• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uhusiano wa China na Afrika chini ya Rais Xi Jinping

  (GMT+08:00) 2018-05-22 08:34:50

  Ni chini ya uongozi wa Rais Xi Jinping ambapo dunia imeweza kushuhudia hamu na mvuto mkubwa wa ushirikiano kati ya China na bara Afrika. Iwe ni ushirikiano katika biashara, elimu, ulinzi au sekta nyingine imekuwa wazi katika miaka miaka michache iliyopita kwamba uhusiano kati ya nchi za Africa na China unaendelea kuwa huku pande zote zikijitafutia maendeleo.

  Jambo hili limekuwa dhahiri kupitia matamshi ya hapa na pale ya Rais wa China Xi Jinping kwa mfano mwezi Aprili aliposema kuwa China na bara Afrika zinajukumu kubwa la kutumia maeneo yao ya nguvu kustawishana. Rais Xi aliyasema haya katika mapokezi rasmi ya Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangangwa mjini Beijing.

  Kufunguka na kushirikiana na Afrika ni sehemu kuu ya sera za China zinazoipa kipaumbele uhusiano mwema unaohakikisha mazao mazuri kwa maeneo yote mbili. Baadhi ya vipengele vya sera za China kuhusu Afrika ni kuhakikisha uhusiano mwema iliyona misingi ya heshima na amani, kutoingilia maswala ya ndani ya nchi za Afrika , umoja na ushirikiano kati ya Afrika na China na hata kuisaidia bara Afrika kuwa na sauti katika jamii ya kitaifa.

  Ni katika muongozo huu ambapo China na Afrika zitakuja pamoja katika mkutano wa kitaifa almaarufu FOCAC mjini Beijing mwezi Septemba mwaka huu.

  Ni katika mkutano huu ambapo viongozi wa China pamoja na viongozi kutoka kote barani Afrika watakuja pamoja kujadiliana kuhusu jinsi kufinguka kwa China kunaweza kutumika kama nguzo ya maendeleo ya kiuchumi kwa pande zote na urafiki.

  Wito huu wa uhusiano mwema kati ya maeneo haya mawili uliungwa mkono na mwenye kiti wa baraza la magavana nchini Kenya Bw. Josephat Nanok aliyeunga mkono juhudi hizi kwa kusema kwamba viongozi wa kila nchi barani Afrika inastahili kutambua maeneo ya taifa yanayohitaji maendeleo iliwaweze kuipa nafasi kubwa katika majadiliano ya ushirikiano. Alisema ni dhahiri kwa serikali za Afrika kuhakikisha kwamba ushirikiano wa aina huu ni wa faida kamili kwa raia.

  Bwana Nanok alikuwa akizungumza mda mfupi tu baada ya tetesi kuzuka nchini Kenya kuhusu malengo ya wafanyi biashara wa Kichina nchini Kenya huku kampuni za China zikiongezeka kila kuchao.

  Jambo hili pia lilizungumziwa na Mkurugenzi mkuu wa kitengo cha maswala ya Afrika cha wizara ya maswala ya nje Bw. Dai Bing katika mkutano na wanahabari wa Afrika. Bw. Dai alisisitiza kwamba ni dhahiri kwa migogoro au shida zozote kati ya Wachina na Waafrika kutatuliwa kama shida zinazotokea kati ya familia kwani urafiki kati iya pande zote mbili lazima utunzwe.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako