• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwanadiplomasia maarufu atoa neno ushirikiano China, Afrika

    (GMT+08:00) 2018-05-21 10:00:24

    Bara la Afrika limeshauriwa kutumia vizuri fursa ya mahusiano yake na China ili liweze kutatua changamoto mbalimbali zinazolikabili na kujipatia maendeleo.

    Katika mahojiano maalum hivi karibuni jijini Beijing, Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Afrika, Dkt. Salim Ahmed Salim alisema Afrika ina kila kitu ambacho China inahitaji.

    Dkt. Salim ambae pia ni Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania na mwanadiplomasia maarufu alilitaka Afrika kuendelea kuwa na imani juu ya China wakati huu ambapo nchi hiyo inaendelea kufungua mipaka yake na kutekeleza diplomasia ya kiuchumi.

    China ni moja ya nchi kubwa duniani zenye mahusiano mazuri ya kidiplomasia na kibiashara na nchi za bara la Afrika. Kwa mujibu wa takwimu, uwekezaji wa China barani Afrika hadi mwaka 2017, ulifika dola za kimarekani bilioni 170.

    "Mpira upo kwetu, ni sisi wenyewe wa kuamua kutumia fursa hii au lah...Wachina na serikali yao hawana shida yoyote na Afrika, lazima tutumie vizuri hii fursa," alisema Balozi wa zamani wa Tanzania nchini China.

    China ilianzisha ushirikiano wake na bara la Afrika kuanzia miaka ya 1960 katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo katika sekta za afya, elimu, ujenzi, biashara na uwekezeaji, kilimo na utamaduni.

    Moja ya miradi mikubwa iliyofadhiliwa na serikali ya China katika bara la Afrika ni reli yenye urefu wa kilomita 1,860 inayounganisha nchi za Tanzania na Zambia, maarufu kama TAZARA.

    Dkt. Salim alisema China ambayo kwa sasa ni nchi ya pili duniani kwa uchumi mkubwa ina fursa nyingi ambazo bara la Afrika lazima ibadilishe namna ya kufanya mambo yake ili liweze kunufaika zaidi.

    "China imekuwa rafiki mzuri kwa Afrika kuanzia miaka ya 1960. Wametusaidia kipindi ambacho hata wao bado walikuwa wanapambana kujiletea maendeleo. Lazima viongozi wetu walitambue hili na kuhakikisha ushirikiano huu unahimarika," alisema Dkt. Salim.

    Kwa Tanzania, Dkt. Salim alisema Tanzania ina historia nzuri na China kuliko nchi yoyote Afrika na kuamini kuwa iko katika nafasi nzuri kuendelea kunufaika na uhusiano huo.

    "Dunia ya sasa ni ya utandawazi. Fursa zipo hivyo ni vema kwa Tanzania ambayo ina ushirikiano wa kihistoria na China kuongeza jitihada ili iweje kuendana na kasi ya dunia ili iweze kunufaika zaidi na ushirikiano wake na China." Alisisitiza.

    Dkt. Salim ambae amewahi kuwa mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa (UN) alisema China kwa sasa inatekeleza dhana ya uchumi wa kidiplomasia, hali inayozidi kutoa fursa kwa Afrika kunufaika maradufu.

    Dkt. Salim kwa upande mwingine pia alishauri viongozi wa bara la Afrika kuweka mifumo mizuri itakayoliweza bara hilo kuweza kusimamia vizuri rasilimali zake kwa faida ya wananchi wake.

    Alisema haileti mantiki kuona pamoja na kuwa na utajiri mkubwa wa rasilimali lakini nchi za bara la Afrika na wananchi wake wanaendelea kuishi katika dimbwi la umaskini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako