• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ripoti ya serikali China, muelekeo imara wa kujiimarisha

  (GMT+08:00) 2018-03-07 10:32:39

  Na Theopista Nsanzugwanko, Dar es Salaam, Tanzania

  NCHI ya China inayoongozwa na chama cha kikomunisti cha CPC kinachoongozwa na Rais wake Xi Jinping inaelezwa kuwa taifa la pili duniani kwa kuwa na uchumi mkubwa, wiki hii imekuwa na mkutano wa kwanza wa bunge la 13 la umma la China.

  Katika mkutano huo, serikali hiyo imetoa ripoti ya utendaji kazi, pamoja na mafanikio ya miaka mitano iliyopita inayoashiria kwa kiasi kikubwa nia ya serikali ya chama hicho kuboresha maisha ya wananchi wake,kwenda sambamba na nchi ya uchumi wa kati.

  Waziri mkuu wa China, Li Keqiang akitoa ripoti hiyo ametoa mapendekezo kwa ajili ya utendaji wa serikali kwa mwaka huu yanayoonesha dhamira ya kweli katika kuhakikisha nchi hiyo yenye uchumi mkubwa kuendelea kujiimarisha.

  Ametoa ripoti ya utendaji wa serikali katika miaka mitano iliyopita, huku akitoa mapendekezo kwa ajili ya utendaji wa serikali kwa mwaka huu,kwa pato la ndani kukua kwa asilimia 6.5, kiwango cha bei ya bidhaa kitapanda kwa asilimia tatu ,huku nafasi mpya za ajira zikiongezeka kwa zaidi ya milioni 11.

  Katika mwaka huu wa 2018, serikali ya China pia imedhamiria katika maeneo ya mijini watu wenye ukosefu wa ajira kuwa kwa asilimia 5.5, huku wakitilia mkazo kukua kwa pato la mtu mmoja mmoja na uchumi kwa ujumla.katika kuonesha dhamira ya kweli ya maendeleo kwa nchi hiyo pamoja na nchi nyingine husan za afrika, China kupitia mradi wa Ukanda Mmoja na Njia Moja unaotarajiwa kuzinufaisha baadhi ya nchi za Kiafrika.

  Baraza la Mashauriano la Kisiasa la China,limeeleza kuwa mradi huo wa mabilioni ya dola za Kimarekani unatarajiwa kufaidisha nchi za Tanzania, Kenya pamoja na nchi zingine za Afrika Mashariki.

  Nchi zingine za Afrika zitakazonufaika na mradi huo ni Ethiopia, Djibouti na Misri, huku ikiwa tayari imefanya uwekezaji wa dola za Kimarekani takribani bilioni 60.

  Mwenyekiti wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la awamu ya 12, Yu Zhengsheng, alisema wameupa uzito unaostahili mradi huo kuhakikisha unakuwa na faida kwa pande zote zinazohusika na wanatarajia miaka ijayo kuongeza uwekezaji kufikia kati ya bilioni 600 na 800.

  Katika mipango hiyo itaenda sambamba na mafanikio ya utendaji wa serikali kwa miaka mitano iliyopita kwa kuwezesha pato la ndani la nchi hiyo kufikia Yuan trilioni 82.7 kutoka yuan trilioni 54 hivyo kuwepo kwa ongezeko la asilimia 7.1 kwa mwaka.

  Ongezeko hilo limefanya mchango wa China kwa uchumi wa dunia uwe zaidi ya asilimia 30, katika kipindi hicho huku mtandao wa reli ya mwendo kasi, biashara ya mtandaoni, malipo kwa kutumia simu za mkononi nchi hiyo kuongoza duniani.

  Kutokana na hali hiyo idadi ya watu maskini nchini China imepungua kwa zaidi ya watu milioni 68, huku waziri mkuu anaeleza kuwa ukuaji wa pato la ndani imebakia sawa na mwaka uliopita lakini matokeo yake yatakuwa na athari kubwa.

  Uchumi wa China katika ukuaji wake kwa mwaka unakuwa kwa lengo la kufikia asilimia 6.9 ikiwa ni ukuaji mkubwa wa kwanza ndani ya miaka saba, lengo la GDP kwa mwaka itafikiwa mapema.

  Shirika la fedha duniani (IFM) mwezi Januari mwaka huu walieleza GDP ya nchi hiyo kukua kutoka asilimia 6.5 mpaka 6.6 jambo linalofanya China kuendelea kuweka mikakati ya kuimarisha uchumi duniani kwa kufungua milango ya ushirikiano na kufungua masoko.

  Anaeleza kutilia mkazo wa upatikanaji sekta za mawasiliano, huduma za tiba, elimu, uangalizi wa wazee na magari yanayotumia nishati mbadala nayo wamekuwa wakiwekeza kwa wageni.

  China imepania kuwainua wananchi wa kundi la wenye uchumi wa kati ,ambao idadi yao inakadiliwa kuwa milioni 400, wameonesha nia ya kuingiza bidhaa mbalimbali nchini humo.

  Katika kuhamasisha uingizwaji wa bidhaa nchini humo, China imeandaa maonesho ya kimataifa ya bidhaa zinazoingizwa nchini humo mwaka huu .

  Katika miaka mitano,pato la ndani limekuwa kutoka Yuan trillion 54 mpaka Yuani trillion 82.7. huku wakitengeneza ajira mpya milioni 66 na watu 68,000 wakiondolewa katika umasikini.

  Keqiang anasema katika kipindi hicho, changamoto ya hali ya hewa katika miji mikubwa imepungua kwa asilimia 50, huku China ikiendelea kuongoza duniani kwa reli za mwendo kasi, biashara mtandaoni,malipo ya huduma mbalimbali bila kuwa na fedha taslimu pamoja na uchumi shirikishi.

  Alisema licha ya mafanikio hayo kuna changamoto za kutoridhishwa na huduma za elimu, makazi na huduma za dawa na nyinginezo, amabzo wamedhamilia kufanyiakazi.

  Uwekezaji mwaka huu imefikia uwekezwa wa Yuan bilioni 732 katika ujenzi wa reli na zaidi ya Yuan trilioni 1.8 katika usafiri wa anga na majini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako