• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yatimiza miaka arobaini tangu kufunguka kwake

  (GMT+08:00) 2018-05-02 09:01:47

  Na Trix Ingado

  Mwakani 1978, aliyekuwa kiongozi wa China Deng Xiaoping, aliiongoza taifa katika mwamko mpya wa kisiasa uliyohusu kufunguka na kufanya mabadiliko yaliyotarajiwa kugeuza hatima ya nchi. Katika enzi zile rais huyo alisisitizia wachina kuwa tumaini la nchi limo katika maendeleo na maendeleo pekee japo kuwa kuendelea sio jambo rahisi.

  Mwaka huu China inaadhimisha miaka arobaini tangu mabadiliko haya ya kisiasa ambayo yamegeuza jinsi ambayo China inatekeleza shughuli zake sio tu humu nchini bali nje pia. Ikumbukwe kuwa mabadiliko haya kimsingi yalifanywa kugeuza hali ya Maisha ya wananchi wa kawaida Uchina.

  Sera za kufunguka na mageuzi zimechangia pakubwa katika ukuzaji wa miji mikubwa ambayo wachina wengi walihamia kutoka mashambani. Idadi kubwa ya raia waliohamia vijiji vikubwa imechangia pakubwa katika kukuza uchumi wa nchi ya China. Kila mwananchi akiwa na ujuzi wake na masomo ya viwango tofauti anajihusisha katika kutafuta riziki katika miji mikubwa na wanavyo endelea kujiendeleza maishani pia uchumi wa miji hii inakuwa. Hii ndio hali ilivyo kuwa kwa miaka arobaini iliyopita , hali ambayo imechangia katika kukuza kuchumi wa China kwa ujumla.

  Huku uchumi wa China ukiimarika sera ya kufunguka na mageuzi ilisababisha raia wengi kujiepusha na makali ya umaskini. Ni katika hii hali ya uchumi ulioimarika ambapo wachina wameweza kupata huduma bora zaidi kutoka kwa sekta ya elimu, afya na hata biashara.

  Na tunapozungumzia hali ya biashara, hii ni eneo moja ambayo imeguswa pakubwa na sera hii kwani serikali ya Uchina ilikata shauri kufanya biashara na nchi za nje kiasi cha kampuni za kimataifa kama vile KFC na Starbucks miongoni mwa nchi zingine kuruhusiwa kuingia nchini kufanya biashara.

  Hatua hii imewezesha China kusaidia katika ujenzi wa uchumi wa dunia kando na uchumi wake. Ushirikiano na kampuni za nje pia imesaidia katika kuleta fursa za ajira nchini. Mwakani 2001 China pia ilijiunga na muungano wa biashara duniani yaani World Trade Organization kama ishara kamili ya jitihada zake kufanya biashara katika kiwango cha kimataifa.

  Miradi kama Ukanda mmoja Njia moja bado inaendeleza sera hii ya kufunguka kwa Uchina kwa kuleta ushirikiano wa kibiashara na miundombinu nan chi tofauti kote duniani.

  Chini ya uongozi wa Rais Xi Jinping sera hii pia imeifanya nchi ya China kuzingatia diplomasia iliyo na msingi wa urafiki bila kuingilia maswala ya ndani ya nchi geni. Kwa mfano barani Afrika, China imewekeza mabilioni ya madola ili maeneo haya mawili yaweze kusaidiana katika malengo yake ya maendeleo.

  Kupitia juhudi hizi China imewezakujenga reli ya kilomita mia saba hamsini nchini Ethiopia iliyogharimu takriban shilingi bilioni nne. Reli hii inawawezesha raia kusafiri kutoka Djibuti hadi Addis Ababa kwa masaa kumi na mbili, safari iliyochukua siku tatu hapo awali. Hii ni moja tu kati ya mamia ya miradi inayoendelea kutekelezwa kwa ushirikiano wa Uchina na nchi tofauti barani Africa.

  Rais Xi mwakani 2013 aliweka njia ya biashara almaarufu silk road inayosaidia katika kuiunganisha China na dunia nzima. Njia hii inajumuisha ujenzi wa reli, njia , mabomba na gridi. Mradi huu unategemea hela bilioni arobaini zilizotolewa na kwa shughuli hii.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako