• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tuzo zatolewa kwa hadithi za Wakichina kuhusu Afrika

    (GMT+08:00) 2018-05-25 14:12:49

    Waandishi waliotoa taarifa za kufana kuhusu wakati wao barani Afrika walipata kutuzwa hapo jana iliadhimishwa hapo jana katika sherehe ya kupendeza katika chuo kikuu cha lugha na utamaduni cha Beijing.

    Mashindano hayo yalihitaji wachina wanaoishi au walioishi barani kwa sababu ya kazi na majukumu mengine kuhadithia maisha yao barani.

    Hii ilipelekea washindani zaidi ya elfu moja kutuma taarifa zao huku wengi wakitumia fursa hiyo kudokeza mambo yaliyowagusa na kuwabaki akili milele.

    Ni kupitia fursa hii wachina mitandaoni waliweza kusoma na kujifunza mengi kuhusu uzuri wa Afrika, wengi walizugumzia mandhari mazuri ya bara Afrika, wanyama pori, ukarimu wa Wanaafrika, undugu na ubora wa kuishi barani.

    Hafla hii kama alivyosema Bw. Chen Xiaodong wa idhaa ya CRI, ilikuwa ishara dhabiti ya ari kuu ya Wachina kufanya kazi pamoja na wanaafrika na akawarai wadau kuunga mkono juhudi kama hizi zinazoimarisha urafiki kati ya Wachina na watu kutoka tabaka mbalimbali Afrika.

    Pia hakusita kusifia umahiri wa filamu za kuchina barani Afrika nyingi zikiwa zimetafsiriwa katika lugha za kiafrika kama vile kiswahili, hausa na kadhalika.

    Takwimu zinaonyesha kwamba maandishi haya yaliweza kuleta wasomaji wapatao laki mia tisa, na wapatao watu mia mbili hamsini elfu walipigia kura hadithi, picha na video zilizowapendeza.

    Ni muhimu ikumbukwe kwamba hadithi hizi ziliandikwa na watu wa kawaida ambao wanahaja ya kutoa ukweli wao kuhusu China kwa dunia nzima. Hii inasaidia pakubwa katika kujifunza kuhusi tabia, tamaduni na hata mahitaji yetu sote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako