• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • CCM na CPC yakutanisha vyama vya siasa Afrika kujadili ushirikiano wao na China

  (GMT+08:00) 2018-07-16 09:16:06


  Na Theopista Nsanzugwanko

  JULAI 17 na 18 mwaka huu, mahusiano ya China na Afrika yanajikita katika awamu mpya ya kihistoria katika mahusiano ya vyama vya siasa ambavyo ndiyo zinaongoza serikali za nchi mbalimbali.

  Mahusiano hayo mapya ya kihistoria yatafanyika nchini Tanzania katika jiji la Dar es Salaam kwa kuweka wazi mahusiano ya kina ya kidiplomasia kwa kushirikiana kuandaa na kufanya mkutano wa Kidunia wa Vyama vya Siasa, Kikao Maalum cha Afrika, Jijini Dar es Salaam.

  Mkutano huo utakaoshirikisha vyama vya siasa 38 kutoka Afrika na kuhudhuliwa na washiriki 130, umeandaliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwenyeji wa mkutano huo kwa kushirikiana na Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC).

  Inaelezwa kuwa mkutano huo ni sehemu ya matokeo ya utendaji kazi wa uongozi wa serikali ya awamu ya tano ya Chama na Serikali chini ya uongozi wa John Magufuli.

  Mkutano huu wa kihistoria ambao ni wa kwanza kufanyika Barani Afrika, unakuwawa pili kufanyika ukitanguliwa na ule wa awali kufanyika Beijing, China Disemba mwaka jana.

  Mkutano wa awali uliongozwa na Rais wa China ambaye ni Katibu Mkuu wa CPC, ukiwa na mada kuu ya Juhudi (vitendo) na Nadharia za Vyama vya Afrika na Chama Cha CPC katika kufanya uchaguzi wa njia sahihi za kujiletea maendeleo na zinazoendana na mazingira ya nchi za Afrika.

  Katika mkutano huo wa kihistoria utadhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama CPC, Song Tao na Makamu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa CPC, mwenyeji wa Mkutano huo Rais John Magufuli anatarajiwa kuzungumza katika mkutano huo utakaofanyika Julai 17 hadi 18 mwaka huu

  Wazo la Mkutano huu wa kidunia linatokana na fikra za Katibu Mkuu wa CPC, ikiwa na mapendekezo ya mwelekeo mpya wa kuenenda kidunia na kutaka kujenga jamii yenye mwelekeo wa pamoja hapo baadaye na kufanya kazi kwa pamoja ili kujenga dunia na kusababisha kuwepo kwa majadiliano ya kidunia kati ya CPC na vyama vya siasa duniani.

  Nchi ya China ikiwa inatimiza miaka 40 mwaka huu ya kufanya Mageuzi na Kuchangamana Kimataifa, mkutano huo utakuwa mwelekeo wa Kongamano la ushirikiano wa China na Afrika (Forum on China-Africa Cooperation – FOCAC) litakalofanyika jijini Beijing, China baadaye mwaka huu.

  Tanzania, Afrika na China katika Mkutano huo watajikita katika mjadala mpana na wa kina wa kuangazia changamoto na fursa lukuki zitokanazo na kujengeka zaidi kwa mahusiano na mashirikiano ya Afrika na China

  China ikiongozwa na CPC na Tanzania ikiwa chini ya usimamizi wa chama cha CCM vina itikadi ambayo inatoa mwelekeo wa Sera za China na Tanzania, Mataifa haya mawili yanaamini katika Itikadi ya Ujamaa. China imeongozwa kwa mafanikio kwa zaidi ya miaka 40 sasa na Siasa na Itikadi ya Ujamaa wa Kisayansi ambao unashajihishwa na tabia ya Taifa la China "Socialism with Chinese characteristics".

  Itikadi ya Ujamaa ndio imewezesha mafanikio ya Mageuzi na Mapinduzi makubwa ya kimfumo, kiutendaji, kiuongozi, kiuchumi na kisiasa ambayo Taifa la China limeyatenda katika kipindi hiki za miaka 40, huku kwa sasa imeanza awamu mpya ya Mageuzi na Mtangamano wa Kimataifa na inaweka jitihada kubwa kufikia lengo la kujenga Taifa la kijamaa la kisasa na imara ifikapo mwaka 2050.

  Wakati China inaweka malengo haya makubwa ifahamike kwamba Bara la Afrika likiwa mojawapo ya mabara yanayokua haraka kiuchumi, kwa idadi ya watu, utangamano na uwezekano mkubwa wa uchumi wake kukua kwa faida na tija duniani huku Afrika ikijitoa kuhakikisha inafikia Mapinduzi makubwa ya kiuchumi na kujitengenezea njia yake ya kukua kulingana na mazingira ya Afrika "exploring independent path of modernisation".

  Ikiwa na lengo moja la kushughulika na shida za wananchi wake, CPC ipo tayari kuimarisha utaratibu wa kubadilishana taarifa, maarifa na watu pamoja na vyama vya siasa vya Afrika ili kujenga jamii ya pamoja ya Afrika na China na yenye lengo la pamoja kuhusu maisha bora ya sasa na ya baadaye kwa watu wetu.

  CPC na CCM pamoja na vyama vyote vya siasa vitakavyoshiriki vitakuwa na majadiliano ya kina na ya kweli huku wakikubadilishana taarifa na maarifa mbalimbali, ikiwemo Majukumu ya kimaendeleo na machaguo ya njia za kujiletea maendeleo kwa China na Afrika", "Fursa zilizopo na Changamoto za Mashirikiano ya Afrika na China" na "Wajibu wa vyama vya siasa katika ujenzi wa maendeleo ya kitaifa na mashirikiano baina ya China na Afrika".

  Mada hizo zitalenga kutoa hamasa katika jitihada za Afrika na China katika kuchagua njia sahihi za kukua, kujiletea maendeleo, kupendekeza programu ya vyama vya siasa katika Kongamano la Ushirikiano wa China na Afrika litakalofanyika Jijini Beijing na kujenga uelewa wa pamoja na hoja katika Ubia wa Kimkakati kati ya Afrika na China na hasa katika kipindi hiki kipya.

  Mkutano huu utakuwa fursa kwa Tanzania kukumbusha na kusisitiza msimamo wake katika diplomasia ya kisiasa na kiuchumi na hasa katika uongozi wa awamu ya tano ambayo imejikita katika kutimiza wajibu wa kizazi cha sasa wa kulikomboa bara la Afrika na Tanzania Kiuchumi ili kuleta maendeleo ya haraka kwa watu wake.

  Katika kwenda sambamba na utenda kazi wa chama cha CPC cha China katika kushughulikia shida za wananchi wake, pia nchini serikali ya CCM imejikita katika ameneo hayo kwa kuimarisha nyanja zote za kiuchumi na kijamii.

  Hatua hiyo imekwenda sambamba na kuimarisha nidhamu ya viongozi na watumishi wa umma, kuweka nidhamu katika makusanyo na matumizi ya fedha za umma, kuongeza uaminifu, uadilifu, uchapa kazi, kuongeza mapambano dhidi ya rushwa na vitendo vya ubadhirifu wa mali za umma na uhujumu uchumi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako