• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ufunguaji mlango ulivyoendeleza China

  (GMT+08:00) 2018-05-21 09:59:51

  CHINA, nchi ya pili kwa uchumi bora duniani, mwaka huu unatimiza miaka 40 ya mageuzi na ufunguaji mlango--sera ambayo imeiwezesha taifa hilo kupiga hatua kimaendeleo na kuimarisha uwekezaji ndani na nje ya nchi.

  Kupitia kwa sera hii, makampuni mbalimbali yameweza kufungua matawi yake china na mengine yameweza kufanya kazi zao za uzalishaji nchini humo kutokana na mazingira mazuri na mfumo bora uliyowekwa na serikali.

  Sera ya mageuzi na ufunguaji mlango, pamoja na mambo mengine, yameiwezesha taifa hili la Asia ya Mashariki yenye idadi kubwa ya watu kupokea uwekezaji wa ndani wa kigeni katika viwanda mbalimbali vinavyozalisha bidhaa na kuuza ndani na nje ya mipaka yake.

  Kukua kwa uchumi wa China kupitia kwa sera hii ya mageuzi na ufunguaji mlango kumeiwezesha taifa hili pia kujihakikishia uchumi imara na kuifanya pia iwe na nguvu ya kifedha ya kuweza kuwekeza na kuendesha miradi mikubwa ndani na nje ya nchi.

  Nchi za Afrika, ukiachilia mbali mataifa makubwa kutoka mabara ya Asia, Ulaya na Amerika, moja kwa moja zimenufaika na zinaendelea kunufaika na mpango huu wa ufunguaji mlango.

  Maeneo mbalimbali ambayo Afrika ushirikiana na China ni pamoja na biashara, uwekezaji, afya, elimu, utamaduni, ujenzi na rasilimali watu.

  Kwa mfano hadi, mwaka jana, 2017, uwekezaji wa China barani Afrika umefikia dola za Kimarekani takribani bilioni 170 huku bidhaa zilizoingizwa nchini humo kutoka Afrika zikipanda kwa asilimia 32.

  Hii ni hatua nzuri na ya msingi sana katika shughuli za biashara na uwekezaji katika pande hizo mbili kwani uhusiano umejengwa katika misingi ya uwazi na kunufaishana.

  Wakati China ikiadhimisha miaka 40 ya ufunguaji mlango, taarifa zilizopo zinaonyesha kuwa mwaka jana, mchango wa taifa hilo katika uchumi wa dunia ulizidi asilimia 30.

  Kama hii haitoshi, China iko nyuma ya mradi wa mabilioni ya dola za kimarekani --Ukanda Mmoja, Njia Moja, ambayo kiuhalisia ni moja ya mikakati ya kuendelea kutekeleza dhana ya mageuzi na ufunguaji mlango.

  Huu mradi unaohusisha mabara matatu--Asia, Afrika na Ulaya utasaidia kuunganisha China, yenye idadi kubwa ya watu duniani na uwekezaji mkubwa nje ya nchi, na mataifa tofauti kutoka maeneo hayo kwa njia na namna mbaimbali ikiwemo reli, barabara na gridi.

  Wachambuzi wa mambo ya kiuchumi wanasema China imeweza kufanya mapinduzi makubwa sana kwa miongo minne, huku nchi hiyo ikizidi kujiwekea mipango mbalimbali ya muda mfupi na muda mrefu kufanya mapinduzi makubwa zaidi.

  Hadi sasa, kwa mujibu wa takwimu, ni Wachina milioni 40 pekee kati ya 1.4 bilioni bado wanaishi katika umaskini na taifa limejiwekea utaratibu wa kuwakomboa takribani milioni 10 kutoka kwenye umaskini kila mwaka.

  Hili linamaanisha ndani ya miaka minne hakutakuwa na umaskini nchini humo.

  Ni vema pia ikaeleweka kuwa pamoja na mbinu mbalimbai zilizotumiwa na taifa hilo katika kuhakikisha hii sera inafanikiwa lakini serikali imeendelea kusimamia baadhi ya sekta ikiwemo fedha, mawasiliano, nishati na vyombo habari.

  Zaidi ya ya hapo China imeweza kuwa na soko huria na watu kuwa huru kufanya biashara ndani ya nchi hiyo, huku wachambuzi wa uchumi wakisema soko huria litaendelea kukua zaidi ndani ya china kwa miaka ijayo.

  Pia uimara wa serikali na utulivu wa nchi umewezesha shughuli za kiuchumi kwenda vizuri.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako