• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Balozi Kairuki: Kuchaguliwa kwa Rais Xi neema Afrika

  (GMT+08:00) 2018-03-18 16:02:46

  na Majaliwa Christopher

  Balozi wa Tanzania nchini China Bw. Mbelwa Kairuki amemuelezea Rais Xi Jinping kama kiongozi imara ambaye anaamini ataendelea kusimamia mipango mbalimbali ya maendeleo aliyoanzisha kati ya China na nchi za Afrika.

  Akizungumza katika mahojiano na mwandishi wetu, Balozi Kairuki amesema Tanzania na Afrika kwa ujumla zinaunga mkono kuchaguliwa tena kwa Rais Xi, amabaye katika kipindi cha miaka mitano iliyopita amedhihirisha kwa vitendo kusimamia kidiplomasia ya kiuchumi yenye usawa na faida kwa pande zote.

  Balozi Kairuki amesema kuchaguliwa kwa mara nyingine kwa Bw. Xi kunafufua matumaini mapya ya kuimarika kwa ushirikiano katika ya China na Afrika kwa ujumla.

  "Sisi Tanzania na Afrika kwa ujumla tunampongeza Rais Xi kuchaguliwa tena kuongoza taifa la China. Tuna imani kubwa kwamba yale mazuri yote aliyoyaanzisha katika kipindi cha miaka mitano iliyopita yataendelea kutekelezwa kwa ufanisi mkubwa." amesema Balozi Kairuki.

  Ametaja maeneo ambayo anaamini yatazidi kupewa kipaumbele kuwa ni mradi wa Ukanda Mmoja na Njia Moja ambao ulianzishwa na Rais Xi mwenyewe.

  Ukanda Mmoja na Njiia Moja, ni mradi kabambe wa mabilioni ya dola unaolenga kuunganisha bara za Afrika, Asia na Ulaya katika sekta zote, kikubwa ikiwa ni katika miundombinu ya reli na barabara. Rais Xi alibuni huu mradi mwaka 2013 kutokana kuwepo kwa changamoto ya kuunganishwa kwa bara moja na nyingine na kusababisha ugumu katika shuguli za biashara na uwekezaji.

  Balozi Kairuki anaamini kuchaguliwa tena kwa Bw. Xi ni neema kwa nchi zinazohusika katika mradi huu kwa sababu ataendelea kusimamia kwa karibu zaidi utekelezaji wake.

  Ameongeza pia kwamba Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) ni sehemu nyigine ambayo viongozi wa Afrika wanaamini utazidi kustawi kutokana na kuchaguliwa tena kwa Bw. Xi.

  Itakumbukwa kuwa Rais Xi akiwa jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini mwaka 2015 katika Baraza la FOCAC, aliahidi kuwa serikali yake itatoa takribani dola za kimarekani bilioni 60 ambayo yataelekezwa katika maeneo mbalimbali ambayo ni chachu katika ukuaji wa uchumi na ustawi wa jamii barani Afrika.

  Balozi Kairuki amesema kuchaguliwa tena kwa Bw. Xi kunampa pia muda wa kufanya maandilizi ya kutosha juu ya mkutano mkubwa wa FOCAC utakaowaleta pamoja viongozi wa Afrika na China hapo mwezi Septemba.

  Kikubwa zaidi katika mkutano huo ni kuendelea kuangazia namna bora ya kuimarisha ushirikiano kati ya China na Afrika na kujadili njia sahihi za kushughulikia changamoto mbalimbali zinazokabili nchi za bara la Afrika.

  Aidha, amezungumzia kuhusu mfumo mpya wa ushirikiano wa China unaogemea katika diplomasia ya kiuchumi wenye kuamini katika usawa na faida kwa wote.

  Amesema sera ya Bw. Xi juu ya diplomasia ya kiuchumi inawiana na ile ya Rais wa Tanzania, Dkt John Magufuli ambae serikali yake ipo katika mageuzi ya uchumi wa viwanda huku akiamini katika ushirikiano wenye usawa na faida kwa pande zote.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako