Na Majaliwa Christopher
China imetangaza rasmi. Imesisitiza. Imeeleza tena.
Mahusiano yake na nchi za Afrika, bado yapo sana. Ije mvua, ije jua. Yaje mabadiliko ya aina gani, hakuna kitakachobadili. Ahadi zake kwa Afrika ziko palepale.
Msimamo huu umewekwa na kusisitizwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Bw. Wang Yi akizungumza na waandishi wa habari Alhamis, pembezoni mwa vikao vya Bunge la Umma vinavyoendelea jijini Beijing.
Ni maneno yanayotia matumaini hasa kwa bara hili la Afrika ambalo linapambana kila kukicha kuondokana na umasikini, maradhi, ujinga, njaa na zaid ya yoyote misuguano ya kisiasa yanayoendelea kudidimiza maendeleo na juhudi za kujikwamua kimaendeleo.
Hili ni jambo jema sana. Na kwa maana nyingine ni kwamba, China linahitaji bara la Afrika kama ambavyo Afrika pia inahitaji china.
China, nchi kubwa zaidi duniani yenye idadi kubwa ya watu, pia imeahid kusaidia nchi za Afrika katika kupammbana na ugaidi, uharamia, majanga ya asili na mambo mbalimbali yanayotishia amani na usalama barani humo.
Nchi mbalimbali duniani kwa sasa, suala la usalama limekuwa tete, hali ambayo ni hatari sana katika ukuaji wa uchumi na mustakabali mzima wa ustawi wa jamii.
Uharamia na majanga ya kiasili kama vile mafuriko na matetemeko ya ardhi kwa upande mwingine pia vimeshika kasi, na hatua ya China, taifa la pili duniani kwa uchumi, kuliona hili ni jambo la kuungwa mkono.
Afrika, ikiwa ni sehemu muhimu kabisa katika harakati za kufanya dunia kuwa pahala pema pakuishi, Waziri Wang anasema halina budi kutupiwa macho kwa ukaribu zaidi.
China bado linaaamini katika mahusiano na mashrikiano yenye kuwa na faida kwa pande zote, ikiwa ni njia pekee bora ya kufikia malengo ya pamoja ya kupiga hatua ya kimaendeleo.
"Mambo yanayohusu Afrika yanahusu China. Vipaumbele vya Afrika ni vipaumbele vya China," anasema Bw. Wang.
Hapa tunaona ni namna gani China iko tayari na imejitolea katika kuhakikisha mahusiano yake na chi za Afrika yanakuwa ya kiundugu, yakijengwa katika misingi ya kujaliana.
Lakini pamoja na kuahidi kuasaidia bara la Afrika katika nyanja hizi za kiusalama, kiuchumi na kijamii, Waziri Wang anatoa changamoto kwa kwa nchi za Afrika, akizikaribisha kuungana nae katika 'safari ya treni ya haraka ya maendeleo.'
Kwamba pamoja na ahadi zote hizi, lakini kwa namna moja ama nyingine nchi za Kiafrika pia hazina budi kujituma kuhakikisha mipango yao yote ya kiuchumi inatekelezwa kwa kasi na kwa viwango vitakavyo leta matokeo chanya kwa kasi.
Waziri Wang anauona mkutano uliopangwa kufanyika mwezi septemba ujulikaonao kama 'FOCAC' kati ya viongozi wa China na viongozi wa nchi za Afrika kama sehemu sahihi ya kuendelea kuimarisha na kuboresha mahusiano kati ya pande hizi mbili.
Katika mkutano huu, pamoja na mambo mengine yatakayojadiliwa, viongozi hawa watapata fursa pia ya kuangalia namna bora na nzuri zaidi ya kufanya mahusiano haya yaweze kuwa endelevu na yenye faida kubwa.
Suala la Ukanda Mmoja na Njia moja, kwa mujibu wa Waziri Wang utapewa kipaumbele kwa kuwa ni moja katika ya miradi ambayo inalenga kuwa na manufaa zaidi kwa nchi zote husika.
Kwa mara nyingine, China imeweka sawa wasiwasi unaoenea kuwa inawezekana huu mradi wa Ukanda Mmoja na Njia Moja utekelezaji wake usiwe wa wazi na hivyo baadi ya nchi zisinufaike nao kama inavostahili.
Anasema kila kitu katika mradi huu utafuata mfumo wa uwazi unaonekana kwa kila mtu, na zaidi ya yote, kila nchi itakayopitiwa na mradi wenyewe utaweza kunufaika vile inavyostahili.
Mbali na nchi za Afrika, China inasisitiza kuwa iko tayari kama ilivyokuwa siku zote kuendelea kufanya biashara na kuimarisha uhusiano ya kidiplomasia na nchi zote ikiweko Marekani na India.
Mwisho—
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |