• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Majadiliano njia pekee ya suluhu mgogoro China na Marekani

  (GMT+08:00) 2018-04-13 08:30:44

  Na Theopista Nsanzugwanko

  MGOGORO wa kibiashara baina ya nchi za uchumi mkubwa Duniani China na Marekani ulioibuka hivi karibuni ni dhahiri umekuwa mjadala Duniani kutokana na umuhimu wake kwa uchumi wa dunia.Ni dhahiri kuwa athari zake hazitakuwa kwa mataifa hayo tu, bali utasababisha uchumi wan chi nyingi duniani kuathirika hivyo ni vema kuwepo kwa nia za majadiliano ili kuondoa mgogoro huo.

  Marekani ambayo ni nchi inayoongoza kwa uchumi duniani, ilipaswa kutafuta njia mbalimbali za kuhakikisha wanashirikiana na China ambayo ni nchi ya pili kwa uchumi kuweka uwiano wa kibiashara kwa ajili ya biashara ya dunia.

  Hakuna ubishi kuwa, nchi hizo kubwa duniani licha ya kushirikiana na nchi nyingine bado zinategemeana kuhakikisha kila moja inaendelea kukuza nzi yake kwa kusafirisha nje ya nchi yake na kupeleka katika nchi nyingine.

  China nchi inayochangia uchumi wa dunia kwa asilimia 30 imekuwa ikikuza uchumi wake kwa kasi,imemua kufikia maamuzi ya kuwekea Marekani vikwazo katika biashara yake kutokana na tishio la Marekani kufanya hivyo kwa bidhaa za China.

  Ikiwa hakutakuwa na ufumbuzi wa haraka athari za kiuchumi zinaweza kuikumba dunia siku za usoni ikiwa hakutakuwa na majadiliano yenye tija ya kibiashara kati ya China na Marekani.

  Aidha, jumuiya za kimataifa ni vema kuingilia kati na kuyashawishi mataifa hayo mawili kukaa mezani kwa nia njema kabisa ya kutafuta ufumbuzi ili kutatua changamoto hii ambayo mwisho wa siku haitakuwa na mshindi

  China imeijibu Marekani kwa kuziongezea ushuru bidhaa zake kwa thamani ya dola bilioni 50, ikitoa orodha ya bidhaa zinazoagizwa kutoka Marekani zikiwemo maharage ya soya, ndege, magari, mvinyo na bidhaa za kemikali.

  Wizara ya biashara pamoja na wizara ya fedha ya China zimesema orodha ya China ya nyongeza ya asilimia 25 ya ushuru kwa bidhaa za Marekani inajumuisha bidhaa 106 zenye thamani ya kibiashara ya dola bilioni 50. Tarehe ya kuanza kutekelezwa agizo hilo itategemea ni lini Marekani itakapoanza kutekeleza mpango wake.

  China wamefikia maamuzi hayo baada ya Marekani kuchapisha orodha ya bidhaa za China za thamani ya dola bilioni 50 ambazo huenda zikatozwa ushuru.

  Orodha hiyo ya Marekani inayojumuisha bidhaa 1,300 itadurusiwa upya katika kipindi cha siku 60 kuanzia siku ya tangazo hilo kabla uamuzi wa mwisho kupitishwa, kuamua ni bidhaa zipi zitakazotozwa ushuru zaidi wa asilimia 25.

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje wa China, Lu Kang, ameyaeleza mapendekezo hayo ya Marekani kuwa hayana msingi na ni utaratibu wa kuyalinda masoko ya ndani.

  Wakati Lu Kang amesema China itaishitaki Marekani kwa Shirika la

  Biashara Duniani (WTO), shirika hilo limesema mgogoro huo utaathiri uchumi wa dunia.

  Tofauti na orodha ya Marekani iliyoujumuisha bidhaa za viwanda, orodha ya China imezilenga bidhaa muhimu za Marekani zinazouzwa katika nchi za nje.

  Wizara ya mambo ya nje ya China imesema iko tayari kufanya majadiliano kuhusu mzozo huo lakini pia siyo kwamba inaogopa vita hivyo vya kibiashara, hivyo ni vema busara zaidi kutumika kwa wachumi wa nchi hizo mbili.

  Ni dhahiri kuwa, athari hizo zinazoelezwa kuwa za kidunia lakini pia zitawagusa zaidi wananchi wan chi hizo ambao wanafanya biashara baina ya nchi hizo jambo ambalo linatakiwa kuchukuliwa maamuzi kwa manufaa ya wananchi husika.

  Mkurugenzi wa idara wa kilimo ya jimbo hilo Alexis Taylor amesema hatua hiyo itakuwa na madhara kwa jimbo la Oregon lililopo Pwani ya Magharibi ya Marekani .

  Ikiwa China itaendelea kutekeleza uamuzi wa kutoza ushuru wa asilimia 25 kwa bidhaa za kilimo zinazotoka katika jimbo hilo,kwani ni mwagizaji mkubwa wa nne wa bidhaa za kilimo kutoka Oregon.

  Alisema mwaka jana peke yake iliuza bidhaa hizo kwa China zenye thamani ya dola za kimarekani milioni 320.

  Hivyo ukweli unabaki kuwa ni vema wachumi, viongozi, wadau mbalimbali wan chi hizo kwa kushirikiana na mashirika ya kimataifa bila kuangalia nchi Fulani waweke majadiliano yatakayotoka na ufumbuzi wa pamoja na kumaliza migogoro hiyo.

  Ikumbukwe kuwa, mwaka jana Viongozi wa nchi hizo mbili Rais wa Marekani Donald Trump na Rais wa China Xi Jinping walipokutana mjini Beijing,China walikubaliana kushirikiana na kuhakikisha wanamaliza tofauti zilizopo katika masuala ya kibiashara.

  Katika ziara hiyo, Waziri wa biashara, William Ross alisema mpango huo ni ishara kamili kuwa ushirikiano wa kiuchumi kati ya mataifa hayo muhimu kiuchumi duniani unazidi kuimarika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako