• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mipango 10 ya ushirikiano kati ya China na Afrika yawanufaisha waafrika kihalisi

  (GMT+08:00) 2018-03-12 08:29:30
  na Trixy Ingado

  Kama ilivyo desturi ya wakati wa kisiasa wa mikutano miwili nchini China, mawaziri wa wizara tofauti wamekuwa wakijitokeza kutoa taarifa kuhusu sekta na wizara husika na njia serikali ya China itatumia kuimarisha uchumi na hali za wananchi wa Uchina.

  Jumapili wiki hii, ilikuwa zamu ya waziri wa fedha Bw. Zhong Shan kutoa taarifa kwa wanahabari na ni katika taarifa hii ambapo alisisitiza kwamba nchi ya Uchina haina mipango wala haja yoyote ya kujihusisha na vita vya kibiashara.

  Kadiri ya hayo Bw. Zhong alisisitiza kwamba nchi hii itatumia mbinu zitakazotakikana kujitetea iwapo Marekani itaanzisha vita vya aina hiyo. Aidha waziri huyo pia aliangazia mipango kadha wa kadha zitakazotumika katika kuimarisha biashara humu nchini na pia na nchi za nje.

  Wizara hiyo pia iliweza kukuza biashara na nchi za nje na kuleta zaidi ya biashara elfu themanini na tano nchini mwaka jana. Waziri aliweka wazi kuwa haya yalitekelezwa licha ya upishano mkali sana katika soko la kimataifa.

  Naibu waziri wa biashara wa China Bw. Qiang Keming aliwaambia wanahabari kwamba mipango kumi ya ushirikiano na bara Afrika ilitangazwa na rais Xi Jinping ilianza kutekelezwa ambapo zaidi ya miradi mia mbili ya kuwanufaisha waafika iling'oa nanga.

  Mwakani 2017, mradi wa reli kati Djibuti na Addis Ababa ulitumiwa kupeleka chakula cha msaada kwa waliokumbwa na njaa. Pia waziri Qiang alisema China imeweza kutekeleza miradi ya reli, mabandari na viwanja vya ndege kote Afrika, miradi ambayo alisema nchi ya China itaendelea kutekeleza kwa ushirikiano na nchi tofauti za afrika.

  Kando na hayo waziri Qian pia alisisitiza kwamba nchi ya China itatilia mkazo miradi itakayosaidia kukuza uwezo wa bara Afrika kujisimamia kwa kusaidia kupunguza umasikini, kuleta ajira kwa watu wa afrika na pia kwa mafunzo mbalimbali. Pia alisema kwamba China itafanya kazi pamoja na mashirika ya kupunguza umasikini kutekeleza haya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako