• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Oriental Pearl TV Tower

  (GMT+08:00) 2018-07-17 14:25:25

  Oriental Pearl TV Tower ni mojawapo ya majengo marefu barani asia.Jengo hili la kupendeza lipo mashariki mwa mto wa Huangpu mjini Shanghai. Likiwa na urefu wa mita mia nne sitini na nane, jengo hili linatembelewa na mamilioni ya watalii kutoka China na sehemu zote za dunia. Watalii hao humiminika jengoni usiku na mchana wengi wakitaka kushibisha ari ya kuyaona mandhari mazuri ya Shanghai kutoka angani.

  Inasemekana kuwa mnara huu wa mawasiliano unaotegemewa na stesheni za radio na televisheni ni mrefu kuliko zote barani asia na wa tatu katika urefu wake duniani. Mbali na kujionea mji katika umbali wamita mia mbili sitini na tatu, mle ndani mna maenyesho ya kihistoria , burudani na hata duka za kujinunulia pipi , vinywaji na vitafunio.

  Wengi hupendezwa pia na hoteli iliyoko katika umbali wa mita mia tatu sitini na moja. Hoteli hii inamadirisha makubwa ya glasi na pia huzunguka iliwatalii waweze kuona pande zote za mji huku wakila. Kama hujatosheka unaweza kupata kutembelea makavazi ya historia ya Shanghai yaliyotengenezwa mlemle. Makavazi hayo yametengenezwa ili yafanane na mitaa ya Shanghai katika enzi za kikoloni. Unapotembea mle , unaweza kupata taswira ya majengo yaliyojengwa na waingereza katika mitindo yao.

  Pia unaweza kupata maelezo kuhusu maisha ya wenyeji kama vile walivyo tafuta riziki, mitindo ya mavazi na jinsi walivyoishi na waingereza miongoni mwao. Kwa ujumla, Shanghai inamaeneo mengi ya kupendeza na mgeni hawezi kukosa pakuenda. Mbali na Oriental Pearl Broadcasting and Television Tower unaweza kutembelea maonyesho yakitamaduni ya The Bund, eneo la The People's Square, majengo ya Jin Mao Tower Shanghai tower na Shanghai Xintiandi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako