye misuli ya kiuchumi na maendeleo makubwa katika sekta ya viwanda.

    Mahusiano ya aina hii ndo huzalisha hii dhana inayoitwa diplomasia ya kiuchumi, ambayo ni aina mpya ya mahusiano, hailengi chochote zaidi ya kuimarisha biashara na uwekezaji.

    Nchi nyingi za Afrika, hasa katika miji mikubwa ya kibiashara Wachina wamejaa wakiendelea na biashara na uwekezaji. Baadhi yao wanaingiza bidhaa zilizokwisha tengenezwa na wengine wameanzisha viwanda vya kutengeneza bidhaa mbalimbali katika nchi husika.

    Lakini kwa upande mwingine, China imelegeza masharti kwa wafanyabiashara wanaoingia nchini humo kuchukua bidhaa kwenda kuuza katika nchi zao. Miji kama ya Guangzhou na Macau ni maeneo ambayo wafanyabiashara hasa kutoka barani Afrika wanakimbilia kuchukua "mzigo".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako