• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UTAMU WA SANYA

    (GMT+08:00) 2018-04-16 09:29:43

    Na Trix Ingado, Sanya, China

    Mji wa Sanya ni moja wapo za vivutio vikuu vya watalii mkoani Hainan. Ni mji wa pwani ambao mbali na kuwa na vivutio vingi vya kimazingira, maeneo mengi ya Sanya yameendelezwa na serikali kuwawezesha wageni kutalii na kustarehe bila ugumu wowote.

    Wenyeji wa eneo hili ni wa asili za Li na Miao. Kabila zote mbili zilizo na tamaduni nzuri na za kufana sana zinazovutia mamilioni ya wageni wa tabaziahka mbalimbali kila mwaka.

    Mila na tamaduni za wenyeji wa hapa zimehifadhiwa katika bustani mbalimbli ambako wenyeji wameajiriwa kuonyesha fani mbalimbali za jadi kama vile ushonaji wa nguo za kiasili, vyakula vya kiasili, densi na uimbaji na michezo ya kuigiza

    Pia wageni wanapotembelea bustani hizi zinazotumika kuhifadhi tamaduni za kabila, wanaweza kuonja sharubati na matunda yanayouzwa na wenyeji wa Sanya. Pia unaweza kununua pipi zilizotengenezwa kwa nazi, na kama unahamu ya pipi za kisasa, pia utapata.

    Wakati huo huo, hii ni fursa ya kujionea jinsi wanawake wakongwe wanatumia mbinu za zamani kutengeneza mavazi ya kiasili kwa kutumia mitambo spesheli iliyoyo tumika ma wahenga wao. Mbinu hii spesheli inahitaji ujuzi wa ajabu kwani kina mama hawa huchukua mda mrefu kushona nyuzi za rangi tofauti ilikutengeneza mavazi mazuri.

    Maonyesho haya pia yanafunza jinsi wajadi walitengenezarangi na kutumia rangi hizi kubadilisha muonekano wa mavazi. Bonde la Binglanggu kwa mfano lina vijiji vya Ganza, Guyin Miao, Tianye, Li na Kijiji cha utamaduni vyote mbavyo vinamaonyesho ya kufana ambayo yanawawezesha wenyeji kupata riziki huko wakiwafunza watalii kuhusu mila ya kupendeza.

    Tamaduni za upandaji miti zinaonyashwa katika bonde hili pamoja na pombe. Kwa wanaopenda mandhari mazuri kuna misitu iliyohifadhiwa na viongozi wa eneo hili kwa mfano misitu ya Yanoda na kisiwa cha Nanwa.

    Yanoda ni msitu wa pekee Uchina na ina miti iliyona miaka zaidi ya mia moja. Msitu huu pia una mito mizuri na chemichemi ya maji ya kupendeza. Ni eneo ambalo watalii pia wanafurahia kwa sababu ya hali nzuri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako