• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Bunge la China lakutana kujadili utendaji wa serikali, mageuzi ya katiba

  (GMT+08:00) 2018-03-08 08:56:13
  Mikutano miwili mikubwa ya mwaka, yaani Baraza la mashauriano ya Kisiasa, na bunge la umma la China, inafanyika. Hii ni mikutano ya uwakilishi wa wananchi, ambayo wajumbe wake wanawakilisha maoni ya wananchi kwa chama na serikali.

  Bunge la umma, ni mfumo wa kawaida kama wetu Tanzania, isipokuwa bunge la China ni la chama kimoja.

  Baraza la mashauriano ya kisiasa, ni utaratibu maalumu wa kisiasa wa China unaotoa jukwaa kwa watu wote wasio na vyama kukutana na chama tawala na serikali ili kutoa maoni kuhusu mambo ya taaluma zao, iwe ni biashara, elimu, sayansi hata michezo.

  Kwa mwaka huu kinachofuatiliwa zaidi ni mkutano wa bunge la umma la China. Bunge hilo ambalo kwa kawaida hukutana kwa siku saba, safari hii linakutana kwa wiki mbili kujadili ajenda mbili kuu. Moja ikiwa ni kusikiliza ripoti ya utendaji wa serikali na mpango kazi wa serikali kwa mwaka unaokuja, na nyingine ni mageuzi ya katiba ya nchi hiyo.

  Ripoti ya utendaji wa serikali inafuatiliwa zaidi kwa kuwa imeeleza kwa kina mambo yaliyofanywa na serikali katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. Ikumbukwe kuwa tangu mwaka 2013, chama cha Kikomunisti cha China na serikali yake chini ya uongozi wa Rais Xi Jinping kiliamua kukabiliana na changamoto zote zinazowakabili wananchi.

  Licha ya China kupiga hatua kubwa kiuchumi, bado kuna idadi kubwa ya watu masikini, ufisadi, uchafuzi wa hali ya hewa na hata ukosefu wa ajira. Kutatua changamoto hizo, Rais Xi alileta wazo la "Zama mpya" kwenye nadharia ya "Ujamaa wenye umaalum wa China" na kufanya kazi kubwa kuondoa matatizo yanayowakabili wananchi.

  Ripoti ya utendaji wa serikali imewasilishwa na Waziri Mkuu wa China, Li Keqiang kwenye ufunguzi wa bunge ambapo inaonyesha kuwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita uchumi wa China ulikua kwa wastani wa asilimia 7.1 ambapo watu milioni 68 waliondolewa kutoka kwenye lindi la umasikini na nafasi milioni 66 za ajira zilitengenezwa huku mapato ya wananchi yaliongezeka kwa asilimia 7.4.

  Mafanikio haya yamepatikana wakati hali ya uchumi wa dunia ikiwa haijatengemaa kutokana na athari za msukosuko wa uchumi wa dunia uliotokea mwaka 2008. Wananchi wa China waliokuwa na malalamiko kuwa maendeleo ya uchumi bado hayajawanufaisha vya kutosha, sasa wananufaika na uongozi wa XI ambaye ametatua changamoto mbalimbali za kijamii na kiuchumi.

  Wananchi wanaamini kuwa manufaa hayo hayajapatikana kirahisi, yanatokana na juhudi za makusudi na yanahusishwa moja kwa moja na juhudi za Rais Xi Jinping katika kutekeleza kwa kasi sera za kuboresha maisha ya watu.

  Ajenda kubwa ya pili kwenye mkutano huo inalenga mabadiliko ya katiba. Mabadiliko haya yanataka kuwekwa msingi wa kisheria wa kuwepo kwa mwendelezo wa sera na utekelezaji wake, kuhakikisha kuwa maendeleo yaliyopatikana yanadumu, na kuendelea kuwanufaisha wananchi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako