• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanafunzi wa shule ya msingi wanatoka shuleni saa tisa na nusu

    (GMT+08:00) 2018-04-16 09:09:52


     

    Ili kupunguza shinikizo la masomo linalowakabili wanafunzi wa shule ya msingi nje ya darasa, na kutatua tatizo la baadhi ya shule kutoza ovyo masomo ya ziada, shule za msingi na sekondari za China zinatekeleza sera ya "kutoka shuleni saa 9:30 mchana". Hata hivyo, sera hiyo yenye nia nzuri imeleta usumbufu mwingi kwa wazazi wanaofanya kazi.

    Bw. Wang ana watoto wawili ambao wote wanasoma katika shule ya msingi. Yeye na mkewe ni wafanyakazi. Kazi ya kuwapeleka na kuwachukua watoto kutoka shuleni imekuwa ni kazi ya bibi. Bw. Wang anaona kutoka shuleni saa 9:30 ni mapema kidogo, kutokana na kazi hawapati muda wa kwenda kuwapokea, na pia hawana muda wa kuangalia watoto wakifanya kazi za nyumbani. Bibi amezeeka, limekuwa ni jambo zuri kwamba anaweza kwenda kuwachukua watoto, lakini hawezi kuwafundisha kimasomo. Kwa hivyo anawapeleka watoto kwenye madarasa tuition. Madarasa kama hayo yanaweza kuongeza muda wa kusoma kwa watoto, lakini gharama zake si ndogo.

    Mwezi Februari mwaka jana, Wizara ya Elimu ya China imetoa mwongozo kuhusu kufanya kazi nzuri baada ya wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari kutoka shuleni, na kutaka shule hizo zibebe wajibu wa kuwahudumia wanafunzi hao baada ya masomo ya siku. Sehemu mbalimbali nchini China zimechukua hatua kuhusiana na mwongozo huo. Kwa mfano, mji wa Tianjin ulitoa agizo kuwa kuanzia mwaka huu, shule za msingi na sekondari zinafanya kazi za huduma baada ya wanafunzi kutoka shuleni, mpaka saa moja kila siku. Mkoa wa Zhejiang pia umetoa huduma kama hizo na malipo husika yatatolewa na serikali, na wazazi hawahitaji kulipa.

    Lakini mwalimu Zhang ana maoni kuhusu jinsi ya kupanga muda baada ya wanafunzi kutoka shuleni saa 9:30 kila siku,.

    Anasema wakati huu wa kutoka shuleni unafaa kwa wanafunzi wanasoma katika madarasa ya juu, kwani wengi wao wanabaki kwa hiari shuleni na kufanya homework, na kuendeleza tabia ya kujisomea wenyewe. Lakini wanafunzi wa madarasa ya chini hawana uwezo wa kujisimamia, kama mwalimu hayupo wanaweza kuzungumza zungumza na kucheza darasani. Ndiyo maana kwa wanafunzi hao, kutoka saa 9:30shuleni kunapunguza muda wao wa kusoma, na ni lazima kuwe na watu wa kuwasimamia wakisoma.

    Malezi ya watoto kwenye jamii ya China ni jambo gumu sana, hasa kama wazazi wote wawili wanafanya kazi

    Kukinzana kwenye malezi ya watoto, kuna wanaoona kuwa sio vizuri kuwapa kazi nyingi watoto, wanahitaji kuwa na muda wa kupumzika na kucheza, na wengine hawa jamaa ni tatizo wanatakiwa kukaa shuleni.

    Sio kila mara kuwa wanafunzi wanaokwenda kwenye mafunzo ya tuition ndio wanafanya vizuri, na badala yake inakuwa ni kupoteza pesa za wazazi, kwa hiyo huu uamuzi wa serikali ni sahihi.

    Hii njia inaweza kuwa na manufaa kwa wazazi wa wanafunzi wa familia zisizo na uwezo mkubwa kifedha, kwa sababu kulipia gharama za tuition hapa china si rahisi.

    Lakini tukisikiliza maoni ya mmoja wa walimu amesema ni jambo zuri kwa watoto kusimamiwa maana, ukiwaacha peke yao hawawezi kujisomea, nadhani mwalimu anajua vizuri watoto hao kuliko serikali

    Tukiangalia uamuzi huo inaonekana kama umelenga maslahi ya mtoto tu, lakini haungalii changamoto za wazazi kwenda kuwachukua watoto shuleni, au bibi na babu ambao hawawezi kuwafundisha nyumbani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako