• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Daraja Kuu La Zhuhai, Makau na Hongkong

  (GMT+08:00) 2018-06-27 09:14:12

  Na Trix Ingado Luvindi

  Mradi wa njia moja ukanda mmoja ina nia ya kuunganisha China na sehemu nyingi za dunia nzima. Hii itaweza nchi hii kujiimarisha kiuchumi kwa kupitia ujenzi wa barabara , reli na pia mabandaro katika nchi mbalimbali.

  Ukubwa wa mradi huu unaonyesha imani ya nchi hii katika kuweka miundombinu za usafirishaji zitakazofanikisha biashara.

  Juhudi hizi za kujiimarisha katika sekta ya usafiri ilikukuza uchumi zinaonekana pakubwa mkoani Guangdong ambako serikali za maeneo ya Macau, Zhuhai na Hongkong yamekuja pamoja katika ujenzi wa daraja kuu linaloziunganisha sehemu hizi.

  Kulingana na Bi. Evelyn Tang ambaye ni naibu msimamizi wa mamlaka ya daraja hilo alisema kwamba dhana ya ujenzi ilipendekezwa na mfanyi biashara zaidi ya miaka kumi iliyopita ila haikuonekana kama hitaji la dharura kwa wakati ule.

  "Ila wakati wa hali ya uchmi ilipozoroteka mwakani 1997 ikawadhahiri kwamba daraja lili lilikuwa muhimu kwa wenyeji ilikuwawezesha kuendeleza shughuli zao za biasha zitakazo leta utulivi katika uchumi wa eneo ile", kasema Bi Tang.

  Ujenzi wa daraja ukang'oa nanga mwakani 2012 na kugharimu mabilioni ya dola za marekani huku , wataalamu na wahandisi wakilazimika kubuni njia spesheli zitakazo wawezesha kujenga daraja la kilomita sitini na mbili majini.

  Ili kutimiza lengo la kuunganisha pande zote mbili za Pearl River Delta , ujuzi ulihitajika kwa sababu maji yalisababisha changamoto si haba.

  Changamoto ya kwanza ilikuwa kuendeleza ujenzi bila ya kuchafua maji au kuhatarisha maisha ya samaki majini haswa wa aina ya White Dolphin.

  Ili kuhakikisha uwajibikaji, serikali ikaweka kikundi cha wataalamu wa mazingira ambao walitarajiwa kufanya kazi kwa karibu na wajenzi . Timu hii iliwaelimisha na kuwasaidia kuendeleza shughuli hii muhimu wakizingatia kwa makini usafi wa mazingira. Juhudi hii inasemekana kusaidia pakubwa katika kudumisha mazingira yale kwani utafiti ulifanywa na kikundi kile kikawa kinakusanya takwimu za samaki majini ili kuhakikisha wako salama.

  La pili lilikuwa umbali wa maeneo yale mawili. Ili kuipa daraja ile msingi bora, ujenzi haungefanya kama kawaida. Wahandisi wakakata shauri kujenga visiwa vitatu bandia majini vitakavyosaidia kuimarisha daraja.

  Nguzo pia zilitakiwa kutiwa chini ya darajakwa sababu ileile. Lakini kwa vile ni vigumu kujenga nguzo kwenye mchanga wa bahari, ikawa dharihi kwamba lazima wachimbe na kuingiza matanki makubwa hadi kwenye sakafu la bahari. Matangi yale kisha yakajazwa na mchanga uliokuwa msingi wa guzo zilizojengewa daraja hatimae.

  La tatu, ilikuwa muhimu kuwa ujenzi huu hauingilii shughuli za bandari , meli na ndege zizinazotoka au kupitia Makau , Zhuhai na Hongkong. Hii ikawalazimu wahandisi kukarabati mpango uliyoifanya daraja kuchukua mkondo mrefu uliogharimu na kuhitaji rasilmali zaidi.

  Katika sehemu moja , ilibidi daraja lile lipititishwe china ya maji ya bahari umbali wakilomita sita na nusu ili lisizuie meli katika zinazopitia sehemu hiyo.

  Nne, ili kuhakikisha daraja hili litadumu licha ya dhoruba na mawimbi ya bahari ambayo huwepo katika maeneo haya. Ikawa lazima watupilie mbali ujenzi wa kawaida wa simiti na kutumia vyuma. Ila vyuma hushika kutu majini haswa ya chumvi.

  Changa moja hii ikaondolewa kwa kutumia vyuma spesheli ambavyo havishiki kutu almaarufu stainless steel.

  Inakisiwa daraji hili itafunguliwa rasmi mwakani humu. Hii ni baada ya kazi , utafiti , uvumbu na gharama kali. Wataalam wanasema daraja hii itakuwa daraja ndefu zaidi kupitia majini dunia nzima.

  Lakini je? Shughuli hii yote ni ya manufaa gani?

  Ni tumaini la uongozi wa maeneo haya matatu kwamba kukamilishwa kwa daraja hili kutawawezesha wenyeji kuwa na uhuru wa kusonga na kufanya biashara bila wasiwasi kuhusu umbali.

  Itachukua dakika thelathini tu kuvuka kutoka upande mmoja hadi mwingine. Hii itarahisisha shughuli za biashara. Hii itasaidia kukuza uchumi wa eneo hizi huku ubora wa maisha pia ukiongezeka.

  Biashara za mitandaoni pia zinatarajiwa kuimarika kwa sababu itakuwa rahisi kufikisha bidhaa kwa wanunuzi safari ikiwa ni ya barabara wala sio ya majini.

  Daraja liligharimu dola bilioni nane nukta nne na linatarajiwa kudumu Kwa mda wa miaka mia moja ishrini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako