• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • VIONGOZI WA AFRICA NA CHINA WAJADILI MBINU ZA KUKUMBANA NA UMASKINI

    (GMT+08:00) 2018-05-11 09:16:50

    Afrika ni bara zuri lenye mandhari ya kupendeza, watu wakarimu, tamaduni na mila za kufana na raslmani si haba.

    Licha ya kuwa na uzuri wa kupindukia, nchi tofauti barani zinakumbwa na umaskini unaowahangaisha raia katika sehemu teule za miji na mikoa. Umaskini umechangiwa pakubwa, ukosefufu wa ajira kwa vijana, ukosefu wa elimu bora, magonjwa na ufisadi.

    China kwa upande wake, licha ya kuwa na maendeleo makubwa ya kiuchumi, bado inakazi ya kuwanusurisha watu wapatao milioni thelathini ambao bado wanavumilia makali ya umaskini.

    Kama mbinu mojawapo za kuweza kuwashughulikia raia waliokatika kikundi hiki, serikali nyingi China na Afrika zimeiga mfumo wa serikali za ugatuzi zilizo na uwezo wa kuwashughulikia wananchi katika pembe zote za nchi.

    Viongozi wa China pamoja na viongozi wa nchi tofauti Afrika hii leo walijihusisha katikaa mazungumzo na majadiliano katika mkutano wa ushirikiano wa serikali gatuzi za China na barani Africa.

    Kulingana na Liu Yung Fu aliye waziri wa kikao maalum cha kupambana na umaskini na maendeleo , China ilichukua hatua mbalimbali zikiwemo kuhamisha watu maskini kutoka mazingira mabaya, kuendeleza sekta ya viwanda, kuwaelimisha raia kuhusu mbinu za kujitegemea, kushirikiana na mashirika kama muungano wa mataifa na kuzingatia mahitaji ya wananchi wa kawaida kabla lingine lolote.

    Ni kupitia miradi na mbinu hii, Bw. Liu alitangaza kwamba China imeweza kupunguza idadi ya watu wanaoishi katika hali ya umaskini kutoka milioni tisini na nane nukta tisa mwakani 2012 hadi milioni thelathini nukta nne sita sasa.

    Hata hivyo, alisema Bw. Liu, pambano dhidi ya umaskini haikuwa bila changamoto zake kwa mfano, ukosefu wa maendeleo mashinani ilhali kuna maendeleo makubwa mijini, zaidi ya watu milioni thelathini kuishi katika hali ya umaskini hata baada ya juhudu kubwa za serikali, China bado kuwa kwenye orodha ya nchi ambazo bado hazijaendelea kika licha ya mikakati kutiwa.

    Kama suluhisho China, chini ya uongozi wa rais Xi Jinping, inatilia mkazo maendeleo yanayo zingatia usawa na pia kufwata miradi na muelekeo wa Rais Xi kuhusiana na umaskini.

    Kwa vile pia Afrika pia inajikumbwa na taabu hii, viongozi walichukua wakati huu kuangazia mbinu wanazotumia kujinusuru makali ya umaskini.

    Nchi ya Afrika Kusini iliyowakilishwa na Bw. Obed Bapela, naibu wa waziri wa Uongozi na Maswala ya Utamaduni aliweza kuashiria kwa ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana kama moja wapo za sababu kuu za umaskini kati ya wananchi wa Afrika Kusini.

    Sababu nyingine ilyotajwa ikawa wananchi kuishi katika mazingira mabaya yasiyoruhusu kunawiri kwa juhudi za kuleta maendeleo.

    Ili kukumbana na shida hii serikali ya Afrika Kusini ilianzisha mfumo wa kuwasaidia wananchi walioathirika pakubwa na umaskini. Kupitia mradi spesheli kwa watu walioathiritha, wanawake maskini waliohitimumiaka sitini na wanaume walio hitimu miaka sitini na saba, watoto na viwete wanaisshi katika hali ya umaskini wanapewa hela na serikali. Hela hizi zinatolewa mara mbili kwa wiki, mara sita kwa mwezi au mara kadhaa kwa mwaka kulingana na mahitaji yao.

    Mradi huu unaowahusisha raia laki mbili, pia umewasaidia vijana kupata ajira kwa kuwapa kazi zinazo faidi nchi kama vile usafi wa mazingira, urekebishaji wa barabara zilizoharibika, kilimo na kadhalika. Masomo pia yanatolewa kwa vijana

    Bwana Bapela pia sema kwamba masomo yanatolewa kwa vijana ilikuwawezesha kupata ajira na kujipatia riziki itakayowabadilishia Maisha.

    Viongozi kutoka pande zote mbili walikubaliana kwamba ni muhimu kwa viopngozi wa Uchina na Afrika kufunzana na kuelimisha kuhusu mbinu tfauti za kuwainua raia wa kawaida.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako